Basi tufanye upendo utamalaki mioyoni mwetu

Basi tufanye upendo utamalaki mioyoni mwetu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,658
Muda ni kama maji yatiririkayo kwenye mkondo wake.
Binadamu tuna mambo mengi ya kufanya lakini muda kamwe hautusubiri.

Tumeumbwa kuwa na mabadiliko, tumeumbwa tukue, tumeumbwa tuishi na tufe.
Hakuna mtu atakayepinga ukweli huu.

Nilikuwa mtoto na sasa ni kijana. Nimeona watu wakizeeka. Nimeona watu wakifa. Wengine wakiwa vijana kabisa. Nikajiuliza ni nini siri ya maisha?

Hata wale tunaowapenda hawatoweza kuishi miongoni mwetu milele.

Angalia maua yanavyokua, na uzuri wake wote maua waridi hayawezi kuishi milele, moja linakufa na kuacha mengine nafasi ya kuchipua.

Kama tusivyoweza kuyashika maji mkononi na muda ndivyo ulivyo haukamatiki.
Tunaishi tunakufa na kuachia dunia wengine.

Ni ukweli kwamba uzuri hauwezi kubaki ndani ya binadamu. Uzuri wa mwanamke ni jambo la kupita.

Kuna hazina katika moyo wa mwanamke, hazina yenye thamani kubwa zaidi ya dhahabu, almasi na lulu. Lete jembe leta na sululu tuchimbe tutafute hazina hiyo.

Katika moyo wa mwanamke kuna mapenzi na upendo wa hali ya juu.

Nilipokuwa mdogo mama yangu alinilea na kunitunza mpaka nimekua. Ni nani anayeweza kupinga kazi wanayofanya wanawake katika hii dunia?

Ni kama ndege wazuri warukao huku na huko wanatafuta majani na kujenga viota vyao, wanarisha makinda yao mpaka hapo yatakapo pata nguvu ya kupaa.

Kwa mwanamume wanafanya maisha yake yawe mazuri zaidi, Mwanamume hawezi kuishi pasipo mwanamke wameumbwa wawe pamoja.

Kuna furaha ya roho itokanayo na mapenzi, kwa umoja wao watalea na kukuza familia ili kizazi cha binadamu kiendelee kuwepo duniani.

Kuna dunia ya kazi na mapenzi, vitu hivi viwili lazima viwe na uwiano ili maisha yawe mazuri,
Hatuwezi kufanya kazi kila muda lakini hatuwezi pia kuendekeza mapenzi kila wakati.
Kuna wakati wa kulima na kuna wakati wa kusimamisha jembe.

ooh mwangaza wangu niruhusu nikupeleke mbali, mbali na macho ya watu twende tukafurahi, Maisha ni mafupi muda si muda tutakuwa na familia twende tukafurahie wakati bado tuko vijana na wenye nguvu. Twende tukajaze akili zetu na kumbukumbu nzuri.

Tena tutakapozeeka tusubiri kifo. Maisha mazuri kama waridi lipendezavyo lakini hayadumu.
Tunafanya kazi na kufanya kazi tunayaacha yote tuliyoyafanya duniani tunawaachia watu wengine wanafurahia kazi za mikono yetu.

Wanasema kila kitu tunachofanya tufanye kwa mapenzi ili tuendelee.

Wawili hawa wameumbwa kuishi pamoja hakutawahi kutokea vita kati ya wanawake na wanaume.

Wakati utakapofika ardhi itachimbwa na mwili wangu utafukiwa na mchanga na huo ndio utakuwa mwishi wangu.

Mabaya yangu na mazuri yangu yatabaki kwenye akili za watu. Katika vizazi vijavyo huenda yakafutika nani anayejua?

Nitawaacha wote ninaowapenda wakiwemo wale wanaojua siri zangu za ndani . Anayejua mwili wangu na anayejua kitanda changu na moyo wangu.

Uzuri wa waridi haudumu. Ndege, miti na kila chenye uhai kitakufa. Ni nani anayejua siri ya kufa na kuzaliwa kama sio mungu mwenyewe?

Basi tufanye upendo utamalaki mioyoni wetu.


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom