Bashe: Kuna kikundi ndani ya TISS kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

lebara

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
646
839
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea.

Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

"Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana".

Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'

Wasalaam
 
Attachments

  • Bashe.png
    Bashe.png
    63.2 KB · Views: 490
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
kuna MAJITU MENGINE HUMU wao chuki zao ni mbele tu HATA KWENYE UWONGO YANAKUBALI TU.....utasikia mtu anasema ETI MAGUFULI nchi imemshinda....SASA hao ambao nchi haikuwashinda walitufikisha wapi???mbna still mlikuwa mna piga kelele???
Afadhali ya huyu amabaye mnasema nchi imemshinda lakini pesa za walipa kodi zipo salama si kwenye mikono ya wachache.......
ACHA TU atunyooshe HII MIAKA 10 AKILI ZIKAE vizuri kichwani......THEN 2025 tutaamua je tunataka RAIS aina ya KIKWETE au MAGUFULI.....tutajaji hili kupitia MAHALI alipotufikisha JPM na mahali alipotuacha JK......
 
Sasa hao mawaziri wanawatumikia Watanzania ama wanayatumikia matumbo yao? Kama wana akili wajiuzulu, vinginevyo wanazitia aibu familia na koo zao kuendelea kufanya kazi chini ya boss ambaye hawezi kusikiliza na kufanyia kazi mawazo yao. Kantasundwa............
 
Huyu BASHE anajistukia TU...kwanini asijilipue KABSA KWA KUTAJA WAHUSIKA MAANA anajijua kabsa HAYUPO CCM tokea kipindi kile LOWASSA amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta ANAZUNGUMZA mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua RAIS....chunguzeni KWANINI wale TEAM LOWASSA wote kama BASHE,MSUKUMA,MALIMA ndio wapiga kelele kila siku??????kwanini wao tu???
Hivi usalama gani wa TAIFA ukawa na kikundi cha UTEKAJI,,na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa???
Huo mnaongea hivihivi na baadae mambo yanatokea.Ben Saanane yuko wapi?
 
Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'

Wasalaam

Liberia mpya inakaribia kuzaliwa rasmi ndani ya ardhi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom