Bayport na mikopo

Bayport na mikopo

mhhh utajuta!!!na hilo banda unaweza kuliuza kabsaaaaa
 
Angalia kwanza interest rate zao - they are sharks! watakumeza mzima mzima!
 
Mkuu Mwana... unafahamu maana ya "loan shark"?
Unataka ku-rostika?
Hao jamaa ni loan sharks tu. Tofauti yao na Loan Sharks wa mitaani ni kuwa wao wana viji-ofisi na leseni ya kudhurumu.

Ni noma!!
 
kama wewe ni mtumishi angalia uwezekano wa kukopa benki ya POSTA au NMB wana riba nafuu....hao jamaa watakuua kwa ukubwa wa riba zao.
 
Kama unataka kulia hapo panafaa kimbia kama ukóma mkopo nafuu ni nbc 20% interest nmb zaid mayb 22hv
 
Nackia ukikopa hapo makato huwa hayaishi. Wataendelea kukukata mpka uende mahakamani. Wengi wanamalizana nao mahakamani. Achana nao kabsaa
 
mkuu skushauri kabisa hao jamaa ni madhulumati watupu hako kabanda unakotaka malizia watakudhulumu
 
Hapana usisikie ya watu njoo ofisini kwetu tuongee ,utapata mkopo kadri utakavyo tena kwa mda mfupi sana .KOPA KWA MAAENDELEO KOPA BAYPORT

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Hapana usisikie ya watu njoo ofisini kwetu tuongee ,utapata mkopo kadri utakavyo tena kwa mda mfupi sana .KOPA KWA MAAENDELEO KOPA BAYPORT

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
wewe acha uongo! nani asiyewajua ninyi bayport? riba kubwa na makato hayaishi mpaka kupelekana mahakamani! sijui kwa nini Serikali haijawamulika unless kama kuna vigogo wa Serikali wana hisa bayport!
KOPA UFILISIKE KOPA BAYPORT!
 
Shauri yako! Kama utaweza kuhimili riba ya asilimia 400% ruksa kwenda kuchukua umalizie banda lako. Nina maana utakachochukua utarudisha maranne ya ulichokopa. Akili kumkichwa! Kwavile umeomba ushauri basi ni juu yako kuamini tukuambiayo au ukaacha kuamini kwa vile ni hiyari na hakuna anayekulazimisha.
 
mbona utajuta, mama yangu aliwahi kuomba milion 2, wakampa laki 7 afu wakaanza kukata 64000 kila mwezi kwa 3yrs. Deni limeisha wanaacha afu wanashitua mwezi 1 wanaacha tena, yani majanga
 
... kuna mtumishi wa Serikali alikopeshwa 800,000 mwaka jana. Analipa Sh 98,000 kwa mwezi kwa miaka mitano! Akiwaomba wampe hata mchanganuo wa mkopo wake wanaleta kona kibao!

Kwa ufupi, kopa kwa hao jamaa, andaa na mazishi yako - hawafai! Bayport, FINCA, Blue (kama bado wapo), PRIDE, nk, wote na walewale tu.

Mkopo? Nenda Benki. Angalau BoT wana-kausimamizi kiasi!
 
Ndugu mteja huduma zetu zimeboreshwa acha kusikiliza maneno ya mtaani kwa watu ambao hata sifa ya kukopa hawana ndo mana unasikia sijui mama alikopa ,achana na majumbu njoo ukope kwa faida yako

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
... poa!
Ninajipanga kurudi Shule. Mara hii kusomea Sheria. Nitajikita kwenye Law of Torts. Wa kwanza kuwabana ni Bayport, Blue, FINCA, Pride na Loan sharks kama nyinyi. Wateja wangu wa awali watakuwa Walimu, Manesi, n.k. nipatieni miaka 2 tu!!
 
Kama unajua siku zako za kuishi zimefika ukingoni au unafukuzwa kazi nenda ukope bayport kwa hao wezi wa mama mkapa. Nilikopa laki 8 mwaka 2008 february walikikata elfu 73 kwa miaka 3 mpaka elfu 2011.
Hao ni majambazi wa kutupilia mbali hapa tanzania.
Tena umshauri na ndugu yako asifanye makosa akakopa kwa hao majangili wa mishahara ya watu.
 
Ndugu mteja huduma zetu zimeboreshwa acha kusikiliza maneno ya mtaani kwa watu ambao hata sifa ya kukopa hawana ndo mana unasikia sijui mama alikopa ,achana na majumbu njoo ukope kwa faida yako

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

huna lolote usitudanganye hapa, hata wenzako wanasema hivyo2 wakati wakitafuta wateja wa kuwakopesha.
 
Back
Top Bottom