Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Baraka Classic jijini Dar es Salaam wamepatwa na taharuki baada ya basi hilo kufeli breki na kushika moto.
Basi hilo lililokuwa safarini kutoka Mtwara kuelekea Dodoma, limeshika moto saa 1 asubuhi ya leo Jumatatu Oktoba 19, 2026.
Tukio hilo limetokea jijini Dar es Salaam, Barabara ya Mandela eneo la Tabata Mwananchi na kusababisha taharuki na hofu kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Hali hiyo ilibainika baada ya moshi kuonekana chini ya tairi la mbele kushoto, huku juhudi za kuzima moto huo zikiendelea kufanywa na wahudumu wa basi hilo.
Akieleza chanzo cha moto huo, dereva wa basi hilo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa, ameeleza chanzo cha moto huo ni hitilafu ya breki ambayo umesababisha msuguano iliyosababisha moto kutokea.
Chanzo : Eatv