Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA (BAWACHA) Kanda ya Kati Emmy Kibatala amesema kuhama kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho hakujawateteresha hasa kuelekea uchaguzi mkuu ambapo amedai watashiriki ikiwa mifumo ya uchaguzi itawekwa sawa
Akizungumza katika Baraza la Mashauriano Mkoa wa Morogoro lililofanyika siku ya Jumatatu, Makamu Mwenyekiti huyo amesema kwenye kanda hiyo yenye majimbo 30 viongozi waliohama CHADEMA na kujiunga na vyama vingine ni wimbi tu linalopita na kanda iko imara kukilinda chama chao
Aidha Emmy Kibatala amesema katika kuendelea kuijenga kanda ya kati, BAWACHA wamepanga kuanza mikutano kuanzia Juni 4, 2025 ili kujenga uelewa kwa Watanzania juu ya dhamira ya chama hicho.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
BA