Benjamin W. Mkapa: Mhariri wa “Uhuru” na “The Nationalist”

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
BENJAMIN WILLIAM MKAPA MHARIRI WA ‘’UHURU’’ NA ‘’THE NATIONALIST’’ KATIKA MGOGORO WA EAST AFRICAN MUSLIM WELFARE SOCIETY (EAMWS) 1968

Katika utafiti wakati naandika historia ya TANU kupitia maisha ya Abdulwahid Sykes nilipewa faili lililokuwa na nyaraka ambazo zilihifadhiwa kwa kificho na Bilal Rehani Waikela kwa miaka kama 20 hivi.

Hizi nyaraka zilikuwa zinataarifa ya mgogoro wa iliyokuwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa ikishughulika na maendeleo ya Waislam wa Afrika ya Mashariki.

Waikela akiwa kiongozi wa EAMWS Tabora alichaguliwa kuwa katika Tume ya Kwikima iliyoundwa kutafuta sulhu ya mgogoro ule.

Sulhu haikupatikana na serikali ikavunja EAMWS na kuunda BAKWATA.

Baada ya kuvunjika kwa EAMWS zikasikika taarifa kuwa yeyote katika wajumbe wale ataekutwa na nyaraza zozote za mgogoro wa EAMWS atakamatwa.

Waikela alipopata taarifa hii yeye akazihamisha nyaraka zake nyumbani kwake akaenda kuzificha mahali pengine salama.

Baada ya miaka mingi kupita hizi nyaraka (mimi katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) nimezipa jina, ‘’Nyaraka za Waikela’’), Waikela alizifikisha kwa wanafunzi wa Kiislam wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wazitunze katika maktaba yao.

Hivi ndivyo mimi nilivyokuja kuziona na kuzisoma nyaraka hizi zikiwa pamoja na ‘’cuttings,’’ za magazeti ya ‘’Uhuru’ na ‘’The Nationalist,’’ magazeti ambayo mhariri wake alikuwa Benjamin William Mkapa.

Mgogoro wa EAMWS ulipoanza mwezi Oktoba 1968 ikawa magazeti haya yamechagua upande wa kuunga mkono.

Kulikuwa na uongozi wa EAMWS chini ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na Bi. Titi Mohamed na kulikuwa na kikundi kingine kikiongozwa na Adam Nasibu mwalimu wa shule ya msingi kutoka Bukoba.

Magazeti ya ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ katika mgogoro huu yalikuwa yanaandika habari za hiki kikundi kilichokuwa kinapambana na viongozi wa EAMWS wakidai kuvunjwa kwa jumuia hiyo kwa sababu baadhi viongozi wake hawakuwa Waafrika wakawa wanachagiza serikali waivunje.

Patron wa EAMWS alikuwa Aga Khan.

Viongozi wa EAMWS chini ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir wao kama viongozi wa Waislam walikuwa upande wa pili wanapigania umoja na Waislam bila ya ubaguzi wa rangi.

Lakini kwa bahati mbaya magazeti haya mawili ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ yalikuwa hayatoi nafasi kwa wao viongozi wa Waislam chini ya EAMWS kueleza upande wao wa mgogoro ule.

Habari za mgogoro ndiyo zikawa habari kuu kwa magazeti ya ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ kwa miezi mitatu Adam Nasibu mtu ambae hakuna aliyepata kumsikia hata siku moja akitokea kwenye kurasa za mbele za ‘’Uhuru’’ na ‘’The Nationalist’’ kama msemaji wa umma wa Waislam wa Tanzania.

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akawa hasikiki popote ukiondoa katika darsa zake alizokuwa akiendesha katika misikiti mbali mbali ya Dar es Salaam mmoja wapo ukiwa msikiti wa Ngazija na Badawy.

Haikupita muda kwa jinsi magazeti haya na radio zilivyokuwa zinamhenga Adam Nasibu akafahamika kuwa Adam Nasibu na kikundi chake walikuwa wanaungwa mkono na serikali.

Katika moja ya mahojiano Adam Nasibu alinukuliwa na ‘’The Nationalist,’’ na ikamnukuu akisema kuwa: ‘’Muslims must know why the East African Muslims Welfare Society should have a constitution which was in line with the country’s policy. We do not know the role of the Aga Khan in our society and that is why we reject him.’’

(‘’Waislam lazima wafahamishwe kwa nini EAMWS iwe na katiba ambayo inaendana na mwelekeo wa nchi. Hatujui nafasi ya Aga Khan katika nchi yetu na ndiyo maana tunamkataa’’).

Wakati ulipozuka mgogoro huu EAMWS walikuwa wanajitayarisha kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam na jiwe la msingi limewekwa na Julius Nyerere akishuhudiwa na Sheikh Hassan bin Ameir na Tewa Said Tewa na mabalozi kutoka nchi za Kiislam wakiongozwa na Balozi wa Misri ambao ndiyo waliotoa fedha za ujenzi wa chuo hicho.

EAMWS ilivunjwa na serikali na ikaundwa BAKWATA ndiyo ukawa mwisho wa ujenzi wa Chuo Kikuu na shule za msingi na sekondari zilizokuwa zinajengwa nchi nzima.

Miaka mingi baadae Benjamin Mkapa sasa akiwa rais wa Tanzania aliwapa majengo Waislam wa Tanzania kuanzisha Chuo Kikuu.

Wakati huo wengine tayari walikuwa wana vyuo karibu ya 20.

Kila ninapofika Muslim University of Morogoro (MUM) nashindwa kujuzuia kukumbuka mgogoro ule wa EAMWS na propaganda za ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ uliopelekea Waislam washindwe kujenga Chuo Kikuu.

Katika kipindi hiki cha mgogoro wa EAMWS Abdul Sykes akafariki dunia.

Hapa ndipo lilipotendeka jambo lililosikitisha watu wengi sana.

‘’Uhuru’’ na ‘’The Nationalist,’’ walipuuza kifo cha Abdul Sykes mzalendo, mfadhili na muasisi wa TANU na mtu aliyempokea Julius Nyerere na kuishinae nyumbani kwake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kilichochapwa na magazeti haya ni taarifa fupi kuwa Julius Nyerere amehudhuria mazishi ya Abdul Sykes makaburi ya Kisutu.

Hapakuwa na kingine zaidi ya hayo.
 
Right now we are very generous in our remembrance of Ben, rightly so but we must be balanced.

My recollection is Ben is the only President of all, even Nyerere, who was properly inducted and worked his way up in the civil service. Nyerere was bririlliant but he had worked only in the party and never in the civil service until he became a high official. Mwinyi similarly was in the Party but never in the civil service. Jakaya too started work in the Party and then jumped into the government machinery. Magu missed both; he never worked in the party and went into the civil service as a junior minister. This is his biggest handicap.

Therefore Ben was very well versed in the workings of a government and his Presidency proved that. Only now we can fairly recall what he was able to achieve.

Ben had a brilliant mind, knew his English and was an avid reader. These are important qualities for a national leader. His biggest positive trait was he was honest and truthful throughout his leadership. He was willing to appear in High Court to defend an official who worked under him. This takes some nerve. I know somebody who had always depended on Ben if he needed anything done or terminated at the highest level because they had built such a high level of trust. Now we have hordes of liars and schemers.

Ben appreciated government revenue mobilization and he was the architect of the cash budget in Tanzania, a tool that is even used effectively to-date. Initiatives he started in the 4th Phase included formation of the TRA, TASAF, MKURABITA, etc which were some of his major accomplishments.

Ben was the ultimate statesman; ensuring the best of relationships with Breton Woods institutions and he had a clear foreign policy which he could articulate and ensure everybody in the Foreign Affairs followed. It was logical. Right now we have no foreign policy at all, damn stupid. Look at our policy towards Israel created by Mwalimu himself; completely upside down and no explanation whatsoever.

But I also think during his final five years Ben’s leadership became thuggish. He regrets sending armed police against unarmed civilians in Pemba as well as the Mwembechai killings. These two he could not excuse to being ill advised so he should take full blame.

I also think he tends to pass the buck when he should assume full responsibility; EPA cant be explained away by poor advise from the BOT Governor. This is blaming the dead, completely unacceptable. He also sold the family silver and other then being poorly advised he has no explanation. Even worse, he took no less than 2 properties for himself! Leave alone what his in laws did in his name. Utterly awful stuff.

I am sure God Almighty will reward him appropriately but as Human Beings we shall say our prayers as usual.
 
Kwanini kila kitu unakieleza kwa kukiunganisha na Dini ya kiislamu? Ina maana wewe huoni uwepo wa dini nyingine, isipokuwa uislamu tu? Kazi unayo.
Rogo,
Waislam wana historia ya kutukuka katika Tanganyika historia ambayo kwa bahati mbaya ilihusudika na ikawa katika hatari ya kupotea kabisa.

Nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nikagundua kuwa ama kwa kutojua au kwa makusudi walimu walikuwa wanasomesha historia ambayo siyo.

Ninayo mifano mingi lakini hapa nitakupa miwili.

Tulikuwa tunasomeshwa historia ya vyama vya wafanyakazi Tanzania kulikuwa na kitabu tunakisoma cha Alfred Tandau aliyekuwa Katibu Mkuu wa NUTA.

Siku moja nikamwambia mwalimu wangu kuwa Alfred Tandau hajui historia ya vyama vya wafanyakazi kama angejua angemtaja katika kitabu chake babu yangu Salum Abdallah Popo.

Nilionekana kichekesho.
Darasa zima lilishika mbavu.

Siku nyingine nikamwambia mwalimu yule yule kuwa hiyo anayosomesha si historia ya kweli ya TANU kwani haiwezekani kufundishwa historia ya TANU bila kuanza na African Association na huwezi kuitaja African Association bila ya kumtaja Kleist Sykes na hivyo hivyo huwezi kuifundisha historia ya TANU bila kumtaja mwanae Abdul Sykes.

Siku ile darasa halikucheka.

Ulitanda mshangao kwani iliwapitikia wanafunzi wenzangu na mwalimu wetu kuwa kuna kitu cha kweli mimi nakifahamu.

Katika historia hii kama wewe unao wengine nje ya hawa tuandikie tuwasome.

Mwaka jana Pius Msekwa aliandika makala moja katika kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akasema Nyerere ndiye aliyeunda TANU.

Niliandika makala nikasema kama nilivyopata kusema huko nyuma kuwa Pius Msekwa haijui historia ya TANU.

Umesema kweli kazi ninayo na si ndogo.

Nimeisahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nafahamu sana unavyotabika kusoma historia hii kila unapogusa unasoma majina ya Waislam ambayo hukupata kuyasoma popote pale.

Hii ndiyo kazi niliyojipa ya kuiokoa historia hii isipotee.
 
Fair even to the deceased ones!
Mkapa's critics must have cojones and the audacity to mention his good deeds too.

I appreciate the way you address fairness in simple words.
Very articulate.
Thank you very much!
 
Rogo,
Waislam wana historia ya kutukuka katika Tanganyika historia ambayo kwa bahati mbaya ilihusudika na ikawa katika hatari ya kupotea kabisa.

Nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nikagundua kuwa ama kwa kutojua au kwa makusudi walimu walikuwa wanasomesha historia ambayo siyo.

Ninayo mifano mingi lakini hapa nitakupa miwili.

Tulikuwa tunasomeshwa historia ya vyama vya wafanyakazi Tanzania kulikuwa na kitabu tunakisoma cha Alfred Tandau aliyekuwa Katibu Mkuu wa NUTA.

Siku moja nikamwambia mwalimu wangu kuwa Alfred Tandau hajui historia ya vyama vya wafanyakazi kama angejua angemtaja katika kitabu chake babu yangu Salum Abdallah Popo.

Nilionekana kichekesho.
Darasa zima lilishika mbavu.

Siku nyingine nikamwambia mwalimu yule yule kuwa hiyo anayosomesha si historia ya kweli ya TANU kwani haiwezekani kufundishwa historia ya TANU bila kuanza na African Association na huwezi kuitaja African Association bila ya kumtaja Kleist Sykes na hivyo hivyo huwezi kuifundisha historia ya TANU bila kumtaja mwanae Abdul Sykes.

Siku ile darasa halikucheka.

Ulitanda mshangao kwani iliwapitikia wanafunzi wenzangu na mwalimu wetu kuwa kuna kitu cha kweli mimi nakifahamu.

Katika historia hii kama wewe unao wengine nje ya hawa tuandikie tuwasome.

Mwaka jana Pius Msekwa aliandika makala moja katika kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akasema Nyerere ndiye aliyeunda TANU.

Niliandika makala nikasema kama nilivyopata kusema huko nyuma kuwa Pius Msekwa haijui historia ya TANU.

Umesema kweli kazi ninayo na si ndogo.

Nimeisahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nafahamu sana unavyotabika kusoma historia hii kila unapogusa unasoma majina ya Waislam ambayo hukupata kuyasoma popote pale.

Hii ndiyo kazi niliyojipa ya kuiokoa historia hii isipotee.
Umeelewa swali la Mhusika?. Mimi nimemuelewa hivi:

Utafiti na maandiko yako yanavutia fikra, hatahivyo inakera kwa jinsi wewe kama muandishi unavyoshabikia udini ndani ya maandiko hayo.

Hatuvutiwi na kufahamu dini za watu, tunavutiwa kufahamu wao wamechangiaje kwenye historia. Awe ni Muislam, Mkristo, asiye na dini, mhindi, mwafirika, mzungu etc hatutaki kujua tunataka kufahamu role yake kwenye history basi.
 
George...
Hao waliofanya juhudi za kuifuta historia ya wazee wangu walisukumwa na dini zao kufanya hivyo.

Au huamini?
 
kaazi kweli kweli
Bhachu,
Kazi ilikuwa kubwa kwani baada ya kutoka kitabu cha Abdul Sykes nilishirikishwa kwenye miradi mitatu - Oxford University University Press New York (Dictionary of African Biography)na Nairobi (Historia kwa shule za msingi).

Na nikapokea mialiko mingi kutoka vyuo mbali mbali Marekani, Ulaya na Afrika.

Nimeandika vitabu kama saba na vyote vinahusu kuirudisha historia iliyokuwa imepotea.

Hakika kazi ilikuwa kubwa sana.
 
George...
Hao waliofanya juhudi za kuifuta historia ya wazee wangu walisukumwa na dini zao kufanya hivyo.

Au huamini?
Kwahiyo, je tuseme bila kupepesa macho kwamba unatumia historia ya masuala ya kisiasa ya nchi yetu kama fursa ya kuelezea misimamo yako ya kidini?
 
Mzee Mohamed heshima yako!naona post zako nyingi unajitahidi kurekebisha historia;hongera sana!Je makusudi hasa ni yepi?Maana unaandika katika namna inayeonyesha Waislam kuonewa!

Ni kweli kwamba haufahamu zama hizi kuna familia zinazoishi na ndugu wa dini tofauti ama kwa ndoa au makuzi!Kulikoni hasa kila uliandikalo unajinasibisha na dini yako au ya wazee wako!?

Nashauri toka kwenye kifungo cha dini kisha andika historia hiyo!na kwa nini kila atakayeandika kama si wa dini yako basi yeye hajui historia!maana kuna watu wakubwa wa umri wa wazazi wako lakini kila siku ukiwakosoa!mzee wangu toka kwenye hilo kasha la udini,himiza umoja na chochea fikra za sayansi na teknolojia maana ndo future ya kizazi hiki
Alamsik
 
Kwahiyo, je tuseme bila kupepesa macho kwamba unatumia historia ya masuala ya kisiasa ya nchi yetu kama fursa ya kuelezea misimamo yako ya kidini?
George,
Hiyo historia ninayoandika haina uhusiano wowote na dini yangu.

Uandishi huu unaitwa "corrective," yaani masahihisho.

Walioandika historia ya TANU labda kwa kutishwa na ule ukweli wa wingi na mchango wa Waislam katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika waliamua kukwepa ukweli huu.

Mimi nimekuja kufanya masahihisho.

Sijatumia historia ya mtu yeyote ila historia ya wazee wangu.

Nakuomba usome kitabu ujifunze yale ambayo huyajui.
 
Mzee Mohamed heshima yako!naona post zako nyingi unajitahidi kurekebisha historia;hongera sana!Je makusudi hasa ni yepi?Maana unaandika katika namna inayeonyesha Waislam kuonewa!Ni kweli kwamba haufahamu zama hizi kuna familia zinazoishi na ndugu wa dini tofauti ama kwa ndoa au makuzi!Kulikoni hasa kila uliandikalo unajinasibisha na dini yako au ya wazee wako!?Nashauri toka kwenye kifungo cha dini kisha andika historia hiyo!na kwa nini kila atakayeandika kama si wa dini yako basi yeye hajui historia!maana kuna watu wakubwa wa umri wa wazazi wako lakini kila siku ukiwakosoa!mzee wangu toka kwenye hilo kasha la udini,himiza umoja na chochea fikra za sayansi na teknolojia maana ndo future ya kizazi hiki
Alamsik
Mtoto...
Unajitisha bure.

Huu niandikao ndiyo ukweli wa nchi yetu.
Kuhusu madhila ya Waislam wenyewe hivi karibuni wameeleza ili viongozi wetu wachukue hatua ya kuweka haki na usawa katika jamii.

Serikali naamini itatoa majibu.
Wewe huna sababu ya kuhangaika.
 
BENJAMIN WILLIAM MKAPA MHARIRI WA ‘’UHURU’’ NA ‘’THE NATIONALIST’’ KATIKA MGOGORO WA EAST AFRICAN MUSLIM WELFARE SOCIETY (EAMWS) 1968

Katika utafiti wakati naandika historia ya TANU kupitia maisha ya Abdulwahid Sykes nilipewa faili lililokuwa na nyaraka ambazo zilihifadhiwa kwa kificho na Bilal Rehani Waikela kwa miaka kama 20 hivi.

Hizi nyaraka zilikuwa zinataarifa ya mgogoro wa iliyokuwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa ikishughulika na maendeleo ya Waislam wa Afrika ya Mashariki.

Waikela akiwa kiongozi wa EAMWS Tabora alichaguliwa kuwa katika Tume ya Kwikima iliyoundwa kutafuta sulhu ya mgogoro ule.

Sulhu haikupatikana na serikali ikavunja EAMWS na kuunda BAKWATA.

Baada ya kuvunjika kwa EAMWS zikasikika taarifa kuwa yeyote katika wajumbe wale ataekutwa na nyaraza zozote za mgogoro wa EAMWS atakamatwa.

Waikela alipopata taarifa hii yeye akazihamisha nyaraka zake nyumbani kwake akaenda kuzificha mahali pengine salama.

Baada ya miaka mingi kupita hizi nyaraka (mimi katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) nimezipa jina, ‘’Nyaraka za Waikela’’), Waikela alizifikisha kwa wanafunzi wa Kiislam wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wazitunze katika maktaba yao.

Hivi ndivyo mimi nilivyokuja kuziona na kuzisoma nyaraka hizi zikiwa pamoja na ‘’cuttings,’’ za magazeti ya ‘’Uhuru’ na ‘’The Nationalist,’’ magazeti ambayo mhariri wake alikuwa Benjamin William Mkapa.

Mgogoro wa EAMWS ulipoanza mwezi Oktoba 1968 ikawa magazeti haya yamechagua upande wa kuunga mkono.

Kulikuwa na uongozi wa EAMWS chini ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na Bi. Titi Mohamed na kulikuwa na kikundi kingine kikiongozwa na Adam Nasibu mwalimu wa shule ya msingi kutoka Bukoba.

Magazeti ya ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ katika mgogoro huu yalikuwa yanaandika habari za hiki kikundi kilichokuwa kinapambana na viongozi wa EAMWS wakidai kuvunjwa kwa jumuia hiyo kwa sababu baadhi viongozi wake hawakuwa Waafrika wakawa wanachagiza serikali waivunje.

Patron wa EAMWS alikuwa Aga Khan.

Viongozi wa EAMWS chini ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir wao kama viongozi wa Waislam walikuwa upande wa pili wanapigania umoja na Waislam bila ya ubaguzi wa rangi.

Lakini kwa bahati mbaya magazeti haya mawili ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ yalikuwa hayatoi nafasi kwa wao viongozi wa Waislam chini ya EAMWS kueleza upande wao wa mgogoro ule.

Habari za mgogoro ndiyo zikawa habari kuu kwa magazeti ya ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ kwa miezi mitatu Adam Nasibu mtu ambae hakuna aliyepata kumsikia hata siku moja akitokea kwenye kurasa za mbele za ‘’Uhuru’’ na ‘’The Nationalist’’ kama msemaji wa umma wa Waislam wa Tanzania.

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akawa hasikiki popote ukiondoa katika darsa zake alizokuwa akiendesha katika misikiti mbali mbali ya Dar es Salaam mmoja wapo ukiwa msikiti wa Ngazija na Badawy.

Haikupita muda kwa jinsi magazeti haya na radio zilivyokuwa zinamhenga Adam Nasibu akafahamika kuwa Adam Nasibu na kikundi chake walikuwa wanaungwa mkono na serikali.

Katika moja ya mahojiano Adam Nasibu alinukuliwa na ‘’The Nationalist,’’ na ikamnukuu akisema kuwa: ‘’Muslims must know why the East African Muslims Welfare Society should have a constitution which was in line with the country’s policy. We do not know the role of the Aga Khan in our society and that is why we reject him.’’

(‘’Waislam lazima wafahamishwe kwa nini EAMWS iwe na katiba ambayo inaendana na mwelekeo wa nchi. Hatujui nafasi ya Aga Khan katika nchi yetu na ndiyo maana tunamkataa’’).

Wakati ulipozuka mgogoro huu EAMWS walikuwa wanajitayarisha kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam na jiwe la msingi limewekwa na Julius Nyerere akishuhudiwa na Sheikh Hassan bin Ameir na Tewa Said Tewa na mabalozi kutoka nchi za Kiislam wakiongozwa na Balozi wa Misri ambao ndiyo waliotoa fedha za ujenzi wa chuo hicho.

EAMWS ilivunjwa na serikali na ikaundwa BAKWATA ndiyo ukawa mwisho wa ujenzi wa Chuo Kikuu na shule za msingi na sekondari zilizokuwa zinajengwa nchi nzima.

Miaka mingi baadae Benjamin Mkapa sasa akiwa rais wa Tanzania aliwapa majengo Waislam wa Tanzania kuanzisha Chuo Kikuu.

Wakati huo wengine tayari walikuwa wana vyuo karibu ya 20.

Kila ninapofika Muslim University of Morogoro (MUM) nashindwa kujuzuia kukumbuka mgogoro ule wa EAMWS na propaganda za ‘’Uhuru,’’ na ‘’The Nationalist,’’ uliopelekea Waislam washindwe kujenga Chuo Kikuu.

Katika kipindi hiki cha mgogoro wa EAMWS Abdul Sykes akafariki dunia.

Hapa ndipo lilipotendeka jambo lililosikitisha watu wengi sana.

‘’Uhuru’’ na ‘’The Nationalist,’’ walipuuza kifo cha Abdul Sykes mzalendo, mfadhili na muasisi wa TANU na mtu aliyempokea Julius Nyerere na kuishinae nyumbani kwake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kilichochapwa na magazeti haya ni taarifa fupi kuwa Julius Nyerere amehudhuria mazishi ya Abdul Sykes makaburi ya Kisutu.

Hapakuwa na kingine zaidi ya hayo.
Toka uko mtoto unalalamika tu

Kijana unalalamika tu dola inakuonea na waislam

Na sasa mpaka umezeeka unalalamika tu

Nimesomesha mpaka nje kila mahala nimefundisha

Haya sasa ardhi hiyo hapo jenga sasa chuo kama mwanaume kweli,umebaki kulalama tu kariakoo/mapipa kwenye vijiwe vya kahawa tunaonewa mfumo kristo.

Toka EAMWS mpaka now hakuna ulichokifanya zaid ya kupiga porojo kila kukicha kuleta propaganda za UGAIDI.

Mmeanza kulalamika toka Nyerere mpaka Magufuli,kokote aliko muislam duniani lazima analalamika anaonewa.

Maandishi yako now nategemea kuona ni kiasi gani ulitaka kujenga chuo/vyuo/shule serikali ikakukwamisha!

Sio stori zako za kubumba za kwenda kuombea hela za kahawa kwa matajiri wa kiarabu kariakoo.
 
George...
Hao waliofanya juhudi za kuifuta historia ya wazee wangu walisukumwa na dini zao kufanya hivyo.

Au huamini?
Dini yao iliwalisukumwa kufuta historia ya wazee wako?
Kama hao walikuwa Ni Wakristo, walitumia kitabu gani Cha kwenye Biblia? Najua Bible msisitizo wake mkubwa ni upendo.
1. Wapendeni adui zenu na kuwaombea
2. Mpende jirani yako Kama nafsi yako
3. Amri kuu ni upendo. Etc
 
Bhachu,
Kazi ilikuwa kubwa kwani baada ya kutoka kitabu cha Abdul Sykes nilishirikishwa kwenye miradi mitatu - Oxford University University Press New York (Dictionary of African Biography)na Nairobi (Historia kwa shule za msingi).

Na nikapokea mialiko mingi kutoka vyuo mbali mbali Marekani, Ulaya na Afrika.

Nimeandika vitabu kama saba na vyote vinahusu kuirudisha historia iliyokuwa imepotea.

Hakika kazi ilikuwa kubwa sana.

Hongera sana Boss, ila bado una kazi kubwa sana.
 
Dini yao iliwalisukumwa kufuta historia ya wazee wako?
Kama hao walikuwa Ni Wakristo, walitumia kitabu gani Cha kwenye Biblia? Najua Bible msisitizo wake mkubwa ni upendo.
1. Wapendeni adui zenu na kuwaombea
2. Mpende jirani yako Kama nafsi yako
3. Amri kuu ni upendo. Etc
Kwenye uandishi wa aina yoyote pale mwandishi anapokua na upendeleo kwasababu yeye ni mnufaika wa habari husika basi habari hiyo yafaa kupuuzwa na wanawema wote wenye msimamo tofauti pamoja na mawazo mbadala na ya mwandishi husika!
 
Toka uko mtoto unalalamika tu

Kijana unalalamika tu dola inakuonea na waislam

Na sasa mpaka umezeeka unalalamika tu

Nimesomesha mpaka nje kila mahala nimefundisha

Haya sasa ardhi hiyo hapo jenga sasa chuo kama mwanaume kweli,umebaki kulalama tu kariakoo/mapipa kwenye vijiwe vya kahawa tunaonewa mfumo kristo.

Toka EAMWS mpaka now hakuna ulichokifanya zaid ya kupiga porojo kila kukicha kuleta propaganda za UGAIDI.

Mmeanza kulalamika toka Nyerere mpaka Magufuli,kokote aliko muislam duniani lazima analalamika anaonewa.

Maandishi yako now nategemea kuona ni kiasi gani ulitaka kujenga chuo/vyuo/shule serikali ikakukwamisha!

Sio stori zako za kubumba za kwenda kuombea hela za kahawa kwa matajiri wa kiarabu kariakoo.
Lukubuzo...
Bahati mbaya umekasirika na badala ya kufanya mjadala umerudi na lugha ambayo si ya kiungwana.

Lugha za "kulalamika," "kuomba hela kwa Waarabu," nk.

Kawaida yangu ni kuwa mjadala ukifikia hali hii mimi humpumzisha ninaejadilinae ili ghadhabu zake zipungue na akili zake zirejee.
 
Dini yao iliwalisukumwa kufuta historia ya wazee wako?
Kama hao walikuwa Ni Wakristo, walitumia kitabu gani Cha kwenye Biblia? Najua Bible msisitizo wake mkubwa ni upendo.
1. Wapendeni adui zenu na kuwaombea
2. Mpende jirani yako Kama nafsi yako
3. Amri kuu ni upendo. Etc
Buji...
Mimi si wa kujibu maswali hayo.

Wewe ndiyo wa kutafuta kutaka kujua ilikuwaje historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ikaandikwa sivyo kwa makosa makubwa?

Ujiulize iweje historia hiyo irekebishwe na mtu binafsi tu Mohamed Said kwa kutumia Nyaraka za Sykes?

Ujiulize hayo niliyoandika yana ukweli wa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom