Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 38,016
Wananchi wakitoka kwenye gari kupitia madirishani.
Aha! kila mmoja akichomoka kujiokoa bila kusahau kipimajoto mkononi...
Basi la RATCO linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Tanga limepata ajali eneo la Kibaha, Pwani leo jioni Aprili 27, 2014.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyefika eneo la tukio alisema gari hilo lilipinduka ubavu baada ya kuacha njia.
Kongowe mkuu, ipi maana mm npo maeneo haya, kabla hujafika ukiwa unatoka bara au ukiwa unaenda?
true nimeongea na mfanyakazi wa ratco kathibitisha kwamba conductor ndiye yuko hali mbaya sana. chanzo ni kwamba gari ndogo lilichomoka tyre ratco ikalikanyaga au likaingia uvunguni na ajali ikatokea. poleni waathirika wa tukio hili.
Almanusura nipande hilo basi pale mkata..... Mungu mkubwa, nikaamua kupanda costaInasemekana mtu mmoja ndio amejeruhiwa. Basi limelalia ubavu wa kushoto.
Basi la kampuni ya RATCO, limetumbukia mtaroni maeneo ya kongowe ya Kibaha muda mfupi uliopita, lilikuwa linatoka Tanga kwenda Dar. Kwa kuwa nilipita hapo nikiwa ndani ya basi jingine, sina taarifa ya majeruhi wala vifo kama vipo...
Ahsante sana kwa taarifa.
Ni jambo la kushukuru kwamba watu wametoka salama!
Basi la kampuni ya RATCO, limetumbukia mtaroni maeneo ya kongowe ya Kibaha muda mfupi uliopita, lilikuwa linatoka Tanga kwenda Dar. Kwa kuwa nilipita hapo nikiwa ndani ya basi jingine, sina taarifa ya majeruhi wala vifo kama vipo.
Picha za ajali