UmkhontoweSizwe
Platinum Member
- Dec 19, 2008
- 10,046
- 9,344
Juzi nimeenda benki kwa nia ya kutuma pesa kidogo kwenda US lakini masharti niliyoyakuta huko sikuamini. Kwanza, Nikaambiwa kama natuma fedha kwa madhumuni ya kibiashara ni lazima nipeleke pro-forma invoice. Nikashindwa kuelewa. Pro-forma invoice ya nini wakati mimi sifanyi manunuzi yoyote ya kiserikali? Mimi siyo taasisi au kitengo cha serikali bwana. Mliwaacha kina Chenge wakanunua ndege ya serikali kwa pro-forma invoice za kughushi mnakuja kutubana sisi watu binafsi?!
Pili, nikaambiwa kama natuma kwa mtu binafsi lazima nilete barua toka kwa mtu ninayemtumia kuonyesha kuwa anahitaji pesa. Kama ni mwanafunzi basi barua itoke shuleni kwake, I-20 yake, Visa etc.
Goooosh, yaani masharti mengine hayana hata msingi. Personal issue yangu mpaka nikawatangazie watu waandike barua! Yaani pasa yangu, kuitumia mpaka Benki Kuu watake! Upuuzi wa hali ya juu. Wamezoea enzi za ujamaa wanadhani dunia bado imesimama kuwasubiri wao na sera zao zisizoleta ufanisi wowote. Nikihamisha akaunti yangu kupeleka Kenya ambako hakuna masharti watu wataniona siyo mzalendo. Lakini sera zetu zinakirihisha na kukatisha tamaa.
Benki Kuu: Fungueni milango itakayohamasisha watu kuingiza $$ zaidi nchini, badala ya kubana njia za kutumia ili kulinda tu kidogo kilichopo. Hizo sera zimepitwa na wakati.
Ombi: jamani nahitaji kutuma $$ kiasi kwenda US. Kama kuna mtu anajua njia nzuri na salama, tafadha naomba un-PM, I'll contact you. For those in the US, I can give the money here (Bongo), and you deliver the same amount to my colleague in the US. He needs money before Thursday next week.
Note: Ni kwa shughuli ambayo ni LEGAL, so shouldn't have to worry.
Thanks in advance.
Pole sana ndugu yangu, lakini utaratibu huo ni wa Dunia nzima bwana . Siku hizi kuna ukiritimba karibia kila sehemu kwa kisingizio cha Hela chafu, kitu cha msingi atokee mdau ambaye ataokoa jahazi kwa US the wewe unaweza kuwapa labda familia yake itakuwa imesaidia. Ila jaribu Western Union inaweza kuwa nafuu sina uhakika lakini nafikiri kuna nafuu.

I think, they were right!This was done in good faith!remember there is world convention on fighting against money laundering!again there is issue of controlling inflow and outflow of foreign exchange currencies!It is reality,they were trying to exercise duties and responsibilities.There is nothing new here!don't complain!
Ana lake jambo!!!! Ukimchunguza sana utaona ni mpinzani wa serikali ya ccm, hivyo anataka kuwaambia wananchi kuwa serikali ya ccm imemzuia kutuma pesa nnje, maana kashaanza na kumtaja chenge.
Ilichofanya BoT ni kuepuka uwezokano wa wewe kutuma pesa kwa matumizi mabaya.
Pole sana ndugu yangu, lakini utaratibu huo ni wa Dunia nzima bwana . Siku hizi kuna ukiritimba karibia kila sehemu kwa kisingizio cha Hela chafu, kitu cha msingi atokee mdau ambaye ataokoa jahazi kwa US the wewe unaweza kuwapa labda familia yake itakuwa imesaidia. Ila jaribu Western Union inaweza kuwa nafuu sina uhakika lakini nafikiri kuna nafuu.
Asanteni kwa mliotoa maoni na ushauri. Nakubaliana na wazo zima la kupambana na pesa chafu, laakini si kweli kwamba huo ni utaratibu wa dunia nzima. Nimekaa nje ya nchi yetu, na nimewahi kutuma pesa kuja TZ mara nyingi. Hakuna mahali popote ambapo nimewahi kupata usumbufu wa aina hii. Nimetuma kwa kutumia banks mbalimbali, na kwa wire transfer, hata kutokea US, hakuna mizengwe ya aina hiyo. Hata Kenya tu nasikia hawana usumbufu wa aina hii.
baba mtu, nimeshangazwa na maoni yako kwa sababu badala ya kujadili hoja ya msingi wewe umejadili illustration, .......funny!
"Ukiritimba" ni sawa na "monopoly" kwa Kiingereza. Labda ulimaanisha "urasimu" (kwa maana ya "bureaucracy"?)Re: Benki kuu: ......................sera za ukiritimba zitatumaliza