PreGE2025 BAZECHA: Tuliwaita kujieleza badala yake wakakimbia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
57,913
Reaction score
133,926
Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA) limeeleza kuwa liliwaita viongozi na wananchama wote ambao walikua na manung’uniko katika chama kuja kujieleza ili kutafuta suluhu na badala yake hawakutokea na kuanza kujiengua

“Mwenyekiti mstaafu alishawai kusema kwama kiundwe chombo ambacho kitasaidia kuponya majeraha, tulishakaa na mwenyekiti mbowe, lissu na katibu Mkuu kwakua watu walidhani wamekanyagana tulitoa nafasi ya watu waje kujieleza ni nani amekanyagwa na kakanywagwa na nani ki vipi, fursa hiyo tuliitoa ndani ya Chama na hawakujitokeza matokeo yake tumesikia kwamba mtu kashuka ndani ya basi katulia njia panda, ni wahakikishie baraza la wazee baada ya kuchunguza chama kipo imara kuliko wakati mwingine wowote bahari inatema uchafu wacha bahari iwe safi”

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ayo yamesemwa na Mwenyekiti wa BAZECHA Kanda ya pwani, James Haule wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.

My Take
Tatizo lenu mliwaita kuwahoji badala ya kuwapa funguo za duka
 
Mi nachukia sana na hii hama hama, japo wanasema siasa haina adui wa kudumu,

Ila ikitokea siku hawa wanaohama saizi mmoja wapo akirejea bado moyoni nitakua na chuki nae,

Maana wametuthaliti kipindi muhimu kuliko wakati wowote kwa harakati za upinzani nchi hii.
 
Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA) limeeleza kuwa liliwaita viongozi na wananchama wote ambao walikua na manung’uniko katika chama kuja kujieleza ili kutafuta suluhu na badala yake hawakutokea na kuanza kujiengua

“Mwenyekiti mstaafu alishawai kusema kwama kiundwe chombo ambacho kitasaidia kuponya majeraha, tulishakaa na mwenyekiti mbowe, lissu na katibu Mkuu kwakua watu walidhani wamekanyagana tulitoa nafasi ya watu waje kujieleza ni nani amekanyagwa na kakanywagwa na nani ki vipi, fursa hiyo tuliitoa ndani ya Chama na hawakujitokeza matokeo yake tumesikia kwamba mtu kashuka ndani ya basi katulia njia panda, ni wahakikishie baraza la wazee baada ya kuchunguza chama kipo imara kuliko wakati mwingine wowote bahari inatema uchafu wacha bahari iwe safi”

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ayo yamesemwa na Mwenyekiti wa BAZECHA Kanda ya pwani, James Haule wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.

My Take
Tatizo lenu mliwaita kuwahoji badala ya kuwapa funguo za duka
Duka?
 
Hivi mtu utaanzia wapi kustuka kwa hawa wanaotoka ndani ya CHADEMA wakati huu, kwamba chama kinadhoofika; wakati ipo wazi kabisa kwamba kuondoka kwao ni kwa manufaa ya chama?

Hawa wote wangebaki ndani ya chama, wangesumbua sana hawa, na inawezekana kabisa wakati ungefika wakatumiwa kukisambaratisha chama moja kwa moja.

Kuondoka kwao ndiyo imekuwa nafuu ya CHADEMA
 
Aliyetukana ni mwingine anayeenda kuomba msamaha ni mwingine,watanzania hatuko hivyo,uungwana ni vitendo,kwa nini walipokuwa wanatukana hawakuwatuma BAZECHA wakawasaidie kutukana.
 
Back
Top Bottom