Ben Saanane amezimika kama moto wa Kibatari, nobody cares. Binadamu wanasahau haraka sana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,862
24,648
Nilikuwa mara nyingi sana najaribu kufuatilia maandishi ya mmoja ya waandishi waliopata kutokea kusimamia walichoamini haijalishi kina athari au ukweli kiasi gani. Ben Saanane alikuwa na kitu ana kiamini. Alisimamia hicho. Dunia ya leo ni ngumu sana kupata watu wenye kitu wanachoamini zaidi ya vyeo,madaraka na pesa ni ngumu sana.

Ben Saanane sikuwa nakubaliana na kila alichoandika. kuna mengine nlikuwa napingana naye. lakini nliendelea kumheshimu kuwa alikuwa au ni kijana anayejua kutafuta support na kile anachoamini ili watu wengine pia wapate kukifahamu.

Naamini alikuwa Mwaminifu kwa mtu au watu fulan. Ben Saanane aliishi maisha yake akiamua kuwa mwanasiasa wa Aina yake ambaye hakuwa na jukwaa ambalo angesimama na kuongea kwa kutumia kipaza sauti.

Yeye alitumia kalamu.Iinawezekana kuna infos alikuwa anapewa au ni juhudi yake mwenyewe kuzitafuta. Lakini kinachonifanya leo hii niukumbushe umma habari hizi ni yu wapi Ben Saanane? Jitihada za kumtafuta zimeishia wapi? Je, watu wamekubali kuwa hayupo, amejificha au amepotea?

Tulimtia nguvu, tulimsifu kwa ujasili wake , leo haonekani mbona hatusaidii kumtafuta? hatukumbushi kumtafuta? Je ni kweli kuwa tumeshamwacha apotee?

Kwa namna hii ya usahaulifu, mnadhani tunaweza kuwa na mashujaa siku zijazo? ni nani anajua alipo ben saanane?
 
Kwa sababu Mbowe na Tundu Lisu ndiyo wanaojuwa walichomfanya!
 
Unataka mpaka waje wakufuate??
 
Kwa sababu Mbowe na Tundu Lisu ndiyo wanaojuwa walichomfanya!
Tuangalie hapa isiye ikawa yale ya Ney wa Mitego kuimba madhambi ya mtu fulani tena kifasihi kama anavyotakiwa kufanya alafu yeye ndiye akawekwa ndani badala ya kufuatilia ukweli au uongo wa alichokiimba.
Ben Saanane alikuwa ni mfanyakazi wa cdm, je walilipoti hili suala kwenye vyombo vya usalama!? Kama walilipoti ni nani anatakiwa kutueleza hatima yake maana cdm wanaweza kuchunguza lakini vyombo vya usalama vinachunguza zaidi na tumeelezwa siku zote kuwa ndivyo vina mkono mrefu na Ben ni raia anayestahili kulindwa kisheria!
 
Kupotea kwa Saanane moja ya kitendawili kikubwa JF. Amepotea kwenye mazingira yapi? Nani anahusika? Kwa nini ndugu marafiki na washirika wake wote kimya? Very mysterious.
 
Mimi nashindwa kuelewa nikijiuliza juu ya huyo Ben Saa8,

Kwanza, je yeye hana familia? Kama anayo mbona wapo kimya?
Au walimuuza kama watoto wanaouzwa na familia zao ili wakajiripue kwa ugaidi?

Mbona chama chake kipo kimya, uongozi wote wa juu? Wanasheria wote? Je, hawajui kuwa kapotea?

Serikali yaani vyombo vya dola angalau vilisema vinaendelea kumtafuta, hapo tunaona jitihada.

Ial hao wote yaani familia/ndugu na chama alichokuwa anatumikia mbona hatujawasikia wakiulizia chochote hata huko polisi ili kujua maendeleo?

Pana usanii sana huko Tanzania yetu hii, hasa siasa uchwara hizi za majukwaani.
 
Si huyo tu huwa nikimkumbuka kamanda Alphonce Mawazo Tanzania naona kama ni kaburi la wanasiasa
 
Dunia hii ina mambo ya ajabu sanaa,ati ben kapotea na jarada limefungwa mbiombio
 
Back
Top Bottom