Basi limezidisha abiria, nitoe taarifa wapi?

Mkuu,hii ni issue ya usalama,ndio maana Magari hua yana limit ya idadi ya abiria,
Si ajabu ikitokea ajali,hata wewe utaanza kulaumu,

Mleta mada yupo sahihi kabisa,mlinzi wa kwanza wa Nchi ni Mwananchi.
Wanasubiria ajali itokee waanze kumtukana Rais na kumkumbuka dikteta
 
Basi limezidisha abiria na konda analeta dharau. Natakiwa kutoa taarifa wapi na namba zao ni zipi?
Hawajabandika hata namba za LATRA au traffic za kupiga?
 
Cha kwanza shuka tafuta usafiri mwingine hao waliobaki kama hawana shida acha wakae kimya
Katika hao waliobaki,huenda kuna Ndugu yako jamaa au rafiki yako ila wewe huna habari kama nao wapo safarini kwenye hilo Basi,

Usalama ni kwa wote bila kubagua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…