Bei ya Nyama Jiji Dar Sasa Inatisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya Nyama Jiji Dar Sasa Inatisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mhache, Sep 9, 2008.

 1. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Maisha ya mwananchi wa kima cha chini yanakuwa magumu siku hadi siku. Wiki iliyopita bei ya nyama ilikuwa ni shilingi 3,200 kwa kilo kwa fedha ya ki-Tanzania. Juzi nilinunua nyama hiyo hiyo kwa shilingi 3,400 kwa kilo. Cha kushangaza ni kwamba leo asubuhi nimenunua nyama kwa shilingi 3,600 kwa kilo moja. Je tutafika?

  Ninachojiuliza ni kwamba wakati wa mfungo Mtukufu wa Ramadhani nyama inatumika kwa wingi sana au tatizo lipo wapi? Nikiangalia sioni sababu ya kufanya nyama ambayo ni kitoweo muhimu kwa wananchi kupanda hasa wakati wa sikukuu kubwa kama hii ya Mfungo, X-Mass na Pasaka. Ninadhani kuna haja ya kufanya juhudi za ziada ili kutuokoa sisi wa-Tanzania.
   
 2. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #2
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndo utandawazi huo, kila sehemu ina bei yake, bei ya manzese na Mbezi beach ni tofauti sana. mimi eneo ninaloishi tunanunua shilingi 3600 kwa kilo hata kabla ya mfungo
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  tunakazi TZ ili tupate suluhisho la kweli..Ng'ombe wangalikuwa wanatoka Nje, basi bei ya Nyama ingekuwa ndogo!!!
   
 4. Lasthope

  Lasthope Senior Member

  #4
  Sep 9, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Unachomaanisha ni kwamba wewe uajivunia kununua bei ya juu kwa sababu tu unakaa mbezi beach? huu ndio ulimbukeni na ndo maana hii nchi inakuwa haina sheria wala utaratibu kwa ajili ya watu wa aina yako, unasdhani kukaa sehemu fulani inahalaklisha wewe kulipa pesa ya juu kwenye bidhaa isivyostahili. kweli wabongo kazi ipo
   
 5. OFFORO

  OFFORO Member

  #5
  Sep 9, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hapa south kwa mzee mandela bei ya nyama kilo moja ni rand 50 ambayo ukiibadilisha ni sawa na shilingi za kibongo kama 7000 hivi

  tukomae tutafika
   
 6. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #6
  Sep 9, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Lasthope naona hujanielewa, kwanza mimi sijasema nakaa mbezi beach, nimetolea mfano tu. me naishi Mwananyamala uswahilini tu na ndo huko ambako nanunua nyama kwa bei nilioitaja. acha kuleta hizo wewe.

  Kwani wewe ni mkimbizi???????????????
   
Loading...