Bashe, Kigwangalah wapigwa panga Nzega | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bashe, Kigwangalah wapigwa panga Nzega

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Sep 23, 2012.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  [FONT=&amp]SEKRETARIETI YADAIWA KUPENDEKEZA WAKATWE,VURUGU ZA NZEGA ZAWAPONZA[/FONT]

  [FONT=&amp]MAKALI ya panga la Sekretarieti ya CCM, yameanza kuonekana baada ya majina ya wagombea wa nafasi ya Halmashuari Kuu (Nec) ya chama hicho kupitia Wilaya ya Nzega, Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Hamis Kigwangalah na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Hussein Bashe kukatwa.

  Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Dodoma zinaeleza kuwa Sekretarieti ya CCM iliyoketi hivi karibuni, kupitia majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ikiwa chini ya Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama iliamua kuyaondoa majina ya Kigwangalah na Bashe kwa madai kuwa wamekiabisha chama hicho.
  [/FONT][FONT=&amp][FONT=&amp]
  Bashe na Kigwangalah waliingia katika mvutano wakati wakichukua fomu ambapo kulitokea malumbano baina yao wakiwa katika Ofisi za CCM, mjini Nzega na kusababisha kutoleana bastola.

  [/FONT][/FONT][FONT=&amp][FONT=&amp]Uamuzi wa kuenguliwa kwa makada hao wa CCM katika kinyang'anyiro hicho, ambao ulikuwa umeenea miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa chama hicho wilayani Nzega, unadaiwa kuchukuliwa na sekretarieti ya chama hicho kwa maelezo kuwa kitendo walichokifanya kinakiabisha chama hicho.[/FONT]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Habari zinadokeza kuwa, wakati wakijadili hoja hiyo, wajumbe wa sekretarieti hiyo wakiwamo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na John Chiligati walikwenda mbali zaidi kumbana Bashe wakieleza kuwa hana msaada kwa chama hicho, ingawa anaendesha chombo cha habari.
  [/FONT][FONT=&amp]
  Hii itakuwa mara ya nne kwa Bashe kuondolewa jina lake katika kinyang'anyiro cha kusaka uongozi ndani ya chama hicho[/FONT].

  [FONT=&amp]Nape alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa Sekretarieti hiyo haina uwezo wa kuengua majina ya wagombea.

  "Sekretarieti haina mamlaka ya kuengua majina ya wagombea," alisema Nape huku akisisitiza kuwa kama ikifanya hivyo, basi ni kinyume na Katiba ya CCM.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Hata hivyo, kwa upande wake Mbunge Dk Kigwangalah alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa hata yeye anazisikia taarifa hizo, lakini hajapata taarifa rasmi.

  "Siwezi kuthibitisha wala kukanusha kwa sababu mimi siyo mjumbe wa kikao kilichoketi na kufanya uamuzi, labda uwaulize waliokuwepo katika kikao hicho," alisema Kigwangalah na kuongeza:

  "…Sidhani kama nitakatwa, kwa sababu mimi nina uwezo mkubwa wa kuwa mjumbe wa Nec, hata viongozi wangu wanajua uwezo wangu."

  Alipoulizwa hatua atakazozichukua iwapo atapewa taarifa rasmi kuwa ameenguliwa kugombea nafasi hiyo alisema: "Unajua, huwezi kuzungumza habari za mto wakati bado hujauvuka."

  Bashe alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema kuwa, hana taarifa za jina lake kufutwa.
  [/FONT]
  Chanzo: Mwananchi Jumapili 23/09/2012
   
 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Waache wavu wazikane
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Not on Mwananchi Website...
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wafukuzwe na uanachama hao wazee wa miguu ya kuku.
   
 5. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  hainihusu kabisa
   
 6. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  wanawaonea tu! mbona polisi wanaotufyatulia masase hawafukuzwi!
   
 7. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa watoe Bastola vizuri
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Waacheni wazidi kubomoana sisi tupete!!!!
   
 9. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nahisi hilo litakuwa pigo kubwa kwa Dr.Kigangwalla kwasababu atashindwa kumsaidia mtu wake kwenye presidential nomination
   
 10. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli,poa tu!!!Bado wengine!!!tusubiri usaliti baada ya baadhi yao kupigwa panga!!!
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kigwangwala ni fungu la kukosa! Hajawahi kushinda uchaguzi tangu aingie kwenye siasa. Akina Makamba Sr waliokuwa wanambeba hawapo tena. Hata ubunge aliopewa sasa upo mashakani. Tulimshauri asaini fomu ya Zitto akasema anakiamini chama chake. Nadhani anamalizia ubunge akauze duka la dawa maana hawezi hata kutoa tiba.
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hakuna wakusaliti hapo. Wote wamekalia kuti kavu. Mmoja kapewa uraia na mwingine kapewa ubunge. Wakisaliti tu, wanafanywa hamna!
   
 13. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,377
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Safi tuuu...
   
 14. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  MPAKA uchaguzi uishe sijui kama watakuwa wamoja.
   
 15. commited

  commited JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bashe, Kigwangalah wapigwa panga CCM Mwananchi Sunday, 23 September 2012 09:27SEKRETARIETI YADAIWA KUPENDEKEZA WAKATWE,VURUGU ZA NZEGA ZAWAPONZA,WABUNGE,MAWAZIRI SASA RUKSA KUWANIA UONGOZIWaandishi WetuMAKALI ya panga la Sekretarieti ya CCM, yameanza kuonekana baada ya majina ya wagombea wa nafasi ya Halmashuari Kuu (Nec) ya chama hicho kupitia Wilaya ya Nzega, Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Hamis Kigwangalah na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Hussein Bashe kukatwa.Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Dodoma zinaeleza kuwa Sekretarieti ya CCM iliyoketi hivi karibuni, kupitia majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ikiwa chini ya Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama iliamua kuyaondoa majina ya Kigwangalah na Bashe kwa madai kuwa wamekiabisha chama hicho.Habari nyingine kutoka mjini humo zinaeleza kuwa Sekretarieti ya CCM pia imepitisha majina matatu ya watakaowania nafasi ya umakamu mwenyekiti wa UVCCM, Tanzania Bara.

  Wanaotajwa kupitishwa ni pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Wakili wa Kujitegemea Anthony Mavunde, Paul Makonda na Mboni Mhita.Bashe na Kigwangalah waliingia katika mvutano wakati wakichukua fomu ambapo kulitokea malumbano baina yao wakiwa katika Ofisi za CCM, mjini Nzega na kusababisha kutoleana bastola.Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Tabora lilieleza kuwa linaishikilia bastola ya Mbunge Kigwangalah na kwamba, wanafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo. Mbali ya tukio hilo kufikishwa polisi, Kamati ya Siasa ya CCM wilayani Nzega iliketi na kutoa mapendekezo kadhaa, ambayo yalimbana Kigwangalah, ambaye aliibuka na kueleza kuwa hana imani na viongozi hao, akiwatuhumu kuwa wanampendelea Bashe. Uamuzi wa kuenguliwa kwa makada hao wa CCM katika kinyang'anyiro hicho, ambao ulikuwa umeenea miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa chama hicho wilayani Nzega, unadaiwa kuchukuliwa na sekretarieti ya chama hicho kwa maelezo kuwa kitendo walichokifanya kinakiabisha chama hicho.

  Habari zinadokeza kuwa, wakati wakijadili hoja hiyo, wajumbe wa sekretarieti hiyo wakiwamo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na John Chiligati walikwenda mbali zaidi kumbana Bashe wakieleza kuwa hana msaada kwa chama hicho, ingawa anaendesha chombo cha habari.Hii itakuwa mara ya nne kwa Bashe kuondolewa jina lake katika kinyang'anyiro cha kusaka uongozi ndani ya chama hicho.

  Mwaka 2007 wakati akigombea ujumbe wa Nec Taifa, jina lake liliondolewa na baadaye wakati akigombea uenyekiti wa UVCCM, ambapo uchaguzi huo ulifutwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na kuamriwa nafasi hiyo igombewe na watu kutoka Zanzibar.Katika mwaka 2010 wakati akiwania kiti cha ubunge kupitia chama hicho Jimbo la Nzega, jina lake lilikatwa kwa madai kuwa siyo raia.NapeNape alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa Sekretarieti hiyo haina uwezo wa kuengua majina ya wagombea."Sekretarieti haina mamlaka ya kuengua majina ya wagombea," alisema Nape huku akisisitiza kuwa kama ikifanya hivyo, basi ni kinyume na Katiba ya CCM.

  Dk Kigwangalah, BasheHata hivyo, kwa upande wake Mbunge Dk Kigwangalah alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa hata yeye anazisikia taarifa hizo, lakini hajapata taarifa rasmi."Siwezi kuthibitisha wala kukanusha kwa sababu mimi siyo mjumbe wa kikao kilichoketi na kufanya uamuzi, labda uwaulize waliokuwepo katika kikao hicho," alisema Kigwangalah na kuongeza:

  "…Sidhani kama nitakatwa, kwa sababu mimi nina uwezo mkubwa wa kuwa mjumbe wa Nec, hata viongozi wangu wanajua uwezo wangu."Alipoulizwa hatua atakazozichukua iwapo atapewa taarifa rasmi kuwa ameenguliwa kugombea nafasi hiyo alisema: "Unajua, huwezi kuzungumza habari za mto wakati bado hujauvuka.

  "Bashe alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema kuwa, hana taarifa za jina lake kufutwa.Mbali na Bashe na Kigwangalah, sekretarieti hiyo pia inadaiwa kukata majina ya makada wengine waliokuwa wakiwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kutokana na kukumbwa na kashfa mbalimbali.Tayari uchaguzi huo ndani ya CCM umegubikwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya makada wakidai kuwa kuchezewa faulo, huku majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali yakijadiliwa na kikao cha Nec mjini Dodoma.Mmoja wa makada hao ambaye ni Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono anayegombea nafasi ya uenyekiti Jumuiya ya Wazazi Taifa, ambaye jina lake linadaiwa kukatwa katika ngazi ya mkoa na kuonya kuwa kama hiyo itafanyika basi patachimbika.Kada mwingine ambaye ameunyooshea kidole uchaguzi huo ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye juzi alikaririwa akisema kuwa chaguzi zinazoendelea ndani ya CCM, zimevurugika kwa kuwa mafisadi wameingilia na kuweka watu wao kwa lengo la kulinda masilahi yao.

  Alisema kuwa watu waliojitokeza kugombea ni mapandikizi na vibaraka wa mafisadi hao."Hivi karibuni tumepata aibu kubwa ndani ya chama chetu, wakati chaguzi zetu zikiendelea, viongozi wamepitisha vipaza sauti vya mafisadi, kazi yao kubwa ni kulinda masilahi ya mabwana zao na kuwafurahisha," alisema Sitta.Kujirundikia vyeo ruksaKatika hatua nyingine, mkakati wa CCM wa kuondokana na baadhi ya wanachama wake na kujirundikia vyeo umeonekana kugonga ukuta baada ya chama hicho kueleza kuwa, busara zinahitajika zaidi kuliko uhalisia ili mkakati huo uweze kufanya kazi.

  Hali hiyo ya imekuja wakati ambapo chama hicho kupitia vikao vyake vya juu, kiliwahi kutangaza kuwa watu wenye nafasi nyingine wakiwemo wabunge, madiwani na mawaziri, hawataruhusiwa kugombea nafasi zaidi za uongozi ndani ya chama.Akionyesha kuwa chama kimebadili msimamo huo ulio kwenye Katiba yake, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu wabunge na mawaziri kugombea nafasi za ujumbe wa Nec, huku wakiwa wana shughuli zingine."Ni kweli, tulipanga kufanya hivyo na hilo siyo geni, lakini kumbukeni nia ya chama chochote ni kushinda na kushika dola hivyo tukisema kwamba tukate majina ya kila mtu hatutakuwa tumetenda haki, tunaweza kujiangusha sisi,'' alisema Nape.Alisema kuwa wako watu ambao ni muhimu kwa chama na kuwa, kuwaondoa katika nafasi zao inaweza kuwa ni tatizo kwa CCM na wananchi wanaowazunguka.Katibu huyo alisema kuwa kwa namna yoyote, wako mawaziri na wabunge watahitajika kuteuliwa na kugombea kutokana na umuhimu wao ndani ya chama na kuwa CCM haiwezi kuwatema.

  Akitoa mfano alisema kuwa Dann Makanga aliyehama kutoka chama cha UDP na kujiunga na CCM, aliteuliwa kwa wakati huohuo kuwa mgombea na alishinda, uamuzi ulioonyesha kwamba asingeteuliwa kungekuwa na madhara.Mpango wa CCM kuzuia wanachama wake kujirundikia vyeo, ulilenga kuwazuia kugombea nafasi zaidi baadhi ya watumishi wa Serikali, wanaokuwa na majukumu ya kila siku, ili kutoa nafasi kwa wajumbe wengine kukitumikia chama hicho kwa uaminifu na uadilifu.Kuhusu uamuzi wa kukatwa majina, Nape alisema kuwa CCM haina kigugumizi na hilo akitolea mfano wa waliokuwa wagombea wa Uenyekiti wa Mkoa wa Mara, Chambili na Gachuma, aliosema majina yao wote yalikatwa na kutangaza nafasi hizo upya.

  Akizungumzia ratiba ya vikao vinavyoendelea kiongozi huyo alisema kikao cha Kamati ya Maadili juzi hakikumaliza shughuli zilizopangwa kufanyika, hivyo kuendelea jana asubuhi.Alisema hali hiyo ililazimu kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichopangwa kufanyika jana asubuhi kisogezwe hadi jana jioni.Kikao cha CC kinatarajia kukamilika leo kabla ya kupisha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kitakachofanyika kwa siku mbili kuanzia kesho na kutoa mapendekezo ya mwisho, kabla ya kufanya uteuzi wa wagombea.
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Wanagombana bure tuu kuwania ujumbe wa NEC kwa chama ambacho mwaka 2016 uwezekano wa kuwa hai ni mdogo. Tatizo ni kuwa CCM haijajiandaa kuwa chama cha upinzani hivi kukilazimisha kuwa hivyo kinaweza kufa kwa mshtuko.
   
Loading...