Bei za Mafuta ya Petroli na dizeli zashuka chini

Bei za Mafuta ya Petroli na dizeli zashuka chini

Tumia akili ndugu yangu.kwani Tanzania tuna visima vya mafuta? Hujuwi kupanda kwa bei za mafuta kulitokana na kupanda katika soko la Dunia pamoja na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji?

We ndo utumie akili kuliko kujidhalilisha kisa tumbo fanya kazi acha kusifia pasipo stahili.

We hujiulizi kwenye mada zako kwa nini wachangiaji huwa wanakuhisi we ni hamnazo?
 
Wewe mwenyewe umekiri kwamba bei ya mafuta imeshuka hasa baada ya kushuka kwa bei soko la dunia .Sasa huyo unayemsifia amehusika vipi na hiyo bei mpya ya mafuta ambayo chanzo cha bei kuwa chini imelieleza vizuri .Hivi vijana wa siku hivi mkoje ?
 
Sijaona uhusika wa rais hasa baada ya kubainishiwa factor za kupandisha na kushusha ni soko/ bei za huko nje!

Mbili ni kwakuwa hatuna visima vya mafuta lakini tuna vya gas asilia, kwanini tusiweke kipaumbele kwenye matumizi ya tulicho nacho tukaachana namafuta tusiokuwa nayo?
Tatu twawezaje kujivunia bei ambayo shilingi elfu 10 ya kitanzania hupati hata lita 3 ilhali zamani elfu 10 ni full tank na chenji inabaki?

Mwisho, uchawa kusifu na kuabudu vimeiua Tanzania bahati mbaya wauaji ni vijana zaidi sijui mbeleni wataishije?!
Tuna vijana wa ovyo sana ambao liabilities hata kwa taifa ni mwendo wa kusifu tu tabia ambayo haiwezi kusaidia serikali kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka
 
Samia anaweza kununua magoli ya Simba na Yanga tu .

Bei ya mafuta kwenye soko la dunia ilishuka tangu mwezi September ajabu bongo ikaapanda.

Sababu nyepesi tu ni kuwa wanaopanga bei ndio wafanyabiashara wenyewe na ndio oil cartels.

Hizo sheli utitiri mnazoziona wamiliki wake 80% ni wabunge na mawaziri mnataka kudangaya watu watashusha bei kwa kiasi ambacho haitomuumiza mwananchi?
 
Lucas hebu tuambie inakuwaje unakuta km 3 kutoka makao makuu ya Wilaya vijiji havijawahi kuona umeme, maji au barabara tangu dunia iumbwe? CCM inafaa kuendelea kutawala?
 
Wewe mwenyewe umekiri kwamba bei ya mafuta imeshuka hasa baada ya kushuka kwa bei soko la dunia .Sasa huyo unayemsifia amehusika vipi na hiyo bei mpya ya mafuta ambayo chanzo cha bei kuwa chini imelieleza vizuri .Hivi vijana wa siku hivi mkoje ?
Wewe unafikiri yangeshuka kama Mh Rais angeamua kujaza tozo kwenye mafuta ?
 
Tuna vijana wa ovyo sana ambao liabilities hata kwa taifa ni mwendo wa kusifu tu tabia ambayo haiwezi kusaidia serikali kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka
Kuongea na kuzungumza ukweli siyo kusifia bali ni uungwana na uzalendo wa kuonyesha uhalisia wa jambo fulani.pia usitake na kulazimisha kila mtu awe na mtizamo ulionao wewe.
 
TANZANIA ITAANZA KUPATA MAENDELEO PINDI TU WATU WAKE WATAKAPOAMUA KUACHA UNAFIKI.
 
Back
Top Bottom