BAVICHA haturudi nyuma- Sosopi

BAVICHA haturudi nyuma- Sosopi

Washinde mara ngapi wakati mmekimbia mechi, njooni uwanjani kichafuke!
kwanini msije peke yenu mnawatanguliza poliCCM? kama kweli nyie ni wanaume mgekuja peke yenu mpasuliwe hayo mavichwa nazi yenu.....mamamae!
 
kwanini msije peke yenu mnawatanguliza poliCCM? kama kweli nyie ni wanaume mgekuja peke yenu mpasuliwe hayo mavichwa nazi yenu.....mamamae!

Njooni uwanjani nyie mmeitisha mechi mnaogopa nini sasa, police mbona wapo mechi zote. Nyie mmetaka mechi wenyewe na katika uwanja wetu. Police itakuwa wanaenda kumlinda amir wao, nyie njooni tu msiogope na zawadi tutawapa wengine mzishuhudie harusi zenu na mjipigie vigelegele.
 
Demokrasi ni moja tu hakuna aina tofauti za demokrasi, acha kupotosha maana ya demokrasi. Kwenye nchi yoyote ama kuna demokrasi au hakuna.
Kama hielewi chochote c ukae kimya.
una hakika kwamba kuna aina moja tu ya democracy?
chura weee
 
Sosopi NDUGU tangu bora jishughulishe na kuuza nyanya! Utaumia na wenzako watakucheka na wala hawakusaidii Kabisa. Uliza Ulimboka yuko wapi!
Wewe ndio wale wanaume mende akiingia ndani unakimbilia kitandani ukipiga yowee!Maakonda kawafukuza hamtaki kuondoka
 
Wewe ndio wale wanaume mende akiingia ndani unakimbilia kitandani ukipiga yowee!Maakonda kawafukuza hamtaki kuondoka
KAMA SOSOPI ANAJIFANYA KIDUME AKANYAGE DODOMA NA WENZAKE KAMA HAWARUDI WAMEVUNJWA VIUNO VYAO!!
 
PATRICK Ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) amesema, kamwe vijana wa chama hicho hawatarudi nyuma katika kupigania demokrasia inayominywa na kukandamizwa hapa nchini.

Hivi karibuni Sosopi alikamatwa na Jeshi la Polisi na kusafirishwa kutoka mkoani Iringa mpaka jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi katika hafla ya mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chadema.

Akizungumzia sakata hilo pamoja na hali ya kisiasa hapa nchini, makamu huyo wa Bavicha taifa amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kumsumbua kwa kumwita mara kwa mara katika Makao Makuu yake pasipo kumfikisha mahakamani.

“Tangu nikamatwe na kuachiwa, natakiwa kuripoti Makao Makuu ya Oolisi. Nilifanya hivyo 6 Julai na 18 Julai mwaka huu na pia wanataka niende tena tarehe 1 Agosti jambo ambalo ni usumbufu usio na maana, kama kuna kosa kwanini hawanipeleki mahakamani?” amehoji Sosopi.

Sosopi amesema, yeye kama kiongozi wa Bavicha anashindwa kufanya ziara za kikazi na shughuli zake binafsi za kujiingizia kipato kwasababu ya wito wa mara kwa mara wa polisi jijini Dar es Salaam huku akilitaka jeshi hilo lichague kumwacha huru au kumfikisha kortini.

“Nalitaka Jeshi la Polisi liache kufanya kazi kwa maagizo ya wanasiasa na badala yake lizingatie weledi.

“Lisijihusishe na propaganda za kisiasa, lifuate taaluma ili lisiendelee kupoteza heshima na mvuto mbele ya umma,” amesema Sosopi.

Sosopi ameyasema hayo, alipozungumza na Mwanahalisi Online ikiwa ni siku tatu kabla ya Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha Taifa kukutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuibuka na kile kinachotajwa ‘mbinu mpya’ ya kukabiliana na wakandamiza demokrasia.

“Bavicha hatuna uoga, kama wanadhani watatutisha kwa kutufungulia kesi kila mahali basi wajue kuwa kamwe hatutarudi nyuma, tutawaongoza vijana wote nchini kuwakabili wakandamiza demokrasia likiwemo jeshi la polisi na serikali.” Amesisitiza Sosopi.

Viongozi wengine wa juu ya BAVICHA akiwemo Patrobas Katambi mwenyekiti taifa na Julius Mwita ambaye ni Katibu wanakabiliwa na kesi uchochezi mkoani Dodoma wakidaiwa kuvaa fulana zenye maneno ya kichochezi; “Mwalimu Nyerere: demokrasia inanyongwa.”

20 Julai Mwaka huu, kamati ya utendaji ya BAVICHA taifa itafanya kikao ambacho pia mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe ambaye hivi karibuni aliwaomba vijana hao kusitisha safari ya kwenda mkoani Dodoma 23 Julai kuzuia mkutano mkuu wa CCM amealikwa kushiriki.

Hatimaye Bavicha watatoa "MBINU MPYA ZA KUPAMBANA NA UMINYWAJI WA DEMOKRASIA" kuna msemo unasema "CHARITY BEGINS AT HOME" Hebu tuone mfano Kwa Bavicha wakihoji uminywaji wa demokrasia ndani ya Chama chao ikiwemo Haki ya kujua matumizi ya ruzuku, ukomo wa uongozi ndani ya chama, ukiikwaji wa katiba Kwa kutoa madaraka NA teuzi mbalimbali .... Wakianza hapo tutajua wako serious NA kutetea demokrasia VINGINEVYO Ni porojo tu ya Bado tupotupo.....
 
Back
Top Bottom