Basena out Simba SC

Hilo ni tatizo la kitaifa, Japokuwa naipenda yanga, Kulikuwa na sababu mbili zilizosababisha simba kufungwe, Ya kwanza, Simba walikuwa katika naafasi nzuri ya kushinda. Simba walilijua hilo, Yanga tulilijua pia. Katika hali ya aina hii, kufungwa ni rahisi sana kwa kutumia saikolojia. Overconfidence ni hatari. Tulijua ni rahisi kutumia saikolojia. Tukamyoa myama.

Pili, Lile goli kwa kadiri ya Mfungaji, Mwapeeeeee! Ni goli La Mungu. Ni neno kubwa. Ni goli la bahati. Na ni bahati tu. Hakuna jingine ni BAHATI Kwani hakukuwa na jitihada upande wa ufungaji. Alicheza sana Niyonzima. Hakufunga. Mfungaji alikwishaitwa ili abadilishane na TEGETE. Wakati anangojea mpira, Malaika wa bwana akamletea mpira mguuni. Mungu akupe nini. Simba wangelikuwa na akili, wangetulia. Mechi ya pili wangelifanya vizuri.

Kwa maamuzi waliyoyachukua, hawatatulia na watachapwa mwako 2012 wote. Watatulia 2013 kwani uongozi utaendelea na mazobezobe. Ni hatari kitaifa kwani soka linadumaa kwa ubumbavu wa viongozi. Bora ingelikuwa Ujinga.
 
Jamani Basena kafiwa na mama yake mzazi leo. Kutimuliwa kwake hakujathibitika bado.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom