Benk Kuu ya Tanzania, BoT imeiunganisha Benk ya Twiga Bancorp na Benki ya Tanzania Postal Bank

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Benki kuu ya Tanzani BOT imeamua kuunganisha Benki ya Twiga Bancorp na Benki ya Tanzania Postal Bank Public limited Company TPBPLC.

Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Dokta. Bernard Kibesse amesema benki hiyo ya Twiga Bancorp iliyokuwa chini ya usimamizi wa benki kuu kwa sasa imeunganishwa na benki ya posta na kwamba utekelezaji wa hatua hiyo unaanza mara moja Mei 17 mwaka huu ambapo mali za wateja na madeni ya benki hiyo sasa yatasimamiwa na benki ya Tanzania Postal Bank Public Limited Company.

Dokta Kabesse amesema baada ya kuuganishwa huko anategemea kutakuwa na ufanisi mkubwa katika utendaji kwa wateja wa benki hiyo.

Kwa upande wake meneja uendeshaji wa bodi ya bima ya amana Bi Rosemery Tenga amewataka walikuwa wateja katika benki ambazo zipo chini ya BOT kufuati mitaji ya benki hiyo kuyumba kwenda katika benki hizo na utaratibu wa malipo utafanyika chini ya usimamizi wa bodi ya amana.

ITV
IMG-20180516-WA0016-1.jpg
 
Hata Postal Bank nayo siamini kama utendaji kazi wao unaridhisha.
My take: Bei za bidhaa kibao ziko juu kama sukari, mchele, maharage na bidhaa nyingine za vyakula huku mazao ya wakulima huko vijijini yakiuzwa kwa bei ya chi mbaya zaidi hata wakulima wa kahawa hawaruhusiwi kuanza kuvuna kahawa zao mpaka wapate kibali kutoka serikalini, kwahiyo savings kwa wanachi ziko down, mabenki mengi yako kwenye msoto, hali hii isipo dhibitiwa mdororo wa uchumi umeshalinyemelea taifa.
 
Sina shaka BoT wanatakuwa wamefanya a proper due diligence on both Banks kabla ya kuchukua uamuzi huu otherwise inawezaleta shida hapo baadae. Ila from banking profession perspective barua ya Deputy Governor inaonyesha mapungufu kuhusu uelewa wa hizi terminologies za Mergers and Acquisitions
Kilichofanyika hapo ni Bank Acquisition na sio Bank Merger.. Anyway 'the end justifies the means'.....
 


Wawe wakweli tu hali ni tete na si vinginevyo.

Tanzania inaingizwa shimoni! Nani ataiokoa Nchi hii iliyokuwa imefika pazuri katika awamu zilizopita japo kulikuwa na changamoto kiasi! Mwelekeo wa uchumi ulikuwa mzuri lakini sasa tuna Viongozi wasiojua lolote kuhusu Uchumi wa Dunia unavyo- operate! Rais Magufuli aambiwe ukweli kuwa tunakubali anayo nia njema na Nchi hii lakini NIA si UWEZO! Miradi mikubwa aliyoingiza Nchi kama SGR,Stiglers Gorge na Ununuzi wa Ndege kwa pesa za Ndani utauwa Uchumi Mchanga wa Nchii hii! Mwinyi,Mkapa na JK wapi Wazee wetu ! Nchi inaelekezwa Shimoni huku mnatazama kimya! It's unfair okoeni Jahazi linazama!
 
Back
Top Bottom