BAVICHA Mnafanya nini?

BAVICHA Mnafanya nini?

Hahaha hahaha unajaribu kuwagawanya wapiganaji. Acha hizo. Hautaweza.

mkuu,pengine sijui mkakati unaoendelea hapa,nimeona majibizano ya hawa jamaa na Ben kwenye thread moja hv,sasa nashangaa huyu Chadema kwanza anamshambulia kila mtu aliekua upande wa Ben.
Samahani kama na mm nitakua msaliti kwa hili.
ALL IN ALL MAKAMANDA TUSIRUHUSU MGAWANYIKO MUDA HUU!
 
BAVICHA kupitia kwa Makamu Mwenyekiti Taifa Ole sosopi wamefanya harakati nyingi tu mikoa ya Iringa,Dodoma,Mbeya na juzijuzi mkoa wa Kagera.
Kote huko wametoa elimu ya uraia pamoja na kuongeza wapiga kura wapya.
Mimi nisichokiona ni harakati za Mwenyekiti wa BAVICHA kamanda Patrobas.
Huenda kabanwa na majukumu yake ya ajira lakini hili si alilitambua alipokuwa anaomba hiyo nafasi?
 
Hoja hii ni ya msingi sana. Hatuoni kazi ya uongozi wa Bavicha hadi sasa. Kweli amkeni unganisheni vijana, hamasisheni watu kujiandikisha, ingieni vijijini, changisheni fedha za kampeni. Fanyeni kazi banaaaa!!

wako busy kuanzisha threads jf
 
Mpaka saiz anayeonekana anatekeleza majukumu yake ipasavyo ni Patrick Ole Sosopi peke yake...!
 
mbona sioni harakati za BAVICHA mikoa ya kanda ya kati (Dodoma na Singida) maana hii mikoa inahitaji juhudi za ziada kidogo kuwapa elimu wananchi wa hii mikoa ili waweze kuachana na CCM. Tafadhali BAVICHA hebu iangalieni hii mikoa ya kanda ya kati maana kama tunahitaji ushindi hapo Oktoba na hii mikoa kura zake zinahitajika
 
Operesheni Delete CCM ambayo iliwaonesha CCM 'rangi zote' kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ilisimamiwa na BAVICHA waliokwenda kwa staili ya infantry (wakati Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu Dk. Slaa wakipiga angani), mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma.

Majuzi wamefanya ziara ya mkoa mzima wa Kagera ambako walizindua operesheni kubwa itakayosambaa nchi nzima kuhusu kujiandikisha na kupiga kura, na sehemu ya Geita. Infantry kaka ndiyo inayoongoza vita.

Wakati unasubiri kuwaona 'wakipiga makelele', vijana wanakwenda chini kwa chini na athari yao kote wanakopita majibu wanayo CCM.

Asante Kiongozi wangu kwa kunifahamisha. Nimefunguka macho
 
Heche tulia na mwenzio afanye kazi
Ukisoma Takwimu hizo za baraza la taifa la Takwimu (National Bureau of Statistics | Statistics for Development) ni kwamba zaidi ya watanzania milioni 30 ni Vijana.Hawa ndio BAVICHA inabeba matumaini yao yote.

Kati yao Milioni 22 ni vijana na watoto chini ya miaka 17.BAVICHA ianabeba matumaini yao.

BAVICHA Inatakiwa itambue kwamba serikali iliyopo imeshindwa kulisaidia taifa hili hasa katika hali ya maisha ,elimu,afya ,ajira,kuondokana na subsistence economy n.k

BAVICHA walifanya Uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana na kupata viongozi wapya

Cha kushangaza sana baraza hili limekuwa kimya kupita kiasi....hakuna kazi zozote zinazoonekana kufanywa na baraza hili....Tulitarajia katika wakati huu vijana hawa wangekua field kuhamasisha wananchi katika mazoezi anuwai ya kitaifa....hasa ukiwa ni mwaka wa uchaguzi mkuu...hatujasikia comment zozote za BAVICHA katika maswala mazito yaliyolikumba taifa....Naomba kukumbusha...Taifa letu ni taifa la Vijana...YOUTH agenda sio ya kukwepa...Wameshindwa kujua kuwa wanabeba matumaini ya idadi kubwa ya Vijana.?

Nauleta huu uzi kwenu ili tuweze kuchambua na kuliweka wazi tatizo la BAVICHA ili waweze kulisaidia taifa kuvuka katika mkwamo huu.

[h=1][/h][/QUOTE]
 
mkuu,pengine sijui mkakati unaoendelea hapa,nimeona majibizano ya hawa jamaa na Ben kwenye thread moja hv,sasa nashangaa huyu Chadema kwanza anamshambulia kila mtu aliekua upande wa Ben.
Samahani kama na mm nitakua msaliti kwa hili.
ALL IN ALL MAKAMANDA TUSIRUHUSU MGAWANYIKO MUDA HUU!

Ukiwa kwenye msimamo wa chama au Mwenyekiti, kamwe huwezi kuwa huru katika kueleza mtazamo wako.
 
Sio kila anayetifautiana na wewe kimtazamo nankifikra basi unampa jina la ACT au msaliti, hizo sio siasa mkuu.

Mm ninachoshangaa kama Chadema inakuwa kwanini inahofu uwepo wa ACT.Hii ni nchi ya Demokrasia,acheni kila mtu awe huru.
 
Operesheni Delete CCM ambayo iliwaonesha CCM 'rangi zote' kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ilisimamiwa na BAVICHA waliokwenda kwa staili ya infantry (wakati Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu Dk. Slaa wakipiga angani), mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma.

Majuzi wamefanya ziara ya mkoa mzima wa Kagera ambako walizindua operesheni kubwa itakayosambaa nchi nzima kuhusu kujiandikisha na kupiga kura, na sehemu ya Geita. Infantry kaka ndiyo inayoongoza vita.

Wakati unasubiri kuwaona 'wakipiga makelele', vijana wanakwenda chini kwa chini na athari yao kote wanakopita majibu wanayo CCM.

Tumaini Makene,sehemu nyingi nimeona concetration kubwa ipo kwa vijana wa kiume,mmewasahau akina DADA na akina MAMA hawa ndiyo wapigaji kura wa ukweli.

Nimeona mara nyingi wanaume wanakaa pembeni na mwisho wa siku kuwalaumu akina mama kuwa wameipigia KURA CCM.Inabidi kuwe na mkakati mahususi wa kwenda nyumba kwa nyumba ili kuwaelimisha akina mama nini maana ya upinzani,na umuhimu wa kura yao kwa kiongozi bora.

Mfano mzuri wale waliompigia Joseph Mbilinyi(Sugu) wengi wao walikuwa wanawake watu wazima na si wanaume.Iangalieni hii,kwani ukimuelimisha mama mmoja umeielimisha jamii!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tumaini Makene nashukuru kujitokeza humu na kujibu baadhi ya hoja

Lakini naomba nikukosoe kidogo

BAVICHA kama taasisi haifanyi kazi pamoja.Kumekua na Juhudi zilizogawanyika za kila mtu kujifanyia anavyotaka
Sosopi anakomaa kufanya anayowza kwa sababu anajijenga yeye binafsi kwenda kwenye kugombea ubunge huko kwao Iringa .Na amefanya hizo Juhudi huko kwao Iringa.

Yule binti wa kule kagera naye amefanya kazi peke yake huko kwao bila shaka katika kujijenga yeye binafsi

Mwenyekiti Patrobas huyo ndiye amelala kabisa anategea alipo Mbowe na yeye anakwenda

Tunachotarajia kukiona ni BAVICHA kufanya kazi kama timu.BAVICHA wafanye movements za pamoja wakiwa timu kamili katika nchi nzima.Huu sio muda wa watu kulala na kuja na visingizio kibao.

Kazi za BAVICHA hazipaswi kuwa za kutafuta kwa tochi.Kwamba eti matokeo ya serikali za mitaa ni matokeo ya BAVICHA? Really? Je BAWACHA wasemeje,je baraza la wazee? je uongozi wa juu wa CHADEMA?

Patrobas atambue na ajitambue kazi aliyoomba ni ya kuwatumikia watanzania.Akusanye timu yake wafanye kazi.Aaamue kipi bora zaidi kwa sasa,Kama aliona ajira itambana ,kwa nini aligombea uongozi?
 
Last edited by a moderator:
Wimbo uliounukuu haujatoka nchi jirani ila tuliumba sana hapa nchini miaka ya 60s na 70s mashuleni na JKT wakati wa kukimbia machakamchaka. Nyimbo nyingine maarufu zilikuwa za kumlaani nduli Iddi Amin na Banda wa Malawi pia kuna nyingine na vibwagizo kibao kama "kaburu akija chija"
 
Fuatilia kabla hujacomment....
 
Bavicha wanafanya kazi nzuri tumeona mafanikio makubwa sana kwenye Operesheni FUTA DELETE KABISA CCM NCHI NZIMA lakini chakuongezea hapo Bavicha bado tuna changamoto kubwa sana hasa kutoa elimu vijijini kwani huko ndo uliopo mtaji mkubwa wa ccm kuwahadaa wananchi na kanga na kofia .
 
Mm ninachoshangaa kama Chadema inakuwa kwanini inahofu uwepo wa ACT.Hii ni nchi ya Demokrasia,acheni kila mtu awe huru.
Chadema hatuna hofu yoyote na uwepo wa Act tunajua hicho kikundi cha wahuni na wasaliti hawawezi kufika mbali
 
Sita Tetereka na watu kama nyie sanasana tutawa delete kwenye operation delete ccm

Utakuwa na stress kali za maisha,haiwezekani kila mtu usimwamini au ukorofishane nae.Akina Zitto na Slaa waliijenga CHADEMA kwa nguvu za hoja,lakini nyinyi mnaikwamisha CHADEMA kwasababu ya chuki zenu.
 
Back
Top Bottom