BAVICHA Taifa
Senior Member
- Jul 25, 2013
- 117
- 661
Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) tunalaani kitendo cha Serikali kuvunja vibanda vya wafanyabiashara/wajasiriamali wadogo katika Soko Kuu la Kariakoo, Jijini Dar Es Salaam.
Tukio hili ni la kinyama na halina utu ndani yake kwani limewasababishia vijana wengi umasikini na ufukara baada ya bidhaa zao kuchukuliwa na mgambo wa jiji waliyokuwa wakiendesha operesheni ya kuvunja vibanda vyao.
Ikumbukwe kuwa Serikali imeshindwa kutoa ajira kwa mamilioni ya vijana wanaomaliza vyuo na shule mbalimbali hapa nchini kwa muda mrefu, inasikitisha kuona kuwa vijana wanapojitahidi kujiajiri wenyewe, Serikali inawaumiza badala ya kuwasaidia ili waweze kujikwamua na ugumu wa maisha.
Tunaitaka Serikali ieleze hawa vijana wamachinga eneo lao la kufanyia biashara liko wapi? na je, Kariakoo siyo kwa ajili ya vijana wa Kitanzania? Nani mwenye haki na Soko la Kariakoo?
Kitendo hiki kinaweza kusababisha ongezeko la uhalifu mitaani kwani hawa vijana hawatakuwa na kazi na hivyo kukosa kipato cha kujikimu.
Serikali iweke miundombinu ya vijana kujiajiri na kamwe isiwe kikwazo kwa vijana kujikwamua kiuchumi.
Imetolewa leo Disemba Mosi, 2022.
Apolinary Boniface,
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano BAVICHA.