Basi la Kilimanjaro Express

Basi la Kilimanjaro Express

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
6,392
Reaction score
8,294
Wiki iliyopita nilisafiri na basi la Kilimanjaro express kutoka Dar kwenda Moshi. Mkanda wa siti niliyokaa pamoja na jirani yangu ilikuwa mibovu. Mikanda ipo lakini haiwezi kufunga kwa kutumia lock. Ilibidi nifunge kinyeji kama nafunga kamba. Nikahisi labda ni bahati mbaya watarekebisha. Jana nikawa narudi Dar kutoka Moshi kwa Kilimanjaro Express basi no. T 830 AXR. Basi zima siti hazikuwa na mikanda. Cha ajabu ni kwamba askari wa usalama barabarani walikuwa wanalikagua njiani, hakuna hata mmoja aliyehoji upungufu huo. Tena kuna askari mmoja alipanda Chalinze akashuka Kibaha, hakuhoji juu ya viti kukosa mikanda ya usalama. Tafadhali wahusika wote wa jambo hili, kuanzia wamiliki wa hii kampuni na askari wa usalama barabarani, timizeni wajibu wenu ili kurekebisha kasoro hii.
 
Safi mkuu kwa kuliona hili..hata mimi nlishasafiri na basi ya Kampuni ya Dar Express seat nyingi zilikuwa hazina mikanda..na hata ukiwepo huwezi kuutumia maana ni michafu(ina vumbi)..nathani wahusika watafanyia kazi hizi observations..
 
Mkuu Dar express ya miaka gani? Kweli huduma zao zimeshuka flan but kwa mikanda wanajitahidi kupita kampuni yoyote ukanda huu...

Naamini hiyo ilikua ni one-off.
 
Wiki iliyopita nilisafiri kwenda Moshi na basis la Kilimanjaro express kutoka Dar kwenda Moshi. Mkanda wa siti niliyokaa pamoja na jirani yangu ilikuwa mibovu. Mikanda ipo lakini haiwezi kufunga kwa kutumia lock. Ilibidi nifunge kinyeji kama nafunga kamba. Nikahisi labda ni bahati mbaya watarekebisha. Jana nikawa narudi Dar kutoka Moshi kwa Kilimanjaro Express basi no. T 830 AXR. Basi zima siti hazikuwa na mikanda. Cha ajabu ni kwamba askari wa usalama barabarani walikuwa wanalikagua njiani, hakuna hata mmoja aliyehoji upungufu huo. Tena kuna askari mmoja alipanda Chalinze akashuka Kibaha, hakuhoji juu ya viti kukosa mikanda ya usalama. Tafadhali wahusika wote wa jambo hili, kuanzia wamiliki wa hii kampuni na askari wa usalama barabarani, timizeni wajibu wenu ili kurekebisha kasoro hii.

Ndugu Kilimanjaro saivi ni bure bora waliite Urru Express
 
Umenikumbusha enzi za scandinavia nilipanda toka dodoma kuja dar, kufika ubungo kushuka lock ya mkanda ikagoma katakata kufunguka walihangaika na kuhangaika haikuwezekana kubanduka kitini, wakaniomba radhi kuwa wangependa kuvunja kile kibanio lakini sheria za kampuni ni mpaka idhini ya marekebisho itoke ofisini kwao, hivyo ikanibidi kwenda nimebanwa hivyohivyo mpaka Kamata zilikokuwa ofisi zao ndiko ikatolewa idhini ya kuukata na wembe

Nilichojifunza ni kuwa baadhi ya mabasi yanakuwa na mikanda iliyo chini a viwango kiasi cha kuhatarisha usalama wa abiria na hasa inapotokea ajali ya bus kuanguka kugongana au kuwaka moto, ukaguzi ukifanywa usilenge tu uona uwepo wa mikanda bali ulenge kuona kama inafanya kazi barabara
 
Ujifunze kutembea na visu vya mfukoni, ikitokea kama hiyo wala humwambii muhudumu unajihudumia mwenyewe kisha una sepa
 
Juzi kwenye ajali ya simba mtoto wami siti yangu mkanda ulikuwa mbovu hivyo nikafunga kama nafunga na kamba hadi jirani yangu akawa ananishangaa. kwa kweli ilisaidia sana ile ajali ilipotokea. nilijifunza kuwa mkanda ni muhimu sana sana na pia pamoja na kufunga mkanda kama utaona ajali ikitokea ni vizuri pia kujishika vizuri
 
Umenikumbusha enzi za scandinavia nilipanda toka dodoma kuja dar, kufika ubungo kushuka lock ya mkanda ikagoma katakata kufunguka walihangaika na kuhangaika haikuwezekana kubanduka kitini, wakaniomba radhi kuwa wangependa kuvunja kile kibanio lakini sheria za kampuni ni mpaka idhini ya marekebisho itoke ofisini kwao, hivyo ikanibidi kwenda nimebanwa hivyohivyo mpaka Kamata zilikokuwa ofisi zao ndiko ikatolewa idhini ya kuukata na wembe

Nilichojifunza ni kuwa baadhi ya mabasi yanakuwa na mikanda iliyo chini a viwango kiasi cha kuhatarisha usalama wa abiria na hasa inapotokea ajali ya bus kuanguka kugongana au kuwaka moto, ukaguzi ukifanywa usilenge tu uona uwepo wa mikanda bali ulenge kuona kama inafanya kazi barabara

Lingewaka moto tungesema Mungu kakupenda zaidi
 
Kilimanjaro kwisha kazi, kwa safari za Dar-Moshi-Arusha bora kupanda gari lingine tofauti na kampuni hiyo.
 
Na wewe mleta mada ulitumia juhudi gani kumweleza askari pale pale hali ya usalama wa basi? Acha woga. Unakuja kutafuta ujasiri hapa au?
 
LIM Safaris na IBRA Line ndio gari zangu siku hizi...! Hizo Dar Express na K'njaro hola tu saivi..!
 
Umenikumbusha enzi za scandinavia nilipanda toka dodoma kuja dar, kufika ubungo kushuka lock ya mkanda ikagoma katakata kufunguka walihangaika na kuhangaika haikuwezekana kubanduka kitini, wakaniomba radhi kuwa wangependa kuvunja kile kibanio lakini sheria za kampuni ni mpaka idhini ya marekebisho itoke ofisini kwao, hivyo ikanibidi kwenda nimebanwa hivyohivyo mpaka Kamata zilikokuwa ofisi zao ndiko ikatolewa idhini ya kuukata na wembe

Nilichojifunza ni kuwa baadhi ya mabasi yanakuwa na mikanda iliyo chini a viwango kiasi cha kuhatarisha usalama wa abiria na hasa inapotokea ajali ya bus kuanguka kugongana au kuwaka moto, ukaguzi ukifanywa usilenge tu uona uwepo wa mikanda bali ulenge kuona kama inafanya kazi barabara

uwe unatembea na mkasi
 
Umesema ulisafiri toka dar -moshi sasa trafik alipanda chalinze na kushuka kibaha tuamini nini ????????
 
Wiki iliyopita nilisafiri na basi la Kilimanjaro express kutoka Dar kwenda Moshi. Mkanda wa siti niliyokaa pamoja na jirani yangu ilikuwa mibovu. Mikanda ipo lakini haiwezi kufunga kwa kutumia lock. Ilibidi nifunge kinyeji kama nafunga kamba. Nikahisi labda ni bahati mbaya watarekebisha. Jana nikawa narudi Dar kutoka Moshi kwa Kilimanjaro Express basi no. T 830 AXR. Basi zima siti hazikuwa na mikanda. Cha ajabu ni kwamba askari wa usalama barabarani walikuwa wanalikagua njiani, hakuna hata mmoja aliyehoji upungufu huo. Tena kuna askari mmoja alipanda Chalinze akashuka Kibaha, hakuhoji juu ya viti kukosa mikanda ya usalama. Tafadhali wahusika wote wa jambo hili, kuanzia wamiliki wa hii kampuni na askari wa usalama barabarani, timizeni wajibu wenu ili kurekebisha kasoro hii.

tafakari alafu chukua hatua
 
Back
Top Bottom