Bayi apenya mkutano mkuu CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Na Dina Ismail

MWANARIADHA mahiri wa zamani na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) hivi sasa, Meja mstaafu Filbert Bayi, amefanikiwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwakilisha Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Bayi amefanikiwa kukata tiketi hiyo kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni, baada ya kupata kura 264, ambapo ataungana na Mary Sulley kura 545, Ori Pembe (kura 460), Fabiola Deo (kura 456) na Amsi aliyepata kura 322.

Katika uchaguzi huo, nafasi ya uenyekiti wa wilaya, ilikwenda kwa Mustafa Mbwambo aliyepata kura 512 na kumwangusha Gerald Gwaha aliyepata kura 148, huku mgombea mwingine aliyefahamika kwa jina la Tippe akijitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa upande wa nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC), Awaki Tlemai, alishika nafasi ya kwanza kwa kupata kura 545 akifuatiwa na Daniel Ilakwahhi kura 114.

Huyu ni shujaa aliyesaulika. Ni bahati mbaya kuwa CCM hiyo hiyo iliyomtelekeza bado ni mwanachama wake. Na hili ndilo tatizo la watanzania walio wengi ingawa si wote. Hili ndilo tatizo kubwa la rafiki yake Fred Sumaye. Woga na kudhani kuwa nje ya CCM hakuna maisha.
 
Hivi ni kweli Samwel Sitta anayajua ?? VIONGOZI woooote wanakimbilia Uongozi CCM ?? Wote wenye Vibiashara Vishule; Viwanda; Mashamba; Wizarani - woote wanaCCM ?

Hadi Filbert Bayi ? ni nini anataka CCM na Ametosheka ? [eti, nadhani Ametosheka]
 
Huyu ni shujaa aliyesaulika. Ni bahati mbaya kuwa CCM hiyo hiyo iliyomtelekeza bado ni mwanachama wake. Na hili ndilo tatizo la watanzania walio wengi ingawa si wote. Hili ndilo tatizo kubwa la rafiki yake Fred Sumaye. Woga na kudhani kuwa nje ya CCM hakuna maisha.

Mtoto wake mmoja anaitwa Englibart sijui yuko wapi
 
hakuna mtu mbaya kama anayeona maovu na kushindwa kuyakemea ni mwovu kuliko anayeyatenda maovu hayo,
Bayi anajua wazi jinsi CCM inavyoangamiza nchi hii badala ya kukemea anakwenda kujiunga nao naye anakuwa kwy
kundi la pili la watu wabaya kuliko mafisadi.
 
Kweli ndio maana tunapata marais legelelege kweli wana ccm mnamchagua Bayi ambaye hata kusimamia timu ya olimpiki anashindwa, kweli bado tuna safari ndefu kweli kwa upuuzi kama huu ccm itaongoza milele tanzania.
 
kweli inashangaza mno hata CHADEMA kuongozwa na mtu aliyeshindwa kuwaongoza KONDOO wa BWANA akageuka kuwatafuna na kuwapa mimba hahahaha inashangaza kweli CCM itaongoza Daima ika
 
Huyu ni shujaa aliyesaulika. Ni bahati mbaya kuwa CCM hiyo hiyo iliyomtelekeza bado ni mwanachama wake. Na hili ndilo tatizo la watanzania walio wengi ingawa si wote. Hili ndilo tatizo kubwa la rafiki yake Fred Sumaye. Woga na kudhani kuwa nje ya CCM hakuna maisha.

mbona ni mwizi tu huyo? kaiba hela za toc kumbe ni kwa ajili ya kampeni.
 
LOL! Sikujua hili. Mie namfahamu Bayi wa miaka ya 80 alivunja rekodi ya dunia wenzake wakachukuliwa na nchi tajiri yeye akadanganywa na kurejea nchini eti ni uzalendo. Kumbe kaishia kuwa kibaka! Kweli Tanzania ni chuo cha ujambazi na ufisadi!
 
Yaani pamoja na mbio zake na kuvunja santuri ya dunia, Bayi kaambulia kura 264, mwanamama mtembea kwa miguu Mary Sulley kampita kwa kura 545, Ori Pembe (kura 460), Fabiola Deo (kura 456) na Amsi aliyepata kura 322. Yaani kawa wa mwisho miongoni mwa wajumbe wateule.
 
Na Dina Ismail

MWANARIADHA mahiri wa zamani na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) hivi sasa, Meja mstaafu Filbert Bayi, amefanikiwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwakilisha Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Bayi amefanikiwa kukata tiketi hiyo kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni, baada ya kupata kura 264, ambapo ataungana na Mary Sulley kura 545, Ori Pembe (kura 460), Fabiola Deo (kura 456) na Amsi aliyepata kura 322.

Katika uchaguzi huo, nafasi ya uenyekiti wa wilaya, ilikwenda kwa Mustafa Mbwambo aliyepata kura 512 na kumwangusha Gerald Gwaha aliyepata kura 148, huku mgombea mwingine aliyefahamika kwa jina la Tippe akijitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa upande wa nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC), Awaki Tlemai, alishika nafasi ya kwanza kwa kupata kura 545 akifuatiwa na Daniel Ilakwahhi kura 114.

ahaaaaaaaaaaaaaaaaa,kumbeeeeeeeeeee.

ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona...........
 
Kauli ya sumaye enzi zile " ukitaka mambo yako yanyooke njoo ccm" mngetaka Bay afanyaje wakati yeye ndiye. ! Njoo ccm shule ziwe. Za 3anzania ili kusaidia tanzania ishike nafasi yÀkwanza kimataifa
 
LOL! Sikujua hili. Mie namfahamu Bayi wa miaka ya 80 alivunja rekodi ya dunia wenzake wakachukuliwa na nchi tajiri yeye akadanganywa na kurejea nchini eti ni uzalendo. Kumbe kaishia kuwa kibaka! Kweli Tanzania ni chuo cha ujambazi na ufisadi!

humo jf wengi ni wageni sana katika siasa ya nchi hii na wengi hatufahamu kabisa mambo mengi filbert bayi amewahi kugombea ubunge jimbo la karatu mwaka 2005 na pia nafasi hiyo aliyogombea amekuwa nayo tangu mwaka 2002 hivyo hakuanza leo
 
Back
Top Bottom