THE COMMISSIONER
JF-Expert Member
- Dec 3, 2012
- 267
- 111
Baraza la vijana la Chadema (BAVICHA) wiki hii tena litawaleta pamoja vijana wa vyama vya Demokrasia Afrika Mashariki kwenye mkutano wa siku mbili utakaojadili Changamoto za Vijana wa ukanda huu.
BARAZA la Vijana wa CHADEMA kwa mara nyingine litakuwa mwenyeji wa mkutano wa vijana wa vyama vya kidemokrasia kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkutano huu utakaofanyika kuanzia tarehe 6 -8 Desemba kwenye hoteli ya Protea Courtyard Jijini Dar es salaam utajumuisha vijana 40 kutoka mataifa wanachama wa umoja wa vyama vya kidemokrasia Barani Afrika (DUA) kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Pia mkutano huu utawahusisha wageni maalumu kutoka nchini Ghana na wabunge kutoka Uingereza ambapo mfunguzi mkuu anatarajiwa kuwa Mh Freeman Mbowe (MB) Mwenyeikiti wa CHADEMA Taifa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.
Mkutano huu uliopangwa kufanyika Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya mafanikio ya Mkutano wa (IYDU) uliofanyika mwezi Julai jijini Dar es salaam, utajikita zaidi katika kujadali kanuni na misingi mikuu ya mrengo wa kati kulia ambao ni itikadi ya CHADEMA na jinsi ya kufanikisha vyama vya mrengo huu kukamata dola.
Mkutano pia utaangalia changamoto mbali mbali za vijana wa Afrika Mashariki na jinsi vyama vya mrengo wa kati kulia (Center Right Parties) vinavyoweza kuzitatua pindi viwapo madarakani.
BAVICHA kuwa mwenyeji wa mkutano huu kunatokana na ukweli kuwa yenyewe imedhihirisha kuwa ni oganaizesheni thabiti ya Vijana sio tu kwa Afrika Mashariki bali pia kwa bara la Afrika .
Aidha, BAVICHA kuendelea kuwa mwenyeji wa mikutano ya kimataifa ya vijana ya aina hii ni ishara ya jinsi taasisi hii inavyoaminiwa na jumuiya za vijana za kimataifa kama ilivyo kwa chama mama CHADEMA na hivyo kudhihirisha jinsi vijana makini wa chama makini wako teyari kuyakamata mamlaka ya nchi kwa ajili ya kujenga taifa makini la Tanzania
Pia Mkutano huu ni muendelezo wa heshima kwa BAVICHA, CHADEMA na Tanzania kwa ujumla kutoka kwenye jumuiya mbali mbali za kimataifa
2. KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA TANZANIA BARA
BAVICHA kwa upande mwingine imepanga kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya kongamano kubwa la vijana na watanzania kwa ujumla jijini Dar es salaam.
Msingi mkuu wa kongamano hili litakalohusisha vijana wa Chadema wa majimbo ya Dar es salaam, wanafunzi wa Chadema wa vyuo vukuu vilivyoko jijini Dar es salaam pamoja na viongozi wa kitaifa wa CHADEMA ni kutoa tathmini halisi ya hali ya taifa kwa kipindi cha miaka 52 na mwelekeo mbadala kutoka Chama Mbadala.
Mgeni rasmi wa kongamano hili litakalofanyika tarehe 09.12.2013 kwenye ukumbi wa Landmark Hoteli Ubungo atakuwa Mh FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB), Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Mh Mbowe atatumia maadhimisho haya kuzungumza na vijana wa Dar es salaam juu ya mustakhabali wa nchi hususani masuala muhimu yanayolikabili taifa kwa sasa.
Mh Mbowe ataambatana na Mh Tundu Lissu, John Mnyika, Mabere Marando, Halima Mdee na Dr. Kamilius Kasala, mbobezi wa masuala ya uchumi nchini.
Imetolewa leo tarehe 05.12.2013 Jijini Dar es salaam na;
Deogratias Munishi
Katibu Mkuu- BAVICHA
+255715 887712
BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
1. MKUTANO WA VIJANA WA VYAMA VYA KIDEMOKRASIA AFRIKA MASHARIKITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI