Basi la Taifa Stars lakamatwa na madalali

Basi la Taifa Stars lakamatwa na madalali

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
Basi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya Mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambalo tunadaiwa hadi litakapolipwa.

Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. TFF imesema hadi sasa imekwishalipa Sh. Milioni 70 katika deni hilo. "Jitihada zinafanyika ili kumaliza deni hilo. Pia tunachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo,"imesema taarifa ya TFF.

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Hili ndilo basi la Stars lililokamatwa kwa deni lililoachwa na utawala wa Tenga TFF[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Basi lililokamatwa ni ambalo TFF ilipewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wadhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars, aina ya Yutong na deni ni wakati ambao shirikisho hilo lipo chini ya Rais, Leodegar Tenga aliyemaliza muda wake mwaka jana. Kwa sasa, Rais wa TFF ni Jamal Malinzi aliyerithi deni hilo. [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mzee imekuwaje tena basi limekamatwa? Tenga ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CECAFA (kshoto) akiwa ni Mkurugenzi wa masoko wa TBL, Kushila Thomas (kulia)
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kila mchezo ukiisha utasikia makato ya mechi ikiwa ni pamoja na gharama za tickets, ilikuwaje gharama ziafikia hapa!?
 
pumbavu kabisa tiketi zinatengenezwa na kampuni ya kenya?
 
Bado nchi na yenyewe inakuja kukwmatwa na deni la taifa sijui ma ccm yanaiba vipi
 
Kachukua uongozi, Kaajiri mchauri maalumu, kahamisha ofisi, kapeleka wachezaji wa zamani seminar Lushoto na Zanzibar. Leo mnataka kumlaumu Tenga? Big institution kuachiwa madeni ni kitu cha kawaida. Ukimuuliza, are justify hayo matumizi, an akimbia eti siri. It's pity, institution Kama TFF, inawekeza Kwenye frame? Uko kwenye prime area, kweli wamekosa ubunifu?. kwa nini hawakukaribisha watu waje na project proposal kwa ajili ya hapo mahala, ili atakayeshinda wamlipe consultants fees. Hapo pangeweza kuingiza pesa ambayo ingegharamia uendeshaji wa offisi yote. The guy is weak and useless.
 
Duuuuuuuuuuuuuh!!!! yaani walikuwa wanazipiga tu bila kuwakumuka watengenezaji wa tiketi?????????
 
Ligi ikianza tu, utasikia kuna makato 70% kwa ajili ya kulikomboa basi..na ligi yenyewe iko mbali watairudisha nyuma sasa hivi!!!!
 
Kachukua uongozi, Kaajiri mchauri maalumu, kahamisha ofisi, kapeleka wachezaji wa zamani seminar Lushoto na Zanzibar. Leo mnataka kumlaumu Tenga? Big institution kuachiwa madeni ni kitu cha kawaida. Ukimuuliza, are justify hayo matumizi, an akimbia eti siri. It's pity, institution Kama TFF, inawekeza Kwenye frame? Uko kwenye prime area, kweli wamekosa ubunifu?. kwa nini hawakukaribisha watu waje na project proposal kwa ajili ya hapo mahala, ili atakayeshinda wamlipe consultants fees. Hapo pangeweza kuingiza pesa ambayo ingegharamia uendeshaji wa offisi yote. The guy is weak and useless.

thanks
 
Ni kweli tatizo limetokea na linatafutiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kupata undani wa deni hili lilioanza 2007.
Kwa wanaozungumzia gharama za maboresho (kama Yombayomba) waelewe kuwa mkataba wa TFF na mdhamini wa national team unapiga marufuku fedha za mdhamini kutumika kwa shughuli nyingine zaidi ya za timu ya Taifa.Hii drama ya basi la TFF ukweli wake utakuja kujulikana tu kuhusu historia ya hilo deni na ukweli wake,its a matter of time,si kwamba hatujui kinachoendelea.
 
Last edited by a moderator:

Mh naomba appointment to meet you!! Kuna mambo naomba nije tuongee...!! Please naomba mda wako japo wa dakika 20 tu!! Nipo dsm
 
Last edited by a moderator:
Rais wa TFF katoa mawasiliano yake myatumie vizuri sio kupiga mizinga au kutukana maana hii inawaogopesha viongozi wengine kutoa namba zao
 
Back
Top Bottom