DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
"Uchaguzi huu wa Oktoba 29, 2025 ni uchaguzi wa kufanya maamuzi kati ya Maisha halisi na anasa, wapo wanaojadili anasa wakitaka ndio ziwe ajenda za uchaguzi kwamba haki na uhuru wetu umeondolewa kwasababu hakuna Twitter, sisi huku Vijijini tunaelewa maana ya hatua unazozichukua.
... Niwaombe ndugu zangu mbegu zimeshaanza kusambazwa, mbolea zimeanza kufika, mvua zimeanza kuonesha dalili, Mama ametupa fedha matrekta yapo na ametoa ahadi ya kuongeza mengine yafikie 10,000 kwaajili ya wakulima wa nchi hii katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Anatoa ruzuku kwenye mbolea, kwenye mbegu na kwenye ugani na amesaini kuanzishwa kwa wakala wa ugani wa Taifa, anatoa ruzuku ya trekta na hii ndio tafsiri ya kukuza utu wa mtu kwani Utu wa mtu unaanzia mfukoni na tumboni.
"Utu wa Mtanzania haulindwi kwa Twitter, Instagram wala Social Media. Tarehe 29 tujitokeze tukapiganie uhuru wetu wa pili ambao ni uhuru wa kiuchumi wa kumuondoa Mtanzania kwenye umaskini. Tuungane sote." Hussein Bashe, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini na Waziri wa Kilimo, akimnadi Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Oktoba 11, 2025, Shinya ga Mjini Mkoani Shinyanga.