Basi la Al Saedy lapata ajali

Swahili AI

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
9,993
88,197
Basi la Al Saedy linalofanya safari zake za Dar-Mpwapwa limepata ajali baada ya kutumbukia kwenye daraja la kijiji cha Ngh'ambi wilayani Mpwapwa wakati linatokea Dar Es Salaam kuja mpwapwa.
Bado haijafahamika majeruhi wangapi na waliofariki wangapi.
ade3dfea34b3cb469506184792d4bc21.jpg
46be45f7d09a8e5a5a4546239c55a114.jpg
4b63008b22eba864fe76068da96d8cb3.jpg
 
Majeruhi 28 mpaka sasa. Wapo hospitali ya kongwa na mpwapwa. Wawili wapo mahututi hospitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma
 
Chanzo dereva alikua anaongea na simu ndipo aliposhtuka tairi moja ya mbele imeingia darajani. Akaruka na kukimbia.
Hakuna aliyefariki
 
Chanzo dereva alikua anaongea na simu ndipo aliposhtuka tairi moja ya mbele imeingia darajani. Akaruka na kukimbia.
Hakuna aliyefariki
Ahsante kwa ufafanuz ingawa nimekuelewa,lakin hapo tairi moja ya mbele imeingia darajani au imetoka darajan na kutumbukia mtoni?
 
Chanzo dereva alikua anaongea na simu ndipo aliposhtuka tairi moja ya mbele imeingia darajani. Akaruka na kukimbia.
Hakuna aliyefariki
inaskitisha dereva anaweka roho za watu kwenye hatari ili tu aongee na simu.
 
Poleni sana majeruhi.bahati yake dereva ametoroka vinginevyo wangemgombania kila mtu aondoke na kipande cha nyama.
 
Aisee hili basi nilikua nalitumia kwenda nalo dodoma, mbona mwendo wake ni kama wa kinyonga sana, what happened?
 
Back
Top Bottom