BAVICHA kufanya ziara mkoa wa Kagera kwa siku saba

BAVICHA kufanya ziara mkoa wa Kagera kwa siku saba

leonce marto

Member
Joined
Aug 3, 2014
Posts
10
Reaction score
5
Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) linaanza ziara mkoani Kagera kwa siku saba mfululizo kuanzia tarehe 7 February na kuhitimisha tarehe 15 February mwaka huu. Ziara hiyo ya Viongozi wa BAVICHA itakayojumuisha viongozi 15 wakiongozwa na Mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA Patrobasi Katambi inatokana na mwaliko wa BAVICHA kutoka mkoani humo.

Ziara hiyo itafanyika kama ifuatavyo :-

Tarehe 07/02/2015 : Bavicha watakuwa Biharamulo
08/02/2015 : " Ngara
09 /02/2015 : " Karagwe
10/02 /2015 : " Kyerwa
11/02/2015 : " Misenyi
12/02/2015 : " Bukoba Vijijini
13/02/2015 : " Muleba Kaskazini
14/02/2015 : " Muleba Kusini
15/02/2015 : " Bukoba Mjini (majumuisho ya ziara)

Pamoja na mambo mengine Viongozi hao watafanya shughuli za ujenzi wa Chama ikiwa ni kukagua Uhai wa Baraza , watatoa elimu ya kutoshiriki kura ya Maoni kwa katiba pendekezwa kama ilivyoamuliwa na UKAWA , watatoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu l wapiga kura na maswala ya jumla yanayoligusa Taifa kama Rushwa , Ufisadi , Afya , Elimu , Maji n.k ......kwa mawasiliano zaidi hii hapa no. ya mkt wa BAVICHA Mkoa wa Kagera 0758035332/07173110538
 
Kamanda Patrobas, atapokelewa kama mfalme huko!
 
Kwa nini mara nyingi ziara ni kagera tu? Lini mikoa ya kusini kama ruvuma, njombe na hata iringa? Wapinzani wakishindwa kuito ccm madarakani mwaka huu, basi tena!
 
Kwa nini mara nyingi ziara ni kagera tu? Lini mikoa ya kusini kama ruvuma, njombe na hata iringa? Wapinzani wakishindwa kuito ccm madarakani mwaka huu, basi tena!

Nyanda za juu kusini yupo kamanda Sosopi anapiga kazi kama kifaru!
 
Nafurahi kusikia Patrobas Katambi atakuwa kwenye msafara maana huyu mwenyekiti tangu achaguliwe septemba 2014 amekuwa mkimya sana.
 
Dah huyo katambi alipiga mkutano mmojo shinyanga wakati huo nimeenda kikazi mwanzoni mwa mwezi january, Aiseeee dogo ni balaaa umati ambao hata mbunge wa shinyanga mjini masele hajawhi kufikia! wakati anapanda jukwaani nilimdharau kwa sababu ya umbo lake,maana nilikuwa simjui namjua heche tu! dah alinishawishi hata nikachangia 20000 kulipa ofisi yao pale shinyanga.
 
Aiseee huyo dogo ni balaaa, alinipigia nondo shinyanga ni hatari! Maana mm nilikuwa cmjui duh chadema hamna ubongo lala aisee, sasa sijui wengine inakuaje.
 
Kwa nini mara nyingi ziara ni kagera tu? Lini mikoa ya kusini kama ruvuma, njombe na hata iringa? Wapinzani wakishindwa kuito ccm madarakani mwaka huu, basi tena!
Hujasoma kuhusu Kamanda Ole Sosopi na ziara yake Mbeya na Iringa wiki iliyopita tu?
 
Dah huyo katambi alipiga mkutano mmojo shinyanga wakati huo nimeenda kikazi mwanzoni mwa mwezi january, Aiseeee dogo ni balaaa umati ambao hata mbunge wa shinyanga mjini masele hajawhi kufikia! wakati anapanda jukwaani nilimdharau kwa sababu ya umbo lake,maana nilikuwa simjui namjua heche tu! dah alinishawishi hata nikachangia 20000 kulipa ofisi yao pale shinyanga.

kijana yuko vizuri lazima achukue mikoba ya wenje, tayari fedha za kumchukulia form zimeshachangwa.
 
Back
Top Bottom