Ni shambani ndo wanachukulia mara nyingi , ingawa kwa Arusha kuna soko la vitunguu linaitwa Kilombero , sasa huko ni Wakenya na wenye mitaji mikubwa ndo wanaenda chukua mzigo , Ila ukitaka kupata mzigo nzuri nenda shambani Mang'ola
Kuhusu suala la kuchambua ni gharama ya mnunuzi kiufupi gharama ziko hivi ( vifungashio + gharama ya vibarua kuchambua , kulalia kwenye magunia , kupandisha kwenye gari + gharama ya usafiri + ushuru ) .