Bei ya vitunguu sokoni ipo vipi?

Bei ya vitunguu sokoni ipo vipi?

Kingdom78

Member
Joined
May 31, 2015
Posts
72
Reaction score
79
Naomba kujua bei ya vitunguu kwa gunia mahali ulipo iko vipi? Hasa katika mikoa ya Dodoma, Dar es salaam, Morogoro na Mbeya?
 
Mimi nimelima kilosa morogoro ivyo natafuta masoko boss ndio maana naulizia ili nijue niuzie wapi.
 
Mang'ola karatu
Hamsini ni kwa ujazo wa neti ya debe saba alimaarufu neti ya magufuli

Na sabini ni kwa ujazo wa debe tisa alimaarufu neti ya mkenya au ya kuvuta
 
Mang'ola gunia la vitunguu size ya Kati au grade 2 ni elfu sabini na tano , grade 1 ni laki moja . Kwa Dar ni laki na nusu Kwa gunia la kilo Mia grade 2
Dar es salaam vitunguu magunia unauzia wapi? Au ndo kupambana na madalali Hornet
 
Kama uko tayari tuwasiliane mi ninakaa Moshi Nataka na Mimi kuanza hii biashara , nataka niwe natoa Arusha ( Mang'ola - Karatu ) kupeleka Dar
Samahani utajuaje gunia ni grade 2 au 1.
Au ni unajaza mwenyewe gunia.
Wewe hii biashara unaijua kiundani? Fitina na figisu figisu zote unazijua.
 
Mang'ola karatu
Hamsini ni kwa ujazo wa neti ya debe saba alimaarufu neti ya magufuli

Na sabini ni kwa ujazo wa debe tisa alimaarufu neti ya mkenya au ya kuvuta
Weka nyama nyama mkuu.
Gunia unajaza mwenyewe?
 
Vipi kwa upande huo wa Ruaha, hali ya mavuno mwaka huu inatabiriwaje?
 
Bora tu kuwa Dalali
unakua hauguswi na hasara...

Nipange basi nataka Mbuzi
Nitafutie soko la vitunguu.
Nataka nikalete vitunguu dada dalali.

Halafu faida tutailia mbuzi.
 
Grade zinapangwa kulingana na size ya vitunguu , ukiwa mang'ola grade one ipo pia inapatikana ni Yale mavitunguu makubwa kabisa
Nimekuelewa.
Lakini hujanijibu.
Ni kwamba vitunguu unachukulia shambani maana yake wanachambua wanapakia kwa gunia unaona au ubakuta tayari gunia wanakuambia hii grade 2 sh kadhaa.
 
Huko Mang'ola ( Karatu ) ndo kuna mashamba ya vitunguu
Hayo mashamba ukifika tu unapata au ndo ya kutafuta? Maana unaweza kuta mashamba kumbe kuna watu waliwekeza hela zao au wana wateja wao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom