Bei ya maji yaporomoka

Bei ya maji yaporomoka

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Punguzo hilo la bei ni sawa na kutoka Sh. 25 kwa lita mpaka karibu ya bure - Sh. 1.60.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, wakazi wa Sengerema walionyesha kufurahia unafuu huo na kuishukuru serikali kwa mradi huo uliogharimu Sh. bilioni 22 na ambao utawanufaisha wakazi zaidi ya 138,000.

Aidha, Mabula Sakambule na Philemon Makelele walisema mradi huo uliozinduliwa na Rais Magufuli Julai 4 utakuwa mkombozi kwao kiuchumi na kijamii.

Makelele aliyedai kuishi Sengerema kwa miaka 34, alisema kwa kipindi chote hicho kero ya maji ilikuwa kikwazo cha kiuchumi na kwamba baadhi ya huduma za kijamii zilidorora, ikiwamo usafi wa soko.

Akizungumzia mradi huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Antony Sanga alisema changamoto zote zilizopo zitakamilishwa wakati wa kipindi hiki kinachoendelea cha maboresho.

Alisema maboresho hayo yatahusu pia kubadilisha baadhi ya miundombinu, ikiwamo mabomba na kuwa wakazi wote waliomo katika mradi huo watafikiwa na huduma hiyo baada ya maboresho kufanyika.

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM) ameishukuru serikali kwa kumaliza kero hiyo na kuahidi kushirikiana na jamii kulinda miundombinu ya mradi huo. Fedha za mradi huo zimetoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na wadau wengine, ikiwamo Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria na Serikali.Mradi huo unatarajiwa kukidhi mahitaji ya mji wa Sengerema hadi mwaka 2030.

Chanzo: Nipashe
 
Dah.... Ajabu bei ya bia iko palepale [emoji15] [emoji15]

Sent from my Osborne II using JamiiForums Mobile App
 
Kwa wakolomije Huduma zinatelemka lakini kwa wengine bei ziko palepale, hii ni double standard
 
unamaanisha nini mkuu
Ninamaanisha hivi; wakati Mh. Rais alipokuwa akizindua huo mradi wa maji kuna Wanaharakati walikuja humu JF na kupotosha Umma kwa taarifa za UONGO zilizojaa Unafiki na uzandiki. Kwamba huo mradi ilikuwa haujakamilika na wahusika walimdanganya Mh.Rais kufungua/kuzindua mradi hewa.

Mpaka hivi sasa ninavyokujibu ni kwamba wananchi wa Sengerema wanafurahia huduma ya Maji kwa bei nafuu. Na Wanaharakati wameingia mitini baada ya kuumbuka kwa upotoshaji wao. Nafikiri utakuwa umenielewa mkuu.
 
Hujui siasa za maji taka mkuu
 
Back
Top Bottom