Achana na hilo la CHADEMA vs ACT, mimi nimeshatabiri kwamba serikali ya awamu ya tano itakaa madarakani kwa awamu moja tu ya miaka mitano. Kwa sababu maisha yanazidi kuwa magumu kila uchao. Jana tumeambiwa madaktari wa hospitali za rufaa wamepunguzwa mishahara kwa 30%, juzi tuliona kupitia ITV taarifa kwamba mizigo imepungua huko kwenye bandari kavu hata waajiri wanafikiria kupunguza wafanyakazi. Huku mtaani nako hali ni mbaya hadi inafikia wananchi kuunga chumvi kwenye chai. Ni watanzania wachache sana wanaoipenda CCM hasa ni wale walionufaika kwa kuteuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali pamoja na familia zao.