Bashe: CCM ni waoga, wanafiki na wa kujipendekeza, hatuna sababu ya kuendelea kubaki madarakani

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Akichangia kwenye bajeti ya mali asili na utalii amewaambia wabunge na serikali kuwa hawajawahi kuweka malengo haswa ya kutatua matatizo ya wafugaji na wakulima, wamekuwa waoga, wanafiki na wakujipendekeza

Ameongezea CCM kwa wingi wao hawana sababu ya kuendelea kubaki madarakani kama wameshindwa kuishauri serikali kwa ukweli.

 
Ameongea ukweli hata hivyo ukisikiliza video utagundua heading ya thread yako inapotosha kidogo. Tatizo la haya mabunge ya commonwealth countries, party caucus zinawafanya wabunge kuwa wanafiki.

Mbaya zaidi inakuja pale serikali haitimizi wajibu wake au viongozi wake ni mzigo. Wabunge itabidi tu waitetee serikali kutokana na party caucus zao. Vivyo hivyo hata kwenye upinzani inabidi tu waitetee serikali yao kivuli hata kama haifanyi vizuri.

Unakuta wabunge wote wanakubaliana kwenye masuala yanayowagusa wao lakini hawakubaliani kwenye masuala yanayovigusa vyama vyao. Hakuna hata general consensus kwenye masuala ya kitaifa. Bashe anaweza kuongea hivi lakini inapofika wakati wa kupitisha bajeti ya serikali inabidi tu apitishe kwa sababu ya maelekezo kutoka kwa mkuu wake wa party caucus yake.

Party caucus ndani ya bunge zinakuwa na faida kwa taifa kama serikali iliyoko madarakani inakuwa active, inasikiliza na kujisahihisha haraka na pia iko tayari kuwatumikia wananchi wengi.
 
Ameongea ukweli lakini tatizo la haya mabunge ya commonwealth countries, party caucus zinawafanya wabunge kuwa wanafiki.

Mbaya zaidi inakuja pale serikali haitimizi wajibu wake au viongozi wake ni mzigo. Wabunge itabidi tu waitetee kutokana na party caucus zao. Vivyo hivyo hata kwenye upinzani.
hata hapa jukwaani kuna watu wanapost upumbavu wa kuitetea serikali hadi unashangaa hawa wana brains kweli?
 
Huyu jamaa kaongea vizuri sana, CCM wanahitaji wabunge kama hawa, wabunge wanaoweza kusema hapana kwa ajili ya Taifa. Issue za zidumu fikra za chama sio wakati huu ambapo dunia iko kwenye utandawazi, watu wanaupeo na fikra nyingi, kwani wabunge wa CCM wangekuwa vile mbona tungekuwa na ahueni, wabunge wengine wa CCM pia wanatakiwa wabadilike.
 
Hii ndiyo sampuli anayoipenda Magurfuli. Inaonekana anaweza kudhubutu kufanya jambo jipya. Ni kijana sana,msomi, hategemei ubunge kama chanzo cha kipato chake, ana uwezo wa kumwambia mfalme kuwa uko uchi. Hawezi kumaliza 5yrs bila kuwa serikalini. WAMA tumbo joto
 
Huenda Bashe ni msikilizaji mzuri wa hotuba za hayati Baba wa taifa hasa ile anayozungumzia mabadiliko ya dhati ndani ya CCM. Hongera Bashe ila chunga wasikukolimbe kwa kuwaambia ukweli kwani CCM walio wengi hawaupendi.
Ni ukweli usiopingika kuwa kuongoza kwenu ni kwa kulazimisha mno na mnaongoza miili badala ya mioyo ya wananchi. Hamstahili na mlitakiwa muongozwe ili mjifunze.
 
Tena hao CCM wanafiki sana linapokuja suala la
masilahi ya umma, na ndani ya CCM hakuna mtu aliyecommited kuwa hudumia wananchi , lakini sio wabunge wa CCM tu hata wapinzani wa kiasi fulani huungana kwa masilahi ya chama kuliko kuwahudumia na kutatua kero za wananchi. CCM na Serikali wafanye kazi ya kutatua matatizo ya wakulima na wafugaji waache mazoea.
 
Lazima awe hivyo kwani ana chembe chembe nyingi Za Mzee Lowassa hawa ni vijana wake alio waacha mtaa wa pili!
 
Back
Top Bottom