Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,963
- 30,311
BENJAMIN WILLIAM MKAPA MHARIRI WA ‘’UHURU’’ NA ‘’THE NATIONALIST’’ KATIKA MGOGORO WA EAST AFRICAN MUSLIM WELFARE SOCIETY (EAMWS) 1968
Katika utafiti wakati naandika historia ya TANU kupitia maisha ya Abdulwahid Sykes nilipewa faili lililokuwa na nyaraka ambazo zilihifadhiwa kwa kificho na Bilal Rehani Waikela kwa miaka kama 20 hivi.
Hizi nyaraka zilikuwa zinataarifa ya mgogoro wa iliyokuwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa ikishughulika na maendeleo ya Waislam wa Afrika ya Mashariki.
Waikela akiwa kiongozi wa EAMWS Tabora alichaguliwa kuwa katika Tume ya Kwikima iliyoundwa kutafuta sulhu ya mgogoro ule.
Sulhu haikupatikana na serikali ikavunja EAMWS na kuunda BAKWATA.
Baada ya kuvunjika kwa EAMWS zikasikika taarifa kuwa yeyote katika wajumbe wale ataekutwa na nyaraza zozote za mgogoro wa EAMWS atakamatwa.
Waikela alipopata taarifa hii yeye akazihamisha nyaraka zake nyumbani kwake akaenda kuzificha mahali pengine salama.
Baada ya miaka mingi kupita hizi nyaraka (mimi katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) nimezipa jina, ‘’Nyaraka za Waikela’’), Waikela alizifikisha kwa wanafunzi wa Kiislam wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wazitunze katika maktaba yao.
Hivi ndivyo mimi nilivyokuja kuziona na kuzisoma nyaraka hizi zikiwa pamoja na ‘’cuttings,’’ za magazeti ya ‘’Uhuru’ na ‘’The Nationalist,’’ magazeti ambayo mhariri wake alikuwa Benjamin William Mkapa.
Mgogoro wa EAMWS ulipoanza mwezi Oktoba 1968 ikawa magazeti haya yamechagua upande wa kuunga mkono.
Kulikuwa na uongozi wa EAMWS chini ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na Bi. Titi Mohamed na kulikuwa na kikundi kingine kikiongozwa na Adam Nasibu mwalimu wa shule ya msingi kutoka Bukoba.
Magazeti ya ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ katika mgogoro huu yalikuwa yanaandika habari za hiki kikundi kilichokuwa kinapambana na viongozi wa EAMWS wakidai kuvunjwa kwa jumuia hiyo kwa sababu baadhi viongozi wake hawakuwa Waafrika wakawa wanachagiza serikali waivunje.
Patron wa EAMWS alikuwa Aga Khan.
Viongozi wa EAMWS chini ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir wao kama viongozi wa Waislam walikuwa upande wa pili wanapigania umoja na Waislam bila ya ubaguzi wa rangi.
Lakini kwa bahati mbaya magazeti haya mawili ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ yalikuwa hayatoi nafasi kwa wao viongozi wa Waislam chini ya EAMWS kueleza upande wao wa mgogoro ule.
Habari za mgogoro ndiyo zikawa habari kuu kwa magazeti ya ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ kwa miezi mitatu Adam Nasibu mtu ambae hakuna aliyepata kumsikia hata siku moja akitokea kwenye kurasa za mbele za ‘’Uhuru’’ na ‘’The Nationalist’’ kama msemaji wa umma wa Waislam wa Tanzania.
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akawa hasikiki popote ukiondoa katika darsa zake alizokuwa akiendesha katika misikiti mbali mbali ya Dar es Salaam mmoja wapo ukiwa msikiti wa Ngazija na Badawy.
Haikupita muda kwa jinsi magazeti haya na radio zilivyokuwa zinamhenga Adam Nasibu akafahamika kuwa Adam Nasibu na kikundi chake walikuwa wanaungwa mkono na serikali.
Katika moja ya mahojiano Adam Nasibu alinukuliwa na ‘’The Nationalist,’’ na ikamnukuu akisema kuwa: ‘’Muslims must know why the East African Muslims Welfare Society should have a constitution which was in line with the country’s policy. We do not know the role of the Aga Khan in our society and that is why we reject him.’’
(‘’Waislam lazima wafahamishwe kwa nini EAMWS iwe na katiba ambayo inaendana na mwelekeo wa nchi. Hatujui nafasi ya Aga Khan katika nchi yetu na ndiyo maana tunamkataa’’).
Wakati ulipozuka mgogoro huu EAMWS walikuwa wanajitayarisha kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam na jiwe la msingi limewekwa na Julius Nyerere akishuhudiwa na Sheikh Hassan bin Ameir na Tewa Said Tewa na mabalozi kutoka nchi za Kiislam wakiongozwa na Balozi wa Misri ambao ndiyo waliotoa fedha za ujenzi wa chuo hicho.
EAMWS ilivunjwa na serikali na ikaundwa BAKWATA ndiyo ukawa mwisho wa ujenzi wa Chuo Kikuu na shule za msingi na sekondari zilizokuwa zinajengwa nchi nzima.
Miaka mingi baadae Benjamin Mkapa sasa akiwa rais wa Tanzania aliwapa majengo Waislam wa Tanzania kuanzisha Chuo Kikuu.
Wakati huo wengine tayari walikuwa wana vyuo karibu ya 20.
Kila ninapofika Muslim University of Morogoro (MUM) nashindwa kujuzuia kukumbuka mgogoro ule wa EAMWS na propaganda za ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ uliopelekea Waislam washindwe kujenga Chuo Kikuu.
Katika kipindi hiki cha mgogoro wa EAMWS Abdul Sykes akafariki dunia.
Hapa ndipo lilipotendeka jambo lililosikitisha watu wengi sana.
‘’Uhuru’’ na ‘’The Nationalist,’’ walipuuza kifo cha Abdul Sykes mzalendo, mfadhili na muasisi wa TANU na mtu aliyempokea Julius Nyerere na kuishinae nyumbani kwake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kilichochapwa na magazeti haya ni taarifa fupi kuwa Julius Nyerere amehudhuria mazishi ya Abdul Sykes makaburi ya Kisutu.
Hapakuwa na kingine zaidi ya hayo.