Basi la Kampuni ya Luwinzo, T853 AUA lapata ajali Morogoro

Basi la Kampuni ya Luwinzo, T853 AUA lapata ajali Morogoro

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
4,131
Reaction score
6,125
Gari la Luwinzo lenye namba za usajili T853 AUA linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es Salaam limepata ajali Morogoro.

Taarifa hizi nimepewa na ndugu yangu ambaye ni mmoja kati ya abiria majeruhi.

Wenye taarifa kamili watujulishe hapa jamvini.

================ Updates ================

Limeigonga Coaster. Kuna watu wamefariki kwenye coaster Ila hilo gari nyingine ni majeruhi tu.

Kwa mujibu wa taarifa ya habari radio one ni watu 10 waliopoteza maisha.




Picha kutoka eneo la ajali, Picha nyingine sitoziweka ili kuwasitiri marehemu

Watu saba wamefariki dunia 26 wamejeruhiwa baada ya basi la Msanga Express likitokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la kampuni ya Luwinzo lililokuwa likitoa Njombe kwenda jijini Dar es Saalam katika eneo la hifadhi ya Mikumi barabara ya Morogoro Iringa.

Wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi la Msanga Express alikuwa akijaribu kulipita lori bila tahadhari na kisha kutoa gari barabarani wakati akikwepa ajali ya uso kwa uso ambapo aligongwa upande wa kulia.

Inaelezwa kuwa watu sita walifariki dunia papo hapo na mwingine amefariki wakati akiwa njiani kupelekwa hospitalini kupata matibabu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hadi sasa mwili mmoja tu ndiyo uliotambulika na miili mingine sita bado haijatambulika na imehifadhiwa katika hospitali ya St Kizito Mikumi.

Amesema madereva wa mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu wakiwa chini ya ulinzi ambapo kufuatia kuongezeka kwa mtukio ya ajali za mfululizo katika hifadhi ya Mikumi jeshi la polisi kwa kushirikiana na hifadhi ya Mikumi waanza kufanya oparesheni maalum kukagua madereva wanoendesha kwendo kasi katika hifadhi.

Katika hospitali ya St. Kizito walikolazwa majeruhi muuguzi wa zamu Josefu Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kueleza amesema hali za majeruhi wanaendelea na matibabu huku majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa wakieleza jinsi tukio lilivyotokea.

View attachment 235943View attachment 235944View attachment 235945View attachment 235946View attachment 235947
 

Attachments

  • Ajali Moro.png
    Ajali Moro.png
    131.9 KB · Views: 2,321
  • Ajali Moro1.png
    Ajali Moro1.png
    92 KB · Views: 2,102
Mkuu lilikuwa linatoka Njombe kwenda Dar au vice versa?
 
Daaah, lilitoka jana njombe linakimbia linafahamika kama "Karibu Kiumeni"
 
naskia imeua 4 na hiyo nyingine imeua 6.. zimegongana uso kwa uso kitonga
 
Gari la Luwinzo lenye namba za usajili T853 AUA linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es Salaam limepata ajali Morogoro.

Taarifa hizi nimepewa na ndugu yangu ambaye ni mmoja kati ya abiria majeruhi.

Wenye taarifa kamili watujulishe hapa jamvini.

================ Updates ================

Limeigonga Coaster. Kuna watu wamefariki kwenye coaster Ila hilo gari nyingine ni majeruhi tu.
Tutaendelea kuwajuza hivi Punde

Mwanahabari huru
 

Attachments

  • IMG-20150319-WA0027.jpg
    IMG-20150319-WA0027.jpg
    177.8 KB · Views: 1,612
  • IMG-20150319-WA0028.jpg
    IMG-20150319-WA0028.jpg
    134.1 KB · Views: 1,428
  • IMG-20150319-WA0026.jpg
    IMG-20150319-WA0026.jpg
    162.3 KB · Views: 1,360
Naona hawa madereva wa mabasi wenye vichwa vya kuku au mbuzi watatumaliza. Pamoja na ajali zote hizi na wao wenyewe kuzishuhudia wanapopita lakini hawajifunzi chochote. Afadhali wao ndio wawe wanakufa.
 
Back
Top Bottom