Benjamin Mkapa aingizwa EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benjamin Mkapa aingizwa EPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 20, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,438
  Trophy Points: 280
  [h=1]Benjamin Mkapa aingizwa EPA[/h][HR][/HR]
  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 13 July 2011

  [​IMG][​IMG][​IMG]  SIRI imefichuka. Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kupelekewa ombi la kuingilia kati Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam apate fedha kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), MwanaHALISI limeelezwa.

  Taarifa zinasema aliyejaribu kutumia mgongo wa Rais Mkapa ili apate urahisi wa kudandia kwenye akaunti ya EPA, ni Yusuph Manji, mtendaji mkuu wa kampuni ya Quality Group Limited (QGL).
  Barua kwenda kwa rais, Kumb. Na. QGL/CEO/PORT.PROJ/2005/09 inaonyesha iliandikwa tarehe 20 Septemba 2005.

  Barua hiyo ilisainiwa na Manji. Majibu ya barua hiyo kutoka kwa rais hayakupatikana.
  Mradi ambao Manji aliomba Mkapa kusaidia, unahusu ujenzi wa “bandari ya pili katika mlango wa bahari wa Dar es Salaam” ambayo anasema haitaingilia shughuli za kampuni iliyopo sasa ya kupakia na kupakua mizigo bandarini (TICTS).

  Mradi ambao imefahamika haujaanza, ulijulikana kama Inland Container Depot (ICD) na inaelezwa kuwa ulilenga “kupunguza mlundikano wa makontena katika bandari” ya Dar es Salaam.
  Ulikuwa uwe katika kitalu 27, Kurasini karibu na Bandari ya Dar es Salaam.
  Sehemu ya barua ya Manji inaeleza kuwa mradi wake ni wa miundombinu; wenye kuhitaji mtaji mkubwa na kwamba QGL tayari imekamilisha mchango wake.

  Lakini anasema, amongst the few specific items of support we seek, is Your Excellency’s indulgence in facilitation of a Bank of Tanzania debt instrument (miongoni mwa mambo machache maalum ya msaada tunaotafuta, ni kuwezeshwa kuhusiana na utaratibu wa mpango wa madeni ya nje).
  Manji anasema sehemu ya pili ya msaada wa rais anayoomba ni kufikiriwa kupewa ardhi ambako watafanyia shughuli zao.

  Barua ya Manji iliandikwa katika kipindi ambapo Benki Kuu ilikuwa imekumbwa na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi ambao ulikuwa haujawahi kutokea nchini, kutoka kwenye akaunti ya EPA.

  Miongoni mwa makampuni yaliyoiba fedha hizo ni Kagoda Agriculture Limited, inayodaiwa kukwapua zaidi ya dola 39 milioni (sawa na Sh. 40 bilioni wakati huo) na ambayo Manji amekiri kuifahamu.

  Miezi minne iliyopita, gazeti hili liliripoti Manji akisema kuwa alisaidia Kagoda kulipa fedha ilizokuwa imetakiwa kurejesha ili isishitakiwe; na wiki tatu baadaye akadai kuwa alikuwa anataka kushitaki Kagoda kwa kuwa haijamrejeshea fedha zake alizoilipia serikalini.
  Wakati Manji anasema hayo; na yapo kwenye maandishi, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) amekuwa akidai kuwa hana ushahidi juu ya Kagoda na ama hajasikia au kumwona Manji ambaye aliikingia kifua Kagoda kwa “kuilipa serikalini.”

  Baadhi ya makampuni ambayo maodita wa Ernest&Young wametaja kuwa yalichota mabilioni kutoka BoT ni pamoja na Bencon International Limited iliyokuwa inamilikiwa na Jeetu Patel na ndugu zake Devendra Patel na Amit Nandy.
  Nyingine ni Changanyikeni Residential Complex Ltd, Manner Planner Consultants, Monner Planner ya Tanzania, BG Monner Kilolo and Brothers, Njake Enterprises ,Vb & Associates LTD of Tanzania, Venus Hotel Ltd of Tanzania na Maltan Mining Ltd of Tanzania, Bora Hotels & Apartment LTD, B.V Holdings Ltd, Ndovu Soap Ltd Ltd, Navy Cut Tobacco (T) Ltd na, Kagoda Agriculture Ltd.

  Makampuni mengine ni G&T International Ltd, Excellent Services Ltd, Liquidity Service Ltd, Clayton Marketing Ltd; M/S Rashtas (T) Ltd, Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloma and Brothers.
  Kumbukumbu za mkampuni ya Rashtas (T) na G&T International Ltd., hazikupatikana katika daftari la Msajili wa Majina ya Makampuni na Biashara (BRELA).
  Kwa mujibu wa Manji, lengo la mradi aliotaka rais kutumia uwezo wake kusaidia, ulilenga kuongeza tija katika bandari, ambapo sasa kazi ya upakiaji na upakuaji wa mzigo inafanywa na TICTS anayodai kuwa ina uwezo wa kuhifadhi makontena 250,000 tu kwa mwaka.

  Katika kufanikisha mradi huu, pamoja na miradi mingine kadhaa, Manji, katika mahusiano yake, anamtaja Walter Bgoya, mchapishaji vitabu wa kampuni ya Mkuki na Nyota, kuwa kiungo muhimu katika mradi huu na mingine.

  Anamtaja Bgoya kuwa mtu mwenye uelewa mpana katika mambo ya Bandari na kwamba anaheshimika hata nje ya nchi. Huyu ni miongoni mwa watu waliokuwa katika timu ya kampeni ya Mkapa mwaka1995.
  Kwa miaka kadhaa, wakati Mkapa akiwa rais, Bgoya alikuwa mjumbe wa bodi ya Mamlaka ya Bandari nchini (THA) akishika nafasi ya makamu mwenyekiti.
  Katika baadhi ya mawasiliano, Manji anamtaja Bgoya kuwa mtu mwenye uzoefu na uelewa katika mambo ya bandari na uchapishaji vitabu.

  Mahusiano kati ya Manji na Bgoya yanaonekana kuwepo hata mwaka 1993 anapomwandikia, “…nilikutana na Mama (Mama Anna Mkapa) Jumatatu ya tarehe 3 na nimemwambia kuwa nitaweza kumpa nyaraka uliyompa bossi (rais Benjamin Mkapa)…”
  Aidha, mahusiano yao yanaonyesha pia kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na Gavana wa BoT, Daudi Balali na alijua iwapo yuko ofisini au safarini.

  Lakini katika mawasiliano yake ya baadaye anasema kama gavana “akiuliza nitawamwabia kuwa kampuni siyo ya kwangu na ukweli inamilikiwa na watu wengine. Natumaini …tutaweza kushawishi watu kufikiri kwamba kuna makosa ya ubia…”
  Haikuweza kuthibitishwa iwapo Manji alishindwa kumshawishi Balali kukaribia akaunti ya EPA ndipo akaamua kutafuta msaada wa rais.

  Gazeti hili, kwa wiki tatu za kufuatilia suala hili (na uchunguzi unaendelea), halikuweza pia kuthibitisha iwapo maombi ya aina ya Manji ndiyo yalitumika kuchota fedha kutoka akaunti ya madeni BoT.

  Taarifa nyingine ambazo Manji anaeleza Bgoya, ni kuhusu katibu mkuu wa wizara ya fedha, kwamba alikuwa na maoni kuwa wamwingize kwenye bodi, bali hilo litafanyika baada ya yeye, Bgoya kuridhia.
  Gazeti hili lilizungumza na Bgoya. Alikana kuwa na mradi wowote na Manji. Alikana pia kuwa katika ubia au ushirika wa aina yoyote ile ndani ya Inland Container Depot.

  Bgoya alisema ana mradi wa kuchapisha vitabu na kuongeza kuwa “hata huu unanishinda. Hapa nahitaji dola milioni 2 kwa ajili ya mradi wangu wa ICD kwenye kiwanja changu, eneo la Kurasini. Sijazipata pamoja na kuhangaika.”
  Mradi wa Bgoya una jina lilelile kama ambalo Manji anataja katika barua yake kwa Rais Mkapa - Inland Container Depot na ufupi uleule – ICD.Manji hakuweza kupatikana kuulizwa kwa nini mpango wao ulikwama; kwa nini walikuwa na mpango wa kudanganya gavana wa benki; wanafanya nini hivi sasa kuhusu mradi huo na ilitokeaje QGL wakawa na mradi wenye jina lilelile na ule wa Bgoya huku Bgoya akidai hana uhusiano naye.
   
Loading...