Bavicha Mkoa wa Iringa Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
BARAZA LA VIJANA MKOA WA IRINGA (BAVICHA)
06/07/2016

Taarifa kwa vyombo vya habari!

Ndugu waandishi wa habari, Awali ya yote naomba nianze Kwa kumshukuru Mungu Kwa kutujalia afya na uzima hata tukaweza kukutana hapa asubuhi ya leo tukiwa salama. Pia tunamshukuru Mungu kwaajili ya ndugu zetu waisilam kwa kufanikiwa kutimiza nguzo yao muhimu ya kiimani ya mfungo, Hivyo tunawatakia sikukuu njema ya EID EL FITRI.

PILI, Naomba kwa moyo mkunjufu na wa dhati kabisa, kutumia fursa hii ya kipekee kuwashukuruni ninyi waandishi wa habari kwa kukubali wito wetu na kuja kutusikiliza. Ni matumaini yetu kuwa mtatusikiliza kwa makini na kwa uhakika ili kuhakikisha ujumbe wetu unaifikia hadhira kubwa si tu ya wana-Iringa bali watanzania wote na dunia kwa ujumla.

Aidha, Baraza la vijana la Chadema mkoa wa Iringa chini ya uongozi wa BAVICHA mkoa iringa na viongozi wote wa baraza kwa ngazi zote za wilaya, majimbo, kata, matawi na misingi tumekubaliana na kuunga mkono kwa asilimia mia moja tamko la baraza la vijana Taifa lililotolewa na makamu mwkt ndugu Patrick Sosopi la Tarehe 02/07/2016 la kukutana Dodoma Tarehe 23/07/2016 ili kulisaidia jeshi la polisi kuwataka wenzetu CCM kutii sheria bila shuruti.
Na kwa mantiki hiyo tunatangaza rasmi kuanzia leo tarehe 06-15/07/2016 zoezi la kuandikisha vijana kwa ngazi zote za uongozi litafanyika mkoa wa Iringa na kwakuwa vijana wengi wamekuwa wakitupigia simu kuonyesha utayari wao basi sasa tunawaalika rasmi kujiandikisha.

Ndugu, Wanahabari mtakumbuka mwkt wa kamati ya siasa ya CCM Iringa mjini ndugu Kiponza aliwaita na kuzungumza nanyi, pamoja na mambo mengine alieleza kile alichoita kuwa ndoto za bavicha kuzuia mkutano wa CCM haziwezekani.sisi tunawaambia wenzetu waache kuweweseka na wasubiri tarehe 23 ili wajue jinsi nguvu ya umma inavyoweza kusimamia amri ya jeshi la police pamoja rais wao ya kuzuia shughuli za kisiasa mpaka 2020 . Pia watambue kuwa kupingana na bavicha ni sawa na kupingana na agizo la mh. Rais tena aliyetokana na chama Chao, jambo ambalo si heshima kwa kiongozi wetu wa nchi. Pia niwakumbushe ccm sisi bavicha mkoa wa Iringa hatuendi Dodoma kufanya vurugu na uchochezi kama wanavyosema wao bali tunaenda kuwasaidia police kuzuia mkusanyiko harama wa ccm



Ndugu Wanahabari, Naomba ieleweke kuwa ninyi wenyewe ni mashahidi wa Tamko lilitolewa na mkuu wetu wa nchi ambalo lilikwenda sambamba na tamko la jeshi la polisi kuvitaka vyama vyote vya siasa na wanasiasa wasijihusishe na shughuli za kisiasa mpaka mwaka 2020 ili kuwapa fursa viongozi waliochaguliwa kutekeleza ilani na ahadi zao kwa wananchi. Sasa sisi tunajiuliza kwanini CCM wanataka kukaidi agizo hili wakati vyama vingine vimekubali na kutii? Havana, ni lazima twende Dodoma tukawaambie CCM wajifunze kutii maagizo ya vyombo vya dola na viongozi wa nchi.
KWANINI TUNAKWENDA DODOMA?

Ndugu Wanahabari tunakwenda Dodoma kwakuwa,
01. Mpaka sasa si rais wala jeshi la polisi aliyetengua kauai au tamko la kuzuia shughuli za kisiasa kwa maana ya vikao vya ndani, makongamano, mkutano ya hadhara au maandamano n.k

02. Haki ya kufanya shughuli za kisiasa haiwezi kuwa ya chama kimoja kwenye nchi yenye mfumo wa vyama vingi tena unaotambulika kikatiba kama Tanzania.

03.kwa mujibu wa katiba yetu ni wajibu wa kila raia kuhakikisha anatii sheria za nchi, Hivyo sisi kama raia wema na tunaowapenda wenzetu hatutaki wapigwe na kuumizwa na virungu vya polisi, tunakwenda kuwasaidia na kuwakumbusha umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ( Coercion without appliances)

04. Mkutano mkuu wa CCM huwakutanisha watu wengi sana na Hivyo jeshi la polisi ambao kwa nchi nzima hawazidi 50,000 pekee yao hawataweza kuwazuia. Tumejitolea hasa kwa kuzingatia ile dhana ya ulinzi shirikishi ili wasipate kazi kubwa sana ya kufanya siku hiyo ya tarehe 23.

05.Tunakwenda Dodoma kusaidia utekelezaji wa kipaumbele muhimu sana kwetu kama Chadema na ambacho kimekuwa hakitekelezwi kikamilifu na kuleta matatizo mengi ambacho ni haki na usawa mbele ya sheria ( Law and order before the law).

Ndugu wanahabari tangu kutolewa kwa tamko la viongozi wetu wa baraza ngazi ya Taifa kumekuwepo na upotoshaji mkubwa eti bavicha wanakwenda Dodoma kufanya fujo. Fujo! Kwanini tufanye Fujo? Tunasisitiza tunakwenda Dodoma kama raia wema na lengo kuu ni kulisaidia jeshi la polisi ili wasitumie nguvu kubwa kuwazuia CCM.Hivyo basi tunatoa wito kwa IGP Mangu na RPC wa mkoa wa Dodoma kutupokea na kutupongeza kwa uzalendo wetu.

Mwisho ndugu wanahabari, nimalizie kwa kumnukuu aliyekuwa rais wa Kwanza mweusi na baba wa Taifa la Afrika kusini Nelson Mandela aliwahi kusema " mahali popote hakuna njia rahisi ya ukombozi na wengi wetu itabidi tupitie, tena na tena kwenye bonde la uvuli wa Martin kabla ya kufikia kilele cha mafanikio". Sisi vijana wa bavicha mkoa wa Iringa tuko tayari kwa gharama kwenda Dodoma ili kusaidia kulinda sharia na katiba yetu isifinyangle finyangwe na chama cha mapinduzi kwa kuamua kwa makusudi kukiuka na kupuuza agizo la rais wetu na Jeshi la polisi.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Imesomwa kwenu
Na, Jackson mnyawami
Katibu Bavicha Mkoa Iringa
Simu: 0762725088
0716884988
 

Attachments

  • IMG-20160706-WA0060.jpg
    IMG-20160706-WA0060.jpg
    60.3 KB · Views: 48
Tuko pamoja kwenda kulisaidia jeshi la police au watengue hiyo kauli yao.

swissme
 
Taarifa ya hovyo Kati ya taarifa zilizowahi kutolewa na wanaojiita viongozi wa Chadema. Hivi Polisi nao wakitoa taarifa kuwa wataweza kuulinda ama kudhibiti kikao hicho (si mkutano) na hivyo hawahitaji msaada wenu mtajificha wapi? Mnajua mbinu za kupambana na waandamanaji? Hii Bavicha ya safari hii mbona hovyo kiasi hiki? Jeshi la Polisi hebu jiandaeni kuwatia adabu wadudu hawa wanaotaka kuuza sura BBC bila kujua dunia haina mpango kuwatazama.
 
Taarifa ya hovyo Kati ya taarifa zilizowahi kutolewa na wanaojiita viongozi wa Chadema. Hivi Polisi nao wakitoa taarifa kuwa wataweza kuulinda ama kudhibiti kikao hicho (si mkutano) na hivyo hawahitaji msaada wenu mtajificha wapi? Mnajua mbinu za kupambana na waandamanaji? Hii Bavicha ya safari hii mbona hovyo kiasi hiki? Jeshi la Polisi hebu jiandaeni kuwatia adabu wadudu hawa wanaotaka kuuza sura BBC bila kujua dunia haina mpango kuwatazama.
BADO HUJAPONA SI KOSA LAKO
 
LAZIMA NIENDE DODOMA KUISAIDIA POLISI HUU NI UZALENDO ULIOTUKUKA
Chama hiki toka Dk. Slaa, Kitila, Zitto, Kafulila, waondoke na Wangwe "auawe" na kinunuliwe na Mchunga ng'ombe kimekuwa kama danguro. Yani kweli kwa ajenda yenu ni Mkutano Mkuu wa CCM ambao lazima ufanyike? Sasa tarehe 24 baada ya JPM kukabidhiwa Kiti mtakuwa na ajenda gani? Mbona mnapelekwa kama ng'ombe mnadani? Ndo mana sitajiunga na chama cha siasa. Ujinga plus.
 
Mungu awabariki sana kwa Moyo wenu wa kulisaidia jeshi la Polisi katika kutekeleza Majukumu yake ya ulinzi wa Sheria za Nchi
 
Ccm fateni sheria bahnaaaa
Sheria ni msumemo
Mnaonekana kama majambazi so lazma tupambane mfatw sheria
 
Hilo ni funzo kwa watawala kwamba unapotoa maamzi fulan hakikisha yako fair kwa upande wako na upande uliokusudia hayo maamzi lakini kwa sababu nchi yetu ni ya uongozi wa hapa mbele kwa mbele ukakasi utakuwa mkubwa sana ktk ktengua kauli ya kusitisha shughuli za kisiasa nchini ivo kutumia mabavu ili kulinda kauli yake kwa kuogopa kuonekana kuwa imekuwa ikitoa matamko bila kuyapima athari zake ktk siasa na maendeleo ya nchi kwa ujumla
 
Back
Top Bottom