Bei za mafuta zaendelea kushuka nchini

Bei za mafuta zaendelea kushuka nchini

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Bei za mafuta ya petroli na dizeli zitakazotumika Oktoba mwaka huu nchini zimeendelea kupungua kwa kiwango tofauti ikilinganishwa na zilizokuwepo mwezi uliotangulia, huku upande wa mafuta ya taa ukiendelea kusalia vilevile.

Bei hizi zinapungua nchini wakati ambao kumekuwa na ongezeko katika soko la dunia kwa asilimia 2.80 kwa mafuta ya petroli, asilimia 3.65 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 3.57 kwa mafuta ya taa.

Pia taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaonyesha kuwa licha ya bei kikomo kupanda katika soko la dunia, gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa wastani wa asilimia 1.95 kwa mafuta ya petroli.

Kwa upande wa dizeli zimeongezeka kwa asilimia 2.39 na hakuna mabadiliko kwa mafuta ya taa. Katika Bandari ya Tanga zimeongezeka kwa asilimia 6.38 kwa mafuta ya petroli na dizeli na katika Bandari ya Mtwara zimeongezeka kwa asilimia 0.49 kwa mafuta ya petroli na hakuna mabadiliko kwa mafuta ya dizeli.

Hali hiyo inafanya bei ya jumla sasa lita moja ya mafuta inayopitia katika bandari ya Dar es Salaam kuuzwa kwa Sh2,720 kutoka Sh2,807 iliyotumika Septemba mwaka huu, dizeli itanunuliwa kwa Sh2,704 kutoka Sh2,754 iliyokuwapo Septemba mwaka huu

Hata hivyo, kwa watumiaji wa mafuta ya taa yanayopitia katika bandari hiyo watalazimika kuendelea kutumia bei ya Sh2,774 iliyokuwapo Septemba mwaka huu.

1759301070221.png


1759301105280.png


1759301133247.png


1759301169239.png


1759301192413.png


1759301215810.png
 
Back
Top Bottom