comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Bunge nchini Benin limekuwa likifanya mjadala kuhusu marekebisho ya katiba ikiwemo kupunguza muda wa rais kuongoza hadi muhula mmoja wa miaka sita.
Kwa sasa rais anaweza kuongoza kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja.
Vuguvugu moja la upinzani lilifanya mgomo mbele ya bunge likisema kuwa raia wanafaa kupewa fursa ya kujadili mabadiliko hayo.
Nchini Benin marekebisho ya kikatiba yanaweza kuidhinishwa kupitia kura ya maoni ama wingi wa kura bungeni.
Rais wa taifa hilo Patrice Talon alisema kuwa atajaribu kubadili katiba hiyo wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka uliopita.