Benki gani YAFAA Tanzania?

Rock City

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,266
501
Salaam wakuu,

Kwa wale wazoefu, naomba msaada wa kujua yafuatayo ili kunisaidia katika nikusudiayo kuyatekeleza.

1. Ni benki gani nzuri Tanzania kwa huduma za kampuni binafsi, kwa huduma za kikampuni?

2. Ni benki gani ambayo mimi kama mteja mwenye kampuni nikaitumia kwa huduma za kawaida, na ambayo, iwapo nikapata mradi mkubwa katika biashara zangu wakaweza kunisaidia mkopo wa haraka katika kuutekeleza na kuufanikisha mradi niliopata mkononi.

3. Ni benki gani ambayo inaweza kunihudumia mimi kama kampuni na ambayo inaweza kutoa huduma za O.D (Over Draft), na taratibu zao zikoje?

4. Kwa aina ya frauds na theft ilivyo katika mabenki yetu, ni benki gani itakayonisaidia kuhudumiwa kwa usalama na usalama wa amana niliyoikabidhi benki husika kunihifadhia?

Kwa hayo, natanguliza heshima mbele na naomba msaada wa kuelimishwa na kueleweshwa juu ya yote hapo juu.

Wasalaam,

R.C
 
Mi kampuni yangu inatumia EXIM...iko pouwa sana nenda kwenye branch utapataa details zake, No Q et al
 
Benki nyingi za kitanzania wakisha kukopesha kusudi upambane na umasikini wao wanajitayarisha kupambana na masikini huyo aliyekopa. Wanaanza kutishia kuuza kila kitu chako ulichonacho kisa umechelewesha tu lejesho. Hakuna benki yoyote duniani kwa ajiri ya kumsaidia masikini. Hata world Bank nao wako hivyo. Ogopa benk ndg yangu
 
Ahsante kwa maoni, mawazo na ushauri mzuri juu ya hili rushanju
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom