Bei za Mafuta ya Petroli na dizeli zashuka chini

Bei za Mafuta ya Petroli na dizeli zashuka chini

TANZANIA ITAANZA KUPATA MAENDELEO PINDI TU WATU WAKE WATAKAPOAMUA KUACHA UNAFIKI.
Tanzania ina maendeleo makubwa sana na Inaendelea kufanya vitu vingi sana vya maendeleo,ikiwepo miradi mikubwa ya kimkakati itakayo chochea kasi ya ukuaji wa uchumi wetu na ustawi wa watanzania.
 
Tanzania ina maendeleo makubwa sana na Inaendelea kufanya vitu vingi sana vya maendeleo,ikiwepo miradi mikubwa ya kimkakati itakayo chochea kasi ya ukuaji wa uchumi wetu na ustawi wa watanzania.
TANZANIA ITAANZA KUPATA MAENDELEO PINDI TU WATU WAKE WATAKAPOAMUA KUACHA UNAFIKI.
 
TANZANIA ITAANZA KUPATA MAENDELEO PINDI TU WATU WAKE WATAKAPOAMUA KUACHA UNAFIKI.
Watanzania wanajitambua na wala siyo wanafiki.wanamuunga kiongozi mchapakazi kama Rais Samia na CCM yake na kuwaacha wapiga porojo na matapeli wa kisiasa kama CHADEMA
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mambo yanaendelea kuwa mazuri chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge,simba wa nyika, komandoo wa vita na nyota ya matumaini. uongozi wake umeendelea kuwa wenye baraka na neema kwa wananchi na wenye kugusa maisha ya watu.

Hii ni baada ya EWURA kutangaza bei mpya za mafuta ambazo zitaanza kutumika leo tarehe 3 januari 2024.ambapo bei zimeshuka ukilinganisha na mwezi uliopita wa december.mfano kwa mkoa wa Dar mafuta ya petroli yameshuka kutoka 3158 mpaka 3084 wakati Dizeli yameshuka kutoka 3226 mpaka 3078.

EWURA imesema sababu za kushuka ni kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia pamoja na kupungua na kushuka kwa gharama za uagizaji wa mafuta.

Hivyo Watanzania wenzangu tuelewe kuwa mafuta yanapopanda bei haiwi dhamira ya serikali kuyapandisha na kumuumiza mwananchi bali inakuwa ni mabadiliko ya bei katika soko la Dunia. Serikali ya Rais Samia imekuwa yenye huruma ,upendo na kuwajali watanzania na kutokutaka kuona tukielemewa na mizigo ya bei kubwa ya vitu.

Hii ndio maana imekuwa ikitoa Ruzuku ya mabilioni katika mambo mbalimbali.mfano katika mafuta serikali yetu imara ilikuwa ikitoa Ruzuku ya Billion mia moja kila mwezi ,wakati kwenye kilimo inatoa takribani billion mia mbili hamsini kama Ruzuku.yote haya yanakuwa yanafanyika ili kuleta ahueni katika maisha ya watanzania na kumtua mzigo mwananchi..

Tuwe tunakuwa watulivu na wasikivu kwa serikali yetu pale hali inapokuwa imebadilika na ipo nje ya uwezo wa serikali yetu.kwa sababu ifahamike ya kuwa sisi hatuna visima vya mafuta hapa nchini,hivyo hatuwezi kupanga bei ambazo haziendani na uhalisia wa mafuta katika soko la Dunia wakati tunaagiza kutoka nje ya nchi ambako sisi hatuhusiki katika kupanga na kuwapangia bei.

Najuwa mtaanza kuuliza habari za kushuka kwa nauli.mimi binafsi naamini hilo litategemeana na utafiti utakaofanyika kuangalia kiwango kilichopungua kama kina kidhi vigezo vya kupungua kwa nauli kwa kila kilometa moja.ila naamini kushuka huku kwa bei kukienda miezi miwili mfululizo na ikapungua kabisa mpaka walau kuwa elfu mbili na pointi naamini nauli nazo zitashuka na zitarejea katika hali ya kawaida kama zamani.hilo tuwaachie na tuwaamini LATRA na serikali yetu ambayo ipo macho muda wote kumtetea , kumpigania na kumlinda mtanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Kushuka kwa bei za mafuta wakati nauli ni zilezile inamsaidia nini mwananchi wa kawaida?
Mauzauza hayataisha nchi hiii
 
Hapana ndugu yangu mimi sitafuti kuonwa bali nawaleteeni habari za ukweli na uhakika.ningekuwa natafuta kuonwa bila shaka ningekuwa nimekataa na tamaa kabisa kuwepo humu jukwaani.
Basi tuseme haujitambui . Kushuka huko kwa bei manufaa yake ni yapi?
 
Basi tuseme haujitambui . Kushuka huko kwa bei manufaa yake ni yapi?
Daaa kweli wewe unahitaji maombi na matibabu .kwa hiyo hujuwi faida na manufaa ya kushuka kwa bei ya mafuta? Au umeandika ukiwa umejimwagilizia kimiminika cha pombe kali kichwani ?
 
Lucas unakera unasifia mno hebu pia uwe unakosoa ikibidi ,kuna wakati uko sahihi lakini muda wote wewe ni kusifia tu ,hali mitaani ni ngumu ngumu sanaa
 
Bei za mafuta na petrol hazijawahi shuka zilipanda mpka leo zipo level ya kupanda!!
 
Lucas unakera unasifia mno hebu pia uwe unakosoa ikibidi ,kuna wakati uko sahihi lakini muda wote wewe ni kusifia tu ,hali mitaani ni ngumu ngumu sanaa
Wala usijali ndugu yangu ukiona nasifia sana basi wewe kosoa sana yake unayoona sijaongelea.kumbuka ya kuwa katika uongozi changamoto ni jambo la kawaida.lakini kinachoangaliwa ni juhudi za kutatua na kumaliza changamoto.serikali ya Rais Samia inafanya kazi kubwa sana katika kutatua changamoto mbalimbali ndio maana mamilioni ya watanzania wanaiunga mkono na kuipongeza sana.
 
Back
Top Bottom