Bei ya bidhaa yazidi kupaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya bidhaa yazidi kupaa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Feb 25, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Keneth Goliama

  OFISI ya takwimu nchini imesema bei ya vyakula vingi imepanda kwa asilimia 26.2 ukilinganisha na mwaka jana ambapo ilikuwa ni asilimia 25.6 kipindi kama hiki.Taarifa hiyo inatolewa wakati wakazi wa miji mbalimbali wakiwamo wa Mbeya, Dar es Salaam , Dodoma, Mtwara na Mwanza wakilalamika juu ya kupanda kwa gharama za maisha hususan masuala ya vyakula.

  Ripoti kutoka Ofisi ya Takwimu iliyotolewa Februari 15 na kupatikana jana, bei ya vyakula nchini inazidi kupanda na kutishia maisha ya wakazi wake.

  Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu ,Dk Albina Chuwa alisema hali ya kupanda kwa gharama ya vyakula bado ni kubwa.Licha ya ripoti kuonyesha bei ya vyakula kuendelea kupanda kwa kiasi kidogo, lakini hali ya gharama ya vyakula katika masoko jijini Dar es Salaam na Mbeya inazidi kupanda.

  “Matumaini ya kushuka kwa bei ya vyakula yanazidi kuota mbawa kutokana na hali ya bei inayozidi kupaa kila siku,’’ alisema.

  Nao wafanyabiashara wa maeneo mbalimbali jijini hapa walilalamikia kupanda kwa maisha pamoja na bei ya vyakula.Wafanyabiashara katika Soko la Buguruni walisema hatua ya kupanda bei ya vyakula kama nyanya, maharage mchicha, mchele na unga kunatokana na usimamizi mbaya wa uchumi nchini.

  Bei ya nyanya moja sasa ni Sh250, bei ya kilo moja ya maharage ni Sh 2,000, bei ya Sukari Sh2,500 kwa kilo na vishina vitatu vya mchicha ni Sh300, embe moja Sh800 wakati bei ya mananasi ni Sh2,000.

  Wakitoa maoni yao juu ya sababu za kupanda kwa bei hiyo walisema ni kutokana na kuongezeka kwa nauli ya usafirishaji wa mazao.Matha Mereni mfanyabiashara wa nyanya alisema jambo lingine linalochangia ni kuwapo kwa soko huria ambapo mazao mbalimbali sasa yamepata soko katika nchi za Afrika Mashariki.

  Naye Hamisi kajuru alisema Serikali imeshindwa kuzuia bei ya usafirishaji ndio maana Watanzania hasa wanaoishi jijini Dar es Salaam wanaendelea kupata maumivu ya bei ya vyakula kila siku.

  Lakini wengine walifafanua kwamba kuongezeka kwa bei ya vyakula kunatokana na kuongezeka kwa walaji wakati wazalishaji wakipungua.Walitoa wito kwa Serikali kutoa motisha kwa wakulima ili vijana wengi wakipende kilimo
  Bei ya bidhaa yazidi kupaa
  Chanzo.
   
 2. n

  naivasha Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Achana na habari ya asilimia!!!!!!!!! Huo ndo mfumuko. Sasa hivi mfumuko kila siku, kila mahali, kila kitu na unazidi kutamalaki. Hakika tumeshikwa pabaya. Ebu tuone pengine jamaa anaweza kuibuka na "Marshall Plan II"
   
 3. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  poleni walaji, Narubongo mwaka huu anampango wa kujenga ghorofa. Sasa hivi nipo bar nasheherekea matunda ya kilimo kwanza na ufugaji wa kisasa
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Hii kwa wajasirimali ni Oportunity za kutosha na wajasiriamali hawapaswi kulalamika kabisa hapa, wakati wa Vita kuu ya Pili ya Dunia hali ya kibiashara na maisha ilikuwa mbaya sana ila ilitoa funzo kwa watu wa lika zote.

  1. Kwa wajasirimali- Kuna watu walitumia Vita kuja na idea ambazo zimewafanya kuwa mabilionea hadi leo hii, Viwanda vingi vya kutengeza zana mbalimbali za kivita zilianzishwa kipindi hicho cha vita

  2. Kwa raia wa kawaida- wengi walipata funzo na ndo maana baada ya vita wanawake hawakutaka kuzaa tena kwa kuhofia kwamba watoto wao watakuja kwenda vitani na pia kwa kohofia matunzo

  So hali inavyo kuwa mbaya ni funzo la kubana matumizi na kuja na mbinu mbadala
   
 5. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 180
  mtalalamika sana sana na bado, mbona bado sn mtakoma, hatuweki mikakati yoyte kudhibiti hiyo hali ngumu ya maisha, mtakoma
   
Loading...