oopps usitaje akiba bank ni kimeo fulu. nitatiririka hapa kama watabisha au kama kuna atakaewatetea.mathematics hukukosea kujiita jina hilo.
NMB wapo vizuri, matawi hadi vijijini, ATM za kutosha, huduma zao pia zimeboreshwa, msongamano wa wateja umepungua baada ya kuongeza matawi zaidi. Hasara yao hawana huduma ya visa card/ master card.
CRDB na wanayo matawi mengi ila hawawazidi NMB, na wenyewe wapo vizuri ila nahisi kwa sasa ni kama vile wamezidiwa wateja, foleni zimezidi zile za NMB hata huduma ya kastama kea sio nzuri tena sababu ya wingi huo wa wateja. Faida yao wana visa / master kadi .
NBC sijawahi kabisa kuwa na akaunti hii benki, sababu sijawahi vutiwa na chochote kweny hii benk, hata hivyo inayo matawi machache na ATM chache kulinganisha na CRDB au NMB. Faida yao pia wana visa/master card.
Vilevile hapo ulipo kama kuna hiz benk ndogo AKIBA bank ,AZANIA bank etc ni nzuri sababu ya uharaka wa huduma zao. Faida yao pia wanatoa mikopo kwa urahisi sana hizi benk ndogo kulinganisha na hizo bank kubwa hapo juu. Hasara wana matawi machache pia na nyingi hazina VISA/ Master kadi.
uzoefu wangu kwa bank hizo ni huo, watakuja wengine kukujuza kuhusu stanbic, standard charted , braclays exim , etc
Makato ya ATM ni lazima sidhan kama kuna benk haichaji kutoa pesa kwenye ATM , pia makato mengine ni ya kila mwezi ya service charge ambayo nayo ni lazima. saving akaunti makato ya kila mwezi ni kidogo kuanzia tsh600, current yanaanzia 5000tsh.
Asante sana 'mathematics'.
Ninaona CRDB watanipa advantage ya MasterCard, otherwise NMB wapo vizuri. Labda NMB wataleta MasterCard/VISA in the future.
Asante sana.
Amani kwako!
Nataka kufungua account mpya bank, ila naomba nipate ushauri kutoka kwa watu wa profession ya mambo ya banking, kwamba ni benki gani na aina gani ya account nikifungua itakuwa vyema zaidi. Kwa sasa hivi najishuhulisha kwa kazi za kujiajiri mwenyewe, hivyo nikiwa account hii itakuwa ni kwa ajili ya kujikusanyia kile ninachopata kwa kushuhulika huko. Ninaweza nikawa nakusanya humo kwa lengo kuwa kikifika kiwango fulani nikitoe nikipeleke kwenye project nyingine.
Ninajali sana mambo ya makato ya mwezi na ATM charges. Kwa ujumla, najali sana taratibu za bank ambazo 'zinakula' hela yangu humo kama mchwa.
Nadhani kuna mambo mengine pia natakiwa kujali, naomba kuelimishwa. Kisha naomba nishauriwe ni benki gani nzuri na accounts zipi.
Ninaamini hapa watakuwepo watu wenye elimu au uzoefu juu ya hili na nitashukuru kwa elimu hiyo. Lengo langu ni kama nilivyojieleza hapo juu.
Otherwise, M-PESA na Airtel Money ndiyo zili-replace CRDB na NBC kwangu!
Asanteni.
mimi nabiisha na naitetea Akibaoopps usitaje akiba bank ni kimeo fulu. nitatiririka hapa kama watabisha au kama kuna atakaewatetea.
Kama unajali sana cost NMB wapo vzr na watakufaa kuhusu visa na masttercard kwa mtu kawaida haina faida yoyote mi nimekuwa na visa card 4rm 2010 na master card lkn sijawahi zitumia, fungua account NMB huta regret kwa makato ya ajabu ajabu
Kwa kuongezea walau kwa uchache tu pale alipoishia mathematics, Kuna benki nyingine kama Mkombozi Commercial Bank, FBME, BancABC, Access Bank, DTB, Eco Bank, FNB, FINCA, Maendeleo Bank, Tanzania Women Bank, Covenant Bank, Efatha Bank na nyinginezo, hizi ni benki ndogo kwa maana ya matawi. Na faida kubwa ya hizi benki ni uharaka wa huduma na urahisi wa kupata mikopo.
Uzoefu unaonyesha benki ndogo ziko effective sana linapokuja suala zima la huduma ukilinganisha na hizi kubwa kubwa. Mengine yameshaongelewa.
Ushauri: Fungua account kulingana na unyeti wa shughuli zako. Kama utakuwa unaitumia account hiyo countrywide ni bora kuangalia benki hizi kubwa zilizoainishwa na Mathematics hapo juu ila kama misele yako inaishia Chalinze nakushauri uangalie uwezekano wa kufungua account kwenye hizi benki ndogo ambazo nyingi zina matawi hapa Dar.
Wasalaaaam
nmb fungua bonus account
ukitaka kumwaga machozi nenda BArclays,huduma mbovu,mbovu tena mbovu kuliko maelezo,mim nimetoka kuclose akaunti yangu huko hivi majuz tena mbaya zaidi wakanidai 40 elfu kama fee ya kufunga akaunti hiyo....nilichoka.Nenda BARLCLAYS
Nenda BARLCLAYS