Kama ni raw milk (maziwa mabichi)
Kwa maeneo ya pale ipogolo kuna wafugaji wadowadogo walikua wanaleta pale kiwandani kwao (kibwabwa).
Cha kwanza lazima uwe registered kulingana na maximum standard/quality wanayohitaji wao.
Unapopeleka maziwa asubuhi unakuwa na invoice book yako, maziwa yanafanyiwa testing kwa kutumia kifaa maalum, kama umechanganya na maji au yana temperature ya juu (karibia kuganda) huwa hawayapokei.
Endapo hayana shida yeyote wakiyapokea unawapa invoice book yako mtu wa reception anasaini kiasi cha maziwa ulicho supply kwa siku hiyo.
Kwa litre moja huwa ni 800 ( kwa wanaoleta kiwandani)
Kwa maeneo kama ya njombe, Rungwe, kidabaga, kyela wana collection centers zao wafugaji hupeleka kwenye sehemu husika na kisha gari huja kubeba, na upande wa bei huwa tzs 600-800 kulingana na msimu husika ( kiangazi low supply, masika high supply)