kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
SERIKALI imesema imejipanga kuhakikisha kuwa bidhaa zinazouzwa hazipandi bei katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ili kutowaadhibu waumini watakaofunga. Aidha, viongozi wa dini nchini wametakiwa kuendelea kuhubiri amani na kuhamasisha njia za mazungumzo, kutatua migogoro mbalimbali.
Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi wakati wa ufunguzi wa semina inayohusu mawasiliano kwa teknolojia na athari zake kwa viongozi hao. Alisema wafanyabiashara wengi wanatumia mwezi huo kupandisha bei za bidhaa ili kujinufaisha binafsi huku wakisahau kwamba wanatakiwa kuwa wazalendo na waadilifu.
‘’Kama ilivyo kwenye suala la sukari wafanyabiashara wengi walificha bidhaa na wengine kusambaza sukari ambayo haifai kwa matumizi ya binadamu na ndio hao hao waumini wetu ambao watapandisha bei ya bidhaa,’’ alisema Hapi.
Alisema wafanyabiashara watakaopandisha bei watachukuliwa hatua kwani serikali inasimamia weledi, ukweli na uadilifu. Alisisitiza kuwa sukari katika kipindi hicho itakuwa ya kutosha kwa kuwa serikali inaendelea kuingiza sukari na kwamba Watanzania ambao watafunga wasiwe na wasiwasi.
Akizungumzia wajibu wa viongozi wa dini, Hapi alisema kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kukemea wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola na kama kuna migogoro wanatakiwa kusuluhisha kwa njia ya mazungumzo.
Kwa mujibu wa Hapi, mauaji yaliyotokea katika Msikiti wa Masjid Rahman uliopo Ibanda, kata ya Mkoloni, Nyamagana jijini Mwanza, inaelezwa kuwa ni kutokana na migogoro kati ya waumini hao.
Alisema mgogoro ndio umesababisha vifo vya watu ambao hawana hatia na kwamba vitendo hivyo vinapaswa kulaaniwa. Hata hivyo, alisema serikali inaendelea kulinda maadili kupinga uovu na mmomonyoko wa maadili unaotokana na matumizi hasi ya teknolojia. Kwa upande wake, Shehe Issa Ponda aliiomba serikali kuweka mikakati imara ya kudhibiti teknolojia ili iwe na manufaa makubwa kuliko hasara.