Bei ya maji Dar es salaam idhibitiwe

encyclopaedia Tanzaree

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
513
397
Hali ni mbaya sana katika sekta maji hasa kwa mkoa wa Dar es Salaam. hii inatokana na kutokuwepo kwa usawa katika upatikanaji wa maji miongoni mwa wanajamii.

Baadhi ya watu wachache wanaomiliki mabomba ya maji wanatumia fursa hiyo kuwanyonya watu wasiokuwa na uwezo wa kumiliki mabomba ya maji.

Bei ya maji ni Tsh 1200 kwa unit moja, ambapo unit moja ni sawa na ndoo 50 za lita 20.

Kitu cha ajabu ndoo ya lita 20 inauzwa 300 hadi 500 ambapo kwenye unit moja ya maji mwenye bomba anayoinunua 1200 yeye anauza 15000 hadi 25000.

Kwa mantiki hiyo mwenye bomba anapata faida kati ya 1250% hadi 2083%.

Huu ni unyonyaji tunaofanyiana watu wa hali ya chini sisi kwa sisi na unapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu.

Wengi wa wanaofanya hivi hata sio wapagani ila ni wakristu wazuri tu ambao huwa wanafanya maombi ya kufunga na mikesha kuombea mambo mbalimbali yanayotatiza maisha yetu kwa ujumla.

Pia wengine ni waislamu wazuri tu ambayo wanaendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Ombi langu kwenu ndugu zangu wenye mabomba hebu ziangalieni upya bei zenu mnazotulipisha tuhitajipo huduma ya maji kwani hazina usawa hata kidogo.

Pia mamlaka husika ziingilie kati hili suala hasa wakati huu wa janga la COVID19 kwa kuwa maji yanahitajika sana.
 
.mmmh mkuu ni wapii wanauza Bei hiyo......sisi kwetu mbona ndoo ni shiling 100 ya Lita 20,pei unit moja ya maji ni 1400, juzi nilikuwa napiga hesabu kwa bili niliyotumiwa.....
 
Vuta ya kwako uwalipe dawasco iyo 1200 per unit..

Sent using Jamii Forums mobile app
๐™ ๐™–๐™– ๐™ ๐™ž๐™ข๐™ฎ๐™– ๐™ ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™– ๐™ฌ๐™š๐™ฌ๐™š ๐™ช๐™ฃ๐™–๐™ ๐™ช๐™ก๐™– ๐™ ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™ช
 
Issue ya maji ni janga kwa watumiaji japo haipewi nafasi.
๐™ฃ๐™™๐™ž๐™ค ๐™๐™–๐™ฅ๐™ค, ๐™—๐™ค๐™ง๐™– ๐™๐™–๐™ฉ๐™– ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™œ๐™š๐™ ๐™ช๐™ฌ๐™– ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™–๐™ช๐™ฏ๐™– ๐™ก๐™ž๐™ฉ๐™– ๐Ÿค๐Ÿข ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐Ÿฃ๐Ÿข๐Ÿข ๐™ก๐™–๐™ ๐™ž๐™ฃ๐™ž ๐™จ๐™–๐™ž๐™ฏ๐™ž ๐™ ๐™–๐™ข๐™– ๐™ซ๐™ž๐™ก๐™š ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™–๐™ฉ๐™ช๐™ ๐™ค๐™ข๐™ค๐™– ๐™ฉ๐™ช๐™จ๐™ž๐™ค๐™ ๐™ช๐™ฌ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™–๐™—๐™ค๐™ข๐™—๐™–
 
Vipi Warusi hawajakutumia tu mkwanja wako?
 
Niliuliza DAWASA wakasema ni 1650

jamaa kwa nini ukae sehemu ya kununua maji hama Mara moja.
maji ni Uhai
Mtu kukaa nyumba isiyokuwa na maji sio kupenda, kwa mfano kama ikiwa ni lazima kila mtu kuishi nyumba yenye bomba basi na uhakika 80% ya watanzania watakosa nyumba za kuishi.
Na hapo hapo ujue miundombinu ya mamlaka za maji sio toshelezi kuwezesha upatikanaji wa maji kwa watu wengi kwa mara moja ndio maana maji muda mwingine hutolewa kwa mgao au yanakuwepo ila hayana pressure.
 
๐™ฃ๐™™๐™ž๐™ค ๐™๐™–๐™ฅ๐™ค, ๐™—๐™ค๐™ง๐™– ๐™๐™–๐™ฉ๐™– ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™œ๐™š๐™ ๐™ช๐™ฌ๐™– ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™–๐™ช๐™ฏ๐™– ๐™ก๐™ž๐™ฉ๐™– ๐Ÿค๐Ÿข ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐Ÿฃ๐Ÿข๐Ÿข ๐™ก๐™–๐™ ๐™ž๐™ฃ๐™ž ๐™จ๐™–๐™ž๐™ฏ๐™ž ๐™ ๐™–๐™ข๐™– ๐™ซ๐™ž๐™ก๐™š ๐™ฌ๐™–๐™ฃ๐™–๐™ฉ๐™ช๐™ ๐™ค๐™ข๐™ค๐™– ๐™ฉ๐™ช๐™จ๐™ž๐™ค๐™ ๐™ช๐™ฌ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™–๐™—๐™ค๐™ข๐™—๐™–
๐Ÿ˜โ‚ฉโ‚ฉโ‚ฌ #โ‚ฌยฃโ‚ฉยฅ# โ– โ—‡ยฃยฃโ‚ฉยฃยฃยฅ โ‚ฉยฃโ‚ฌยฃ&/#
 
Back
Top Bottom