Akizungumza mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amegoma kuzungumzia yeye kushikiliwa na polisi hapo jana na kusema suala hilo kamuachia katibu mkuu wa chama hicho, Abdurahman Kinana. Alipoulizwa kama ana hofu ya kutimuliwa chamani, amedai hana hofu hiyo kwani hayo mambo hufanyika kwa utaratibu.
Pia amedai mabadiliko yanayofanyaka ndani ya chama ni kawaida na hii inaweza kuwa mara ya nne kubwa katika historia ya chama na kumekuwa na mabadiliko ya kila wakati.