Basi la Kampuni ya Princess Muro lapata ajali Morogoro!

Basi la Kampuni ya Princess Muro lapata ajali Morogoro!

Jana nilipanda gari (costa) kutokea mbeya mjini kwenda tunduma,nilikaa jirani na jamaa wawili ambao hawakulipa nauli kwa sababu walikuwa members.

Tukikaribia kufika mwisho wa safari,abiria wakiwa wamepungua jamaa wakawa huru zaidi kufanya mazungumzo yao.

Mmoja wao,katika namna ya kujisifia sana akamuelezea mwenzake mkakati wake wa kuleta gari bomba sana la abiria kwenye route hiyo,kwamba anaagiza bord la gari pamoja na chasis kutoka china,aina ya magari ya kichina ambayo yapo dar route za kimara posta,gongo la mboto posta n.k made from china.Kisha anaweka injini ya scania,anasema "litakuwa linadhauliwa machoni kwamba ni la kichina halikimbii lakini watakiona cha moto,sababu litakuwa linakatiza fyuuuu.

Nilisikitika sana,nikamuomba Mungu anisaidie busara,katika harakati zangu za kibiashara nisije nikajisahau na kujikuta nafukuzana na faida bila kujali hatari nitakayokuwa nawasababishia wateja wangu.

Serikali au specifically agent husika wa usimamizi wa vyombo vya usafiri pamoja na sheria husika,waangalie uwezekano wa kutoa leseni kwa magari yatakayopaswa ama kuingia nchini au kufanya biashara ya ubebaji abiria,yawe kutoka kwa authorized producers/makers of motor vehicles,sababu naamini kabisa magari na vyombo vingine vya usafiri vinavyotengenezwa kwa kuunga unga tena na watu wasiokuwa na uelewa wa kisayansi wa nguvu mbalimbali zinahusika katika vyombo husika ni chanzo kikubwa sana cha ajari,sidhani kama hawa waungajiungaji wanatambua uwepo wa nguvu za upepo,uzito wa gari,speed,friction,matairi n.k na namna nguvu hizo zinavyointeract wakati gari likiwa barabarani.

Yaani unakuta bord la kichina,chasis ni mchanganyiko wa mti wa mninga na vyuma mbalimbali,injini ya scania,nini sijui vya landrover,ni mchanganyiko hatarishi sana,ukizingatia asikari ambao ndio wadau pekee ambao huwa nawaona wakizugazuga mabarabarani kusimamia usalama ni watu wenye uelewa mdogo sana hata wa usalama wao wenyewe.

Au na usimamizi wa hili ubinafsishwe?
 
hatari sana. Pole wahanga
Sio wahanga mkuu, ni waathirika!
Mhanga ni mtu anayejitosa katika eneo la hatari kama ndani ya nyumba inayoungua au majini ili kuokoa mtu, watu au vitu. Ndio maana utasikia fulani amejitoa mhanga kujitosa ndani ya nyumba inayoungua ili kumtoa mtoto au mtu. Anayekumbwa na majanga kama ajali, moto, mafuriko nk huyo anaitwa muathirika
 
Mkuu, unauhakika kuwa neno wahanga halipaswi kutumika katika ajari hiyo?
 
Mkuu, unauhakika kuwa neno wahanga halipaswi kutumika katika ajari hiyo?
Ndiyo mkuu wangu. Wote waliokuwa ndani ya hilo basi ni waathirika (victims)kwa maana ya kuumia, safari yao kukatishwa, kupoteza mizigo nk Ingekuwa baada ya ajali lile basi lilikaa mkao wa kubiringika na ndani kukiwa na mtu au watu walionaswa(wathirika) halafu akatokea mtu na kujitolea kuingia mule kuwaokoa huyo tunasema amejitoa mhanga na kwahiyo ni mhanga - ame take risk amehatarisha uhaii wake kwaajili ya kuokoa. Hata wanaokwenda vitani huwa ni watu walijitolea mhanga kwa maana wanakwenda kufanya kazi ya hatari kwa maisha yao ili kuokoa na kulinda raia na nchi. Ni hayo tu mkuu. I stand to be corrected
 
Ndio maana amejitahidi kwa kila alipoweza kufikisha taarifa alizozipata yeye, kama kuna mwingine mwenye taaarifa zaidi atatujuza, sidhani kama kuna tatizo lolote kwa alivyofanya mleta taarifa

True, imagine.mpaka sasa hakuna aliyeleta updates, kwa hiyo jamaa alitaka tusipate taarifa hii mpaka sasa.
 
Ndiyo mkuu wangu. Wote waliokuwa ndani ya hilo basi ni waathirika (victims)kwa maana ya kuumia, safari yao kukatishwa, kupoteza mizigo nk Ingekuwa baada ya ajali lile basi lilikaa mkao wa kubiringika na ndani kukiwa na mtu au watu walionaswa(wathirika) halafu akatokea mtu na kujitolea kuingia mule kuwaokoa huyo tunasema amejitoa mhanga na kwahiyo ni mhanga - ame take risk amehatarisha uhaii wake kwaajili ya kuokoa. Hata wanaokwenda vitani huwa ni watu walijitolea mhanga kwa maana wanakwenda kufanya kazi ya hatari kwa maisha yao ili kuokoa na kulinda raia na nchi. Ni hayo tu mkuu. I stand to be corrected
nendeni jukwaa la lugha...
 
Haya mabasi sinto kaa nipande tenaa ....Mwaka jana Chrismass nilitoka Dar saa 12 asubuhi nikafika Arusha saa 4 usiku...
mi nilitoka njombe saa 12 asubuhi nikafika saa 5 usiku,sina hamu hata bure sipandi
 
mi nilitoka njombe saa 12 asubuhi nikafika saa 5 usiku,sina hamu hata bure sipandi
Ndiyo matatizo ya wasafiri. Yakienda kasi ili mfike haraka na ikatokea mmefika salama mnawasifu madereva lakini ajali ikitokea mnamgeuka dereva kuwa alikuwa mwendo kasi ndio maana ajali imetokea. Yakienda pole pole ili mfike salama napo mnalalamika kuwa hayana mwendo mnachelewa kufika au mnasema mabovu. Hakuna jema chini ya jua!
 
sure mkuu!! mitanganyika ndivyo tulivyo,kila kitu ni kulalamika tuuuu!! shenx zetu!!!!
 
Mkuu mijadala yote humu inafanyika kwa njia ya lugha. Kusahihishana pamoja na kuelekezana ni sehemu ya mijadala na lazima hayo yafanyike contextually.
kuna vi2 vingine vidogo sana kutambua na kuelewa but vingine naona havina ulazima kiivo kama wewe ni GT.. na ndo dfntion ya GT.
 
Back
Top Bottom