GE2025 Bashungwa: Uongozi wa Rais Samia, Karagwe imekuwa kama Switzerland kutokana na ujenzi wa miradi mikubwa

GE2025 Bashungwa: Uongozi wa Rais Samia, Karagwe imekuwa kama Switzerland kutokana na ujenzi wa miradi mikubwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Bashungwa acha uongo wewe! Hiyo Switzerland unajua vizuri kweli! Uchawa unakusumbua sana

Vumbi limejaa pale, wakazi wengine hata maji hakuna
======================

Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Karagwe Mkoani Kagera na Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Innocent Bashungwa amesema ndani ya miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wilaya ya Karagwe imekuwa kama nchi ya Switzerland kutokana na ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo pamoja na miundombinu ya barabara za Viwango vya lami pamoja na taa zake.

Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu za Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya Bashungwa, Kayanga, Karagwe leo Jumatano Oktoba 15, 2025, Bashungwa ameyataja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya 5 za Msingi pamoja na madarasa mapya 201, vyote vikigharimu Bilioni 5.5.

 
Karagwe yenyewe sasa na miradi mikubwa ya Mama Samia

SWIPE kuona KARAGWE ambayo inafanana na SWITZERLAND….SLIDE ya kwanza na pili; OMORUSHAKA na KAYA.jpg
 
Ni nchi ndogo yazungukwa na mataifa makubwa na haina bandari yaani "landlocked"

Wana benki zinohifadhi fedha za kutosha.

Watengeneza saa za mkononi

Wana utalii kwenye milima ya Alps.

Ni nchi maarufu kwa kutengeneza chocolate na jibini (cheese) za maana.

Ina viwanda vingi vya madawa na vya kutengeneza madawa ya kibaolojia yaani "biotechnology".
 
Back
Top Bottom