BAWACHA hakuna kulala, leo kutikisa Magu, Uwanja wa Sabasaba

CHADEMA

Political Party
Joined
Apr 13, 2013
Posts
495
Reaction score
2,540
Mapokezi ya kimalkia yanawasubiri wapiganaji wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), wakiongozwa na Mwenyekiti wao Taifa, Halima Mdee, leo mjini Magu wakitokea Ukerewe walikofanya mkutano mkubwa jana Uwanja wa Nansio.

Makamanda wamepiga moja kwa moja kutoka Ukerewe kwenda Magu kuwahi mkutano wa leo ambao wananchi wa mji huo na vitongoji vyake wanausubiri kwa hamu kubwa kupata elimu juu ya uchakachuaji wa Katiba Mpya, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, maandalizi ya Kura ya HAPANA kwa Katiba Mpya ya CCM, maandalizi ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Tayari msafara umeshaingia mjini Magu na mkutano utafanyika Uwanja wa Sabasaba.

Wanapiga 'hakuna kulala mpaka kieleweke' kwa vitendo.

Waunge mkono BAWACHA katika Operesheni hii ya 'DELETE CCM, FUTA KABISA'
 
Wapeni ruhusa hao wanawake wakasalimie hata kidogo familia zao nyumbani.. Mwezi umeshaisha hawajakanyaga majumbani mwao. Kama kuna wake za watu mwisho wataachika.. Mwenzao Halima Mdee ni seniour bachela hana mume hata akikaa mwaka bila kurudi nyumbani kwake anaona poa tu.
 
Chadema ni zaidi ya Maji Usipokunywa Utaogea Asante sana Chadema mkombozi wa wanyonge wa nchi hii. Mwaka huu tutaelewana tu
 
Kumbe ndiyo maana Mdee alipewa ile tuzo? Huyo mtoto ni chui! CCM angalieni mnazama!
 
Hakika wanawake wa CHADEMA hakuna anayeweza kujitia kura yake kwa kumchagua Halima Mdee na timu yake'
 
Wapeni ruhusa hao wanawake wakasalimie hata kidogo familia zao nyumbani.. Mwezi umeshaisha hawajakanyaga majumbani mwao. Kama kuna wake za watu mwisho wataachika.. Mwenzao Halima Mdee ni seniour bachela hana mume hata akikaa mwaka bila kurudi nyumbani kwake anaona poa tu.

Aisee hadi unapumulia masikio kweli ebola imeingia ndani ya CCM sasa hakuna atakayesalimika pona yenu labda mhamie Ukawa ndio kuna yule nyoka wa shaba ukimtizama tu tayari umepata uponyaji amini hivyoo.
 
Wapeni ruhusa hao wanawake wakasalimie hata kidogo familia zao nyumbani.. Mwezi umeshaisha hawajakanyaga majumbani mwao. Kama kuna wake za watu mwisho wataachika.. Mwenzao Halima Mdee ni seniour bachela hana mume hata akikaa mwaka bila kurudi nyumbani kwake anaona poa tu.

VUTA-NKUVUTE ajirini hata waliomaliza form four huyu hata neno senior hawezi kuandika halafu anataka wanawake wenzake warudi nyumbani wakati yeye hajaolewa
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa kutujuza, uwe unatupa update kwa wakati.
 
Go go go go go BAWACHA..Hakuna kulala mpaka kieeweke...Hii harakati haitaicha CCM salama..
 
Mapokezi ya kimalkia yanawasubiri wapiganaji wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), wakiongozwa na Mwenyekiti wao Taifa, Halima Mdee, leo mjini Magu wakitokea Ukerewe walikofanya mkutano mkubwa jana Uwanja wa Nansio.

Makamanda wamepiga moja kwa moja kutoka Ukerewe kwenda Magu kuwahi mkutano wa leo ambao wananchi wa mji huo na vitongoji vyake wanausubiri kwa hamu kubwa kupata elimu juu ya uchakachuaji wa Katiba Mpya, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, maandalizi ya Kura ya HAPANA kwa Katiba Mpya ya CCM, maandalizi ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Tayari msafara umeshaingia mjini Magu na mkutano utafanyika Uwanja wa Sabasaba.

Wanapiga 'hakuna kulala mpaka kieleweke' kwa vitendo.

Waunge mkono BAWACHA katika Operesheni hii ya 'DELETE CCM, FUTA KABISA'
Safi sana weka picha mkuu
 
Back
Top Bottom