figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,681
- 59,181
BASATA wametoa siku saba kwa wamiliki wa wavuti, na wale wenye akaunti kwenye mitandao ya kijamii Kuondoa nyimbo zenye kusambaza chuki,matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji wa watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasiasa.
Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, amevitaka pia vyombo vya habari ikiwamo redio, luninga, kuondoa na kuacha mara moja kucheza au kurusha nyimbo zote zenye maudhui hayo.
============================
Update kwenye Magazeti;
Chanzo: Mwananchi
Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, amevitaka pia vyombo vya habari ikiwamo redio, luninga, kuondoa na kuacha mara moja kucheza au kurusha nyimbo zote zenye maudhui hayo.
============================
Update kwenye Magazeti;
Dar es Salaam. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii, wamiliki wa wavuti, na wale wenye akaunti kwenye mitandao ya kijamii kuondoa nyimbo zote au maudhui yenye mwelekeo unaoenda kinyuma na maadili, matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji wa watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na kitaifa.
Taarifa ya Basata iliyotiwa saini na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza umevitaka pia vyombo vya habari ikiwamo redio, luninga, kuondoa na kuacha mara moja kucheza au kurusha nyimbo zote zenye maudhui hayo.
Mngereza alisema kuwa maudhui ya kashfa, matusi, kejeli, udhalilishaji zinatishia kuigawa jamii ya Watanzania katika kipindi hiki ambacho taifa linaendelea na kampeni za kisiasa na kujiandaa na uchaguzi mkuu.
Alivitaja kifungu namba 118 (a-d) cha Sheria ya Bunge namba 9 ya Mawasiliano ya Mtandao ya mwaka 2010 vinaeleza kuwa ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza, kuzalisha, kusambaza au kutangaza ujumbe ambao una mlengo wa matusi, dharau, uzushi au jinai kwa lengo la kutukana, kutisha, kusumbua au kushusha hadhi ya mtu mwingine.
Alisema Sheria ya Bunge namba 4 ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 45 (1) (a-c) kinatoa mamlaka kwa taasisi au mtu yeyote anayebaini uvunjifu wa sheria katika mitandao kutoa notisi kwa yeyote yule anayesambaza au kutangaza ujumbe au maudhui yanayovunja sheria za nchi kuacha mara moja au vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote anayekaidi.
Kwa msingi huu, Basata linawaagiza wasanii wote nchini kuacha mara moja kubuni na kutengeneza kazi za sanaa zenye kuashiria kuigawa jamii katika misingi yoyote ya kibaguzi na zaidi kutumia sanaa kubomoa jamii badala ya kuijenga, alisema Mngereza.
Aitumia taarifa hiyo pia kuwasisitiza wamiliki wa vyombo vya habari wakiwamo wa radio na luninga na watangazaji kuhakikisha hawawi chanzo cha kusambaza maudhui yoyote ya sanaa yenye mlengo wa kuibua chuki, matusi, kashfa na mgawanyiko wa taifa.
Chanzo: Mwananchi