Bei ya Magari "KUPATANA"

spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,719
6,253
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu,kuna huu mtandao wa kuuza na kununua bidhaa unaitwa kupatana,binafsi nimejikita kwenye magari baada ya kuona bei za watu wanayoyauza ,hivi kuna member yeyote mwenye ushuhuda wa kununua gari kupitia huu mtandao..........kifupi nimeona bei ya magari kidogo ni nafuu sasa najiuliza huo unafuu unaendana na bei ya gari husika bila magumashi yeyote ya gari yenyewe ama muuzaji.
 
Attachments

  • Screenshot_2016-02-08-20-13-33.png
    Screenshot_2016-02-08-20-13-33.png
    105.3 KB · Views: 1,556
  • Screenshot_2016-02-08-20-13-47.png
    Screenshot_2016-02-08-20-13-47.png
    147.8 KB · Views: 1,241
  • Screenshot_2016-02-08-20-14-04.png
    Screenshot_2016-02-08-20-14-04.png
    125.4 KB · Views: 1,240
  • Screenshot_2016-02-08-20-14-36.png
    Screenshot_2016-02-08-20-14-36.png
    149.8 KB · Views: 1,236
  • Screenshot_2016-02-12-17-08-16.png
    Screenshot_2016-02-12-17-08-16.png
    112.9 KB · Views: 1,225
Mimi nishafanya biashara sana kupitia mtandao huo!alafu tambua bei za magari na Vitu vingine vinawekwa na wamiliki/wauzaji na elewa siyo kila mwenye mali yKe mule ni mmiliki wako pia madalali wana post magari na Vitu vingine mule.
 
Je sio kwamba hizo bei ni bila kodi?
 
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu,kuna huu mtandao wa kuuza na kununua bidhaa unaitwa kupatana,binafsi nimejikita kwenye magari baada ya kuona bei za watu wanayoyauza ,hivi kuna member yeyote mwenye ushuhuda wa kununua gari kupitia huu mtandao..........kifupi nimeona bei ya magari kidogo ni nafuu sasa najiuliza huo unafuu unaendana na bei ya gari husika bila magumashi yeyote ya gari yenyewe ama muuzaji.
kwahizo bei mimi nina wasiwasi
 
Kuna matapeli mitandaoni
ila huko kupatana elewa kuwa sio mtandao wa kupatana unaouza magari
ni watu binafsi

kinachofanyika unakuta mtu biashara yake ni kuuza magari na anayo mengi
anaweka moja na kuweka bei nafuu sana
ukiuliza atakwambia njoo ulione
ukifika anakwambia keshaliuza ila anayo mengine ambayo bei sio nafuu kama lile alilotangaza

ni mbinu ya biashara...ni sawa na supermarket wanakutangazia sukari bei nafuu kuliko kote
ukiingia unajikuta unanunua vingine vingi ambavyo hukupanga
 
Spleen....kuna watu wengine huwa wanakosea Ku type bei?ila ni kweli kwenye mitandao wapigaji wapo kuanzia wauzaji had wanunuzi!
Kikubwa ni umakini wa kufanya biashara tu
 
Back
Top Bottom